Je, ni busara kupima UKIMWI kama siumwi na chochote?

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,232
2,000
WADAU wa JamiiForums naomba USHAURI wa bure kutokana na kadhia hii.

Mabwana afya wanasisitiza watu kupima afya zao hasa kupima maambukizi ya gonjwa hatari la UKIMWI na uishi ukijijua afya yako. Ikibidu uanze kumeza mawe.

Leo katika pita pita zangu nilikutana na mdau mmoja katika mazungumzo ya hapa na pale tukagusia suala la kupima kwa hiyari. Yeye binafsi anasema alishawahi kufanya hivyo na yupo salama.

Sasa nikifiria upande wangu nimekuwa mtu wa kuuza mechi kila kukicha. Aisee hivi ni busara kweli kupima na kujijua?

Ama nikaushe mpaka pale ambapo mambo yatakapokuwa wazi?

NAOMBA USHAURI WENU.

NB.
Katika maisha yangu sijawahi kupima zaidi ya uzito, malaria na U T I.

USHAURI tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,430
2,000
Kausha tu mpaka pale mambo yatakapokuwa wazi
Akikuta amechelewa mashambulizi yamekuwa makali kiasi kinga zimezohofu kabisa unafikiri nini kitampata..?

Nachomshauri aangalie ushauri wa wataalum na analotaka kulifanya lipi litakuwa na manufaa kwa afya yake.
 

financial services

JF-Expert Member
May 17, 2017
8,508
2,000
Naona ni vizuri kujua mapema kabla haijawa too late, Kwani kiuhalisia ni kwamba kama ugonjwa upo ni upo tu and vice versa is true,so usipofahamu ni kwamba unajichelewesha tu.

Ila kupima nako ni shughuli aisee, hasa ukiwa unasubiri majibu upo nje, ukimuona doctor katoka kamoyo kanarukaa huku unasali sala zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Baraja

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
1,203
2,000
Mzee wa Kusawazishaaaa, njoo uone Kasumba za mzee mwenzio hukuu.


Kuna mdada mmoja alinisimulia, alipokuwa mjamzito wa mtoto wake wa pili, ikawa anatakiwa akapime. Akamwambia daktari bana ee, mi nilishapima mimba iliyopita, daktari akamwambia hiyo ni mimba iliyopita, hapa unatakiwa upime upyaaa, yule mdada jasho la jino lilimtoka ananiambia.

Kaenda kupima, ile kumaliza hakusubiri majibu akasepa. Ilibidi daktari ampigie simu afuate majibu yake, akamuuliza kwenye simu, vipi yupo fresh au kaungua!? Jamaa akamwambia asiogope yapo fresh, pamoja na hivyo hakwenda kuyachukua. Akanisimulia ya kaka yake sasa, nilicheka mno
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
50,013
2,000
Ni hivi, ukipima mapema tena ukiwa bado na nguvu zako na ukutwe ve+
1. Kufubaza haraka virusi na wewe kuendelea na maisha yako.

2. Kutoambukiza wengine na ukaishi maisha yako kama kawaida.
 

Pist_Sr

Member
Mar 6, 2020
75
125
Ni hivi, ukipima mapema tena ukiwa bado na nguvu zako na ukutwe ve+
1. Kufubaza haraka virusi na wewe kuendelea na maisha yako.

2. Kutoambukiza wengine na ukaishi maisha yako kama kawaida.
Mwambie na upande wa pili wa shilingi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom