Je ni haki kufukuzwa kazi au kulipwa nusu mshahara iwapo umepewa bed rest wakati wa ujauzito? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni haki kufukuzwa kazi au kulipwa nusu mshahara iwapo umepewa bed rest wakati wa ujauzito?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Geen, Oct 28, 2011.

 1. Geen

  Geen JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 287
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wanaojua naomba mnijuze kuhusu hili maana limemtokea rafiki yangu
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Ungepata ushauri mzuri na wa uhakika zaidi kama ungetoa detaills zaidi kuhusiana na kadhia hiyo. nijuavyo mimi, kwa kawaida ujauzito haupaswi kubadilisha terms (eg mafao, cheo au ajira yenyewe) of employment to the detriment ya mwajiriwa.
   
 3. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuna haja ya kuangalia lakini wakuu, mimba zingine tata sana, labda binti kapewa bed rest tangu mwezi wa kwanza wa mimba, sasa ukichanganya miezi 9 ya ujauzito na ile mitatu ya maternity lazima boss macho yasogeleane!
   
 4. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Taarifa hazitoshelezi. Huyo mjamzito ana masharti yepi ya ajira? Mara ya mwisho alipewa lini maternity leave? Ameruhusiwa kukaa nyumbani kwa sababu ya ugonjwa au alijiruhusu mwenyewe?
   
 5. Geen

  Geen JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 287
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mjamzito amepewa bed rest kuanzia mwanzo wa ujauzito kulingana na masharti ya daktari,alilazwa kabisa baadae akaruhusiwa kurudi nyumbani lakini asiende kazini miezi yote tisa
   
 6. Geen

  Geen JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 287
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mwajiriwa hajawahi kuchua maternity leave,hii ni mimba ya kwanza
   
 7. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hapo kuna tatizo, wataalam wa mambo ya Utumishi watatoa ufafanuzi.
   
 8. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ameajiriwa Serikalini au kwenye Taasisi binafsi?

  Alichukua likizo ya ugonjwa?

  Ana umri gani kazini?
   
 9. Geen

  Geen JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 287
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ana mwaka kazini,alikuwa akipelewa vyeti ya daktari vyote kazini kuonyesha anatakiwa kupumzika
  Anafanya taasisi binafsi
   
 10. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Msaidie kupata ushauri kutoka kwa Katibu wa chama chake cha wafanyakazi kabla ya kwenda kwenye usuluhishi.
   
 11. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  View attachment 40245
  Duh, kama kweli anaumwa nampatia pole, lkn kama anachukulia mimba kama kigezo cha ku-dodge kazini kwa kuwahonga hao wanapjiita ma"Dr." ujue anajiharibia - hakuna mwajiri anayependa mtumishi mvivu. Wanaweza kutafuta kila njia il wamwachishe kazi hata kwa kumtega ili afanye kosa then wale kichwa kisheria! Awe makini.
  Kisheriawanaweza kuwa sahihi au wanakosea wanapomkata salary, inategemea HPI (history of presenting illness) yake! Ah, sorry, nilifikiri niko hospitali nam-attend mgonjwa! I meant inategemea na undani wa case yake (details zaidi zinatakiwa kuweza kumshauri).

  Refer: Employment and Labour Relations Act, 2004; Part III (Employment Standards); Sub-part D (Leave);Section 32 (Sick Leave) and 33 (Maternity Leave.

  Mimi naona wako sahihi kama amekaa nyumbani kwa siku 63 za mwanzo ambazo mwajiri amemlipa 100% ya salary, akaongeza tena siku zingine (0-63 days = 126 in total) mwajiri amemlipa 50% ya monthly salary, provided kwamba hizo 0-63 days za pili hazigusi commencement ya maternity leave. Ambapo maternity leave ni 84 days. Akiendelea kuleta uzembe (kama anachezea ajira, WATAPIGA CHINI!). Someni sheria. Wanasheria watasaidia zaidi. I am not a lawyer, though I am among the BIG THREE in the world, (DOCTORS, Lawyers and Clergy)
   
 12. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli sheria hii inamruhusu mtumishi kulipwa mshahara wake wote iwapo ataugua kwa muda wa siku 63 baada ya hapo ni nusu mshahara .Baada ya miezi sita atamuondoa kazini kabisa.Hii ina apply kote kwa makampuni binafsi na hata serikalini.
   
 13. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #13
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  sawa sawa, hapa kuna kaujanja kanafanyika. kama anataka aombe likizo ya bila malipo itayaoishia tarehe anayotegemea kujifungua.
  ili akirudi tu kazini alambe na maternity leave. japo inavyoonekana ameshindwa kuimanage hii situation vizuri.
   
Loading...