Je, ni biashara gani Mtanzania anaweza kuifanya nje ya nchi (export)?

Paul S.S

JF-Expert Member
Aug 27, 2009
6,402
3,242
Mara nyingi najiuliza hili swali hivi sisi hapa Tanzania ni bidhaa gani tunaweza kuuza nje ya nchi ukiondoa biashara ya Ng'ombe,Mbuzi, Vitunguu tunavyopeleka Comoro? Kuna nchi wachovu tu kama sisi lakini zina uza sana mboga mboga, maua,pilipili, asali/nta,ndege,unga wa mahindi/mtama, mbuzi/kondoo vikapu,vinyago nk nchi za Uarabuni,Ulaya hadi USA

Hivi ni wapi naweza kwenda nikapata mwongozo mzuri wa kupata masoko ya bidhaa zetu za kawaida kabisa ukiondoa biashara za minofu ya samaki,madini, magogo inayohitaji huge capital na inafanywa na vigogo mafisadi

Ukiangalia kiundani utaona ni kama hatuna ubunifu sana wa biashara tunabaki kuigana tu, ukizunguka mji mzima biashara ni zile zile, yaani mtu unabiashara jina tu lakini kiukweli hazilipi kivile

Kuna haja ya kufikiria nje ya box, tufikiri kuvuka mipaka , issue hapa ni kujua masoko yalipo tu na na namna ya ku handle mzigo wako, mfano kama una export mboga mboga au matunda lazima kunakuwa na namna ya kuhandle ili vifike vikiwa fresh
Tusiishie kwenda Dubai, Hong Kong na China tu ku import nadhani tunao uwezo wa ku export pia kama tutatumia njia wanayotumia kuimport.

Nakaribisha mawazo na changamoto za ugumu wa kuikabili biashara hii, ila tukiamua tunaweza

PIA, SOMA:

Mkuu

You have a point, market ya europe na sehemu nyingine inatushinda kwasababu ya quality ya bidhaa zetu especially branding na packaging

Nashauri labda tujikite na semi-processed products halafu hao wazungu wakaumize kichwa kwenye brand name na packaging, imagine ukianza kununua asali ulkaipack kwenye madumu ya liter 200 uka export kama semi processed honey bee? au ngozi zilizo safishwa,, au semi-processed wood/timber and so many to mention

There should be a way forward and this is the right time

This is a very good thread
 
Mkuu International Business ni biashara ngumu sana inayo hitaji kujipanga sana, ni tofauti sana na Domestic trade,

Kwa upande wa Bidhaa za ku export nje ziko nyingi sana ila kuna matatizo kadha wa kadha kama ifuatavyo

1. Quality- Mkuu kuingiza bidhaa Ulaya au Marekani si kitu cha mchezo kabisa hasa vyakula na ndo maana Ulaya na marekani tunauza Vinyago pamoja na Pamba, hii ni kutokana na sheria kari sana za maswala ya Ubora ili kuwalinda wananchi wao
- Kwenye swala la matunda kuna soko huko but kumeet quality standard yao ndo kazi pevu sana

2. Quantity- Mkuu quantity nayo niatatizo kubwa sana, kunawatu wengi wamepata masoko lakini kwenye quantity imekuwa kazi sana,kuna jamaa yangu alipata soko la mafuta ya alzeti lakini alishindwa kwa sababy ya qiantity, wanaweza kuambia wanataka tani laki 5 za mafuta ambayo hayajasafishwa ya alizeti, utazitoa wapi
- Mara nyingi qunatity nayo ni kikwazo kikubwa sana make wanataka in volume so inawawia vigumu kusaply

3. Competition- Tambua kwamba ukipata soko mfano la Matunda huko ulaya unakwenda kushindana na nchi za ASIA ambazo zinasifika kwa kulima matunda sana na mbogamboga, au unashindana na wakulima wa huko huko ulaya na asia

4. Vikwazo vya kibiashara- Kuna vikwazo vingi sana kwa upande wa kibiashara, mfano Jumuia ya ulaya wao wanalinda wazalishaji wao so wanaweka sheria kari sana na kodi kubwa kwa wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya jumuia ya ulaya. marekani nayo ni hivyo hivyo,
-Ila Wanachama wa Jumuia ya ulaya wao wanauza bila shida ndani ya jumuia yao ni kama ilivvo kwa East Africa comunity

5. Ghalama za uzalishaji - Ghalama za uzalishaji huku Bongo ziko juu mno kiasi kwamba inakuwa vigumu ku export na still umeki profit,

- Kuhusu masoko, mkuu mara nyingi masoko unatakiwa utafute mwenyewe na usitegemee serikari ndo ikutafutie masoko na,

MASOKO YA NJE YANAWEZA PATIKANA KUPITIA NJIA HIZI

1. kupitia maonyesho mbalimbali ya kibiashara yanayo fanyika katika nchi hizo- haya maonyesho mara nyingi yanakutanisha wauzaji na wanunuzi so ndo moja ya maeneo mwafaka ya kupata masoko,

2. Kupitia website za kibiashara za makampuni mbalimbali

3.Ziara binafisi ya wewe mwenyewe kwenda kutafuta masoko, kwani hata wao huwa wanakuja kutafuta masoko huku kwetu directilly
 
Soko la ulaya na marekani ni zuri lakini kuna masoko mengine yanafaa tu kibiashara, tunaweza uza sukari mchele mahindi kenya uganda rwanda burundi hata sudan ya kusini, tunaweza export investments pia mfano CRDB wanaweza fungua matawi nchi za nje kama Msumbiji Sudan ya kusini Burundi Rwanda Congo, Mzee Mengi anaweza jenga kiwanda cha coca cola Lubumbashi hivyo wigo wa ajira kwa watanzania ukatanuka na makampuni hayo yakarudisha faida nchini.

Tanzania ingeanzisha dirisha maalumu la kuwasaidia wafanyabiashara wakubwa wanaotaka kufanya biashara za kimataifa, Mtanzania anaweza agiza bidhaa china kwa lengo la kuziuza Congo, Sudan ya kusini, Msumbiji, Zambia na Zimbabwe.

Bidhaa kama Whitedent na Kandambili za Tz zinasoko kubwa sana zimbabwe na Botwana. Mabeseni na ndoo za plastic zinahitajika sana Angola. Kimsingi nchi za Africa zinaweza fanya biashara zenyewe kwa zenyewe kwa kutizama soko lililopo.

Nilimsikia waziri mmoja wa kenya akisema pamoja na watanzania kuzuia mahindi lakini wakenya hawakufa njaa! maanayake tunaweka taratibu ambazo hazinamanufaa na hazitekelezeki.

Kagame aliwahi sema mipaka yetu inawazuia wanyankole wanaohama na Ng'ombe tu wafanyabiashara na watu wenye uwezo wanapita bila wasiwasi wowote. Ukienda Kibirizi, Kabanga, Rusumo,Mtukula, Sirari na namanga bidhaa zinapita mchana na usiku kwa punda, pikipiki, michomoko, fuso na hata muda mwingine wapagazi hukodiwa. Sasa kwanini tusiweke taratibu za wazi watu wakafanyabiashara na kodi ikalipwa pasipo shaka.
 
@komandoo, kuhusu quantity nafikiri wafanyabiashara wafikirie kuunganisha nguvu na sio kuwa wabinafsi. Kama zinahitaji litres 5 kwa mfano wakati mimi naproduce tatu, kwa nini nisitafute mzalishaji mwingine ambae anaweza kuzalisha mbili ili tuweze kuexport!? Huyo mtu angeweza kufanya hivyo na suala la quantity lisingekuwa kikwazo.
 
mkuu

you have a point, market ya europe na sehemu nyingine inatushinda kwasababu ya quality ya bidhaa zetu especially branding na packaging

nashauri labda tujikite na semi-processed products halafu hao wazungu wakaumize kichwa kwenye brand name na packaging, imagine ukianza kununua asali ulkaipack kwenye madumu ya liter 200 uka export kama semi processed honey bee? au ngozi zilizo safishwa,, au semi-processed wood/timber and so many to mention

there should be a way forward and this is the right time

this is a very good thread
Semi processed products inamaana kwao inaweza kuwa ni raw materials?
 
  • Thanks
Reactions: LAT

Mkuu hapo kwenye red, Tatizo ni kwamba tunasumbuliwa na kiasi, umesahau kwamba Tanzania sukari haitutoshi? umesahau kwamba wakina mohamed entrprises wanaagiza sukari kutoka brazil? hiyo ya kuuza Sudani inatoka wapi? au tuagize Brazil then tupeleke sudani?
Hata swala la mahindi serikali inazuia kwa sababu wanajua wakiruhusu itabidi tena tuanze na sisi kuagiza mahind kutoka nje,

Tanzania bado hatuna uzalishaji mkubwa wa kuweza kutosheleza ndan na kiasi ku export nje, chukulia mfano wa Mchele, Mashamba makubwa ya mpunga hapa Tanzania ni mangapi? Hata mashamba ya mahindi mfano kwa mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro hakuna shamba la ukubwa wa ekari 1000, mengi ni yanarenj kwenye ekari 400 hayo ndo makubwa sana,

Ukisikia mashamba ya miwa huko Brazil au mashamna ya mahindi huko marekani si mchezo ni hecta za kufa mtu mkuu
 
@komandoo, kuhusu quantity nafikiri wafanyabiashara wafikirie kuunganisha nguvu na sio kuwa wabinafsi. Kama zinahitaji litres 5 kwa mfano wakati mimi naproduce tatu, kwa nini nisitafute mzalishaji mwingine ambae anaweza kuzalisha mbili ili tuweze kuexport!? Huyo mtu angeweza kufanya hivyo na suala la quantity lisingekuwa kikwazo.

Mkuu kile kiwango walicho kuwa wanataka ni kikubwa sana na ni kwa kila mwezi.
 
semi processed products inamaana kwao inaweza kuwa ni raw materials?

Husninyo

very right, they will do final processing or re-processing, do their own branding and packaging of the product to add value for their own market
 
Mie binafsi sioni busara ya kuzuia sukari kwenda kenya! Kimsingi utazuia sukari kuuzwa kenya kihalali ila huwezi kuzuia sukari kwenda kenya, sanasana utatengeneza ajira mpya ya wapagazi na usuru bandia wa askari wa doria na maafika wa forodha. Acha sukari ya kilombelo iende kenya na Mohamed entr alete ya Brazil. Mbona Rangerover zinauzwa japan na Toyota zinauzwa marekani na hammer zinauzwa uingereza. sasa sisi inakuwa ajabu sukari ya tanzania kuuzwa kenya na sukari ya brazil kuuzwa Tz?
 
mkuu

you have a point, market ya europe na sehemu nyingine inatushinda kwasababu ya quality ya bidhaa zetu especially branding na packaging

nashauri labda tujikite na semi-processed products halafu hao wazungu wakaumize kichwa kwenye brand name na packaging, imagine ukianza kununua asali ulkaipack kwenye madumu ya liter 200 uka export kama semi processed honey bee? au ngozi zilizo safishwa,, au semi-processed wood/timber and so many to mention

there should be a way forward and this is the right time

this is a very good thread

Pazuri hapo! Tazama wenzetu wa kenya! wana sambaza kahawa na chai ulimwengu mzima! Europe ndio usiseme. Hivi Tz si tunavyo hivi vitu (kahawa, chai na kadhalika zote?) na katika harakati zangu mwanakijiji kuna wakati nilibeba Afri Coffee. ilipendwa sana huko safarini lakini whats next?? kwenye supermarket nyingi ukiingia na kununua chai unakutana na Mkenya kwenye shelf! what happened to the east africa thing ya kufungua mipaka na kushirikiana na kusaidiana kibiashara!! au walimmanisha hii kwa ajili ya kuuza local kati yetu. Dah
 
Cc Invisible hii thread muhimu sana katika kuwafumbua macho wabongo ili nao wafaidi masoko ya nje nimeona ni muhimu uka weka kama sticky thread.
 
Sisi watanzania wengi tunapenda kufanikiwa overnight. Hatupendi kufanya research kupata information hasa kwenye mitandao kuna taarifa za kutosha kukufumbua macho na kukuonyesha njia. Kuna vijana niliona wako nafikiri Moshi au Arusha. Wanawawezesha wakulima wadogo wanalima kunde mbichi wana process na packing zinasafirishwa nchi za ulaya kila siku.

Pia kuna organisation nyingi tu zinatoa funds, grants, or mnaingia into agreement wanakupa pesa baada ya kupresent proposal wakaikubali...na hili si jambo la overnight na pia unaweza jikuta unatuma hata to more than several organisations hapa unakataliwa lakini hutakiwi kukata tamaa eventually unapata. Hawa jamaa wa kunde mbichi nafikiri walifanikiwa kupata.

Pia sisi watanzania ukiangalia bidhaa zetu tunavyouza hazina ubora usafi n.k. hivyo ukianzisha kitu ni vizuri kuhakikisha kiko na ubora.
Kwa anayetaka kupata more information na kujifunza mengi juu ya biashara na jinsi ya kuwafahamu na kupata wanaoweza kukuwezesha kwenye business kubwa. Kuna kitabu kinauzwa kinaitwa 101 WAYS TO BE RICH IN AFRICA. Humu kuna ideas nyingi za biashara na ni jinsi gani waweza kufanya na pia ni watu gani wanaweza kufund hizo business.

Hii karne ya kuwa mbunifu maana kila business ipo ila inabidi kuifanyia ubunifu zaidi ya yule anayeifanya.
 
Kuna bidhaa nyingi tu zinazotoka kenya kama bamia, chai. Uganda wanaleta ndizi, viazi vitamu unga wa ulezi unga wa sembe. Kuna maembe. Ila kwa ipande wa Tz bado.
 
Back
Top Bottom