Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Biashara ni kipaji na si wote wanaweza kufanya biashara na kufanikiwa kwa kiwango kile anachokitamani.Kuwekeza fedha kwenye biashara kuna kupoteza au kufanikiwa.Kwa wale ambao hatuna uzoefu au kipaji kwenye biashara huwa tunakimbilia kwenye ujenzi tukiamini kule hela haipotei hata kama hakutakuwa na faida.
Pia inategemea na chanzo cha fedha au mtaji;kwa mfano ukiangalia wanaojenga viwanda,hotel n.k kwa asilimia kubwa wanatumia mikopo..na wanaamini hata wakishindwa kurejesha mikopo hiyo lile jengo litatumika kama 'bond'.Kwa hiyo inategemea na kipaji cha mtu husika katika biashara.
 
Just imagine alienunua kariakoo nna kujenga nyumba akiuza saivi ana make mkwanja gani

Kwetu tulinunua kiwanja laki 4 hapo dar wilaya ya ubungu 1994 tulianza kujenge mdogomdogo haki ikawa nyumba kubwa enzi hizo hili eneo lilikuwa nyumba moja moja Ila leo zimekuwa nyingi Hadi biashara zinatembea kweli just imagine tukiuza hiyo nyumba leo tuna kiasi gani

Cost za ujenge wa nyumba na thamani ya kiwanja muda ule hata 15 milioni sidhani Kama inafika Ila leo tunaweza una hio nyumba sio chini ya 50m maana sio ya kisasa sana



Sent using Jamii Forums mobile app
1994-2020 = 15m-50m?
 
Ukitaka kufaidi biashara ya guest nenda ikwiriri tengeeza guest za kawaida za 10000
Nimekuwa nasafiri sana kwenda ikwiriri sijawahi pata guest bila kuweka oda. Ikifika satatu waweza kuzurura mji mzima mwisho ukalala stendi
Ikwiriri ndo wapi?.
 
Nyumba ya kuishi muhimu mana usijekuwa mpangaji milele...

Ila kwa ajili ya kujiongezea kipato ni bora kwa sasa kudeal na huduma zinazohitajika na kuingiza pesa walau kila siku mfano chakula na usafiri
 
Nitarudi kuchukua madini

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyumba sio biashara inayolipa sasa hivi. Hats ukijenga guest hamna wageni wa kulala. Unaweza kupata wageni 2 au 3 na gharma ya uendeshaji haipungui iko fixed. Guest nyingi zimefungwa au zinaendeshwa kwa hasara tupu. Japan wamefika mahali Serikali inawapa wananchi nyumba za bure .vizazi vimekuwa vikijenga tangu karne kadhaa sasa imefika mahali idadi ya nyumba imezidi watu. Ndio maana hata utajiri wa Trump hauongezeki kwa sababu biashara ya majengo aliachiwa na baba yake tena nyumba zake ni prime area kama k/koo au msasani lakini bado anasttuggle vijana zuckerburg wanatoboa kwa sababu ya nature ya biasjata inayoenda na kizazi husika.
 
Wahindi hawaangaiki Kujenga mapagala Mapinga na Mbweni. Wanajibana nyumba za NHC/Msajili huku akaunti zimetuna. Mbongo anajenga squatter Buza kutwa kulalamika maisha magumu, anapeleka mtoto shule za kayumba mwishowe mtoto anakuja kuwa Mpiga debe, dereva wa daladala, kibarua viwanda vya wajindi au saidia Fundi
 
Wahindi hawaangaiki Kujenga mapagala Mapinga na Mbweni. Wanajibana nyumba za NHC/Msajili huku akaunti zimetuna. Mbongo anajenga squatter Buza kutwa kulalamika maisha magumu, anapeleka mtoto shule za kayumba mwishowe mtoto anakuja kuwa Mpiga debe, dereva wa daladala, kibarua viwanda vya wajindi au saidia Fundi
hahahahaha umewaponda wabongo sana
 
Back
Top Bottom