Je, Ni busara kumwambia mumeo kama ananuka mdomo?

zen

Senior Member
Feb 6, 2016
106
94
Hala!

Natumai mpo wazima kama title inavosema, je unawezaje kumwambia mumeo au mpenzi wako kama anaharufu mbaya ya mdomo na inakukera sana wakati wa tendo la ndoa?

AU VIPI NAWEZA MSAIDIA BILA YEYE KUJUWA AU KUMWAMBIA ILI ASIJISKIE VIBAYA?

Ushauri wenu please.
 
Mimi kuna kipindi jino lilianza kulika ndani na sikuwa najua, harufu ya mdomni ikawa kali bila mwenyewe kujijua. Wife aliniambia bila kumung'unya maneno, namnukuu "Aka mwenzangu mdomo wako unanuka siku hizi, osha kinywa vizuri" nilicheka tu ikabidi nianze kutwa mara tatu mswaki, lakini wapi hadi ilipogundulika baadaye ni jino. Kwa hiyo kama sio wewe wa kumwambia, nani amwambie?? Akimind atakuwa bado pre matured.
 
Hala!natumai mpo wazima...kama title inavosema je unawezaje kumwambia mumeo au mpenzi wako kama anaharufu mbaya ya mdomo na inakukera sana wakati wa tendo la ndoa ?AU VIPI NAWEZA MSAIDIA BILA YEYE KUJUWA AU KUMWAMBIA ILI ASIJISKIE VIBAYA?ushauri wenu pls.
mwambie twende wote tukapige mswaki
 
NI vizuri kumwambiaili wewe ne yeye msiteseke

KUnuka mdomo ni ugonjwa kama magonjwa mengine
 
Kwani kuna v2 ambavyo huwezi kumueleza mtu ambae mpo kwny ndoa km unaona ni tatizo?!....mbona issue ndogo tu
 
Mwambie hakuna tatizo,ila mwambie kwa ustaarabu.
Ukimwambia atatafuta matibabu.
Binadamu hatujakamilika kuna wengine wananuka mdomo,wengine vikwapa,wengine wanatoa harufu sehemu nyeti nk.
Ukimpenda utamwambia na yeye atatafuta matibabu ili hiyo hali isiendelee.
Mimi binafsi napenda mtu aniambie ukweli kuliko akae kimya.
 
Kupiga mswaki siyo suluhisho unaweza kupiga mswaki na mdomo utaendelea kunuka.

Kweli kabisa.

Kupiga tu mswaki si suluhisho.

Suluhisho bora ni usafi wa kinywa kwa ujumla wake na utanabahi kuhusu hatua za huo usafi.
 
Dah!!! Yaani kama nakuona vile wakati wa tendo kama ni kama vile unabakwa au mnabakana kwa jinsi unavyojitahidi kumkwepa kinywani.....haina jinsi ni bora kumwambia ili muwe mnafurahia tendo...
 
Muambie kwa upendo aende kwa daktari wa meno. ukimshawishi na kumsindikiza, huko atapewa ushauri na jinsi ya kutunza kinywa pia. kuna umuhimu wa kusafishwa meno hospital kila mwaka kutoa uchafu uliogandamana

Kumbuka kubadilisha mswaki kila baada ya miezi 2.
 
Hala!natumai mpo wazima...kama title inavosema je unawezaje kumwambia mumeo au mpenzi wako kama anaharufu mbaya ya mdomo na inakukera sana wakati wa tendo la ndoa ?AU VIPI NAWEZA MSAIDIA BILA YEYE KUJUWA AU KUMWAMBIA ILI ASIJISKIE VIBAYA?ushauri wenu pls.


Huyo mme lazima awe juha sana kwa sababu katika hali ya kawaida, angerahia kukosolewa na mkewe kabla hajajichora kwa watu. Ni sawa na mke kuogopa kumwambia mmewe hajafunga zipu ya suruali kwamba atajisikia vibaya aendelee kutembea akiwa uchi?

Lipi jema kuambiwa na mkeo tatizo lako ili mlitafutie suluhu au kuachwa uutembee nalo hadharani?

Na wewe mwanamke, lipi jema, kumwabia ukweli mmeo ili afahamu au kumwambia uwongo ili atembee katika huo uwongo huku jamii ikimcheka na yeye asijue. Huu ni uuaji na hufai kuwa mke.

Na wewe mwanamme, kipi chema kuukubali ukweli kutoka kwa mkeo na kuufanyia kazi, au kuukubali uwongo wa hadaa kwa mkeo lakini utembeapo katika jamii unaonekana kituko?

Honesty is the best policy!. PERIOD!
 
Back
Top Bottom