Je, Nelson Mandela anastahili anavyotukuzwa?

hyphym

Member
Jun 13, 2011
12
3
Namheshimu sana Nelson Mandela, natambua sana mchango wake kwa taifa la Afrika ya Kusini. Historia yake ya kutoka gerezani na kuingia ikulu hakika inavutia na ni kitu cha kutia moyo kwa wapigania haki. Zaidi atakumbukwa kwa RECONCILIATION a...liyoleta Afrika ya Kusini baina ya Weupe na Weusi......... LAKINI...... Zaidi ya hapo hivi ni MCHANGO gani Mandela ametoa kwa bara la AFRIKA?

JE NI KWELI huyu Mandela ni zaidi ya viongozi kama Mwl. Nyerere, Kwame Nkrumah na Ghadafi kwa maana ya kujitoa kusaidia bara la Afrika?

.................. Moja ya mambo ambayo jamii ya watu weusi wanalaumu ni kushindwa kwake kuutafsiri uhuru wa KISIASA katika hali yao ya maisha na manyanyaso ya KIUCHUMI............... Urafiki wake na Mataifa ya MAGHARIBI ulibadilisha mtazamo wake na kuweka mazingira mazuri kwa Wageni kwa hasara ya Waafrika wenzake..... Faida aliyopata ni KUTANGAZWA NA VYOMBO VYA HABARI vya kibepari kama Kiongozi mwenye MCHANGO ZAIDI KWA BARA LA AFRIKA!!!

Mungu akupe afya njema Mandela. Binafsi nakuheshimu kama kiongozi uliye na historia ya kuvutia uliyeanza vizuri na kumaliza VIBAYA
 
NELSON MANDELA anatukuzwa kwa jambo moja kuu duniani kama ALAMA YA MSAMAHA.

Aliweza kuwasamehe waliomfunga, akafanyanao kazi serikalini na alipokuwa rais aliwaalika waliomfunga wakiwemo maaskari wa gereza katika tafirija ya chakula Ikulu lakini pia aliunda TUME ya upatanisho kati ya watu weupe na weusi kwa lengo la kuzika kumbukumbu za ubaguzi wa rangi.

Na mengine WENGINE wataongezea
 
Mandela ni kiumbe wa ajabu wa karne hii anastahili kupewa heshima ya kweli
 
NYOTA njema huonekana asubuhi. Binafsi naamini mandella kafanya makubwa hadi kuhatarisha maisha yake na familia ndipo akafungwa kifungo cha maisha. Lakini siamini kwamba alijitoa zaidi kuliko hao wengine.

wazungu wamemjenga zaidi mandella kwa sababu zao binafsi. kumbuka Afrika kusini ndilo taifa pekee la Afrika lenye wazungu wenyeji wengi. Kutoa msamaha wa dhati kwa hawa wazungu kumechangia mataifa ya magharibi kumbeba zaidi kuliko wenzake. Kwa mfano, ni nani anakumbuka kazi kubwa aliyofanya Nyerere kuikomboa Afrika hadi akatumia rasilimali zetu. hili wazungu haliwahusu kulipa promo.
 
Namheshimu sana Nelson Mandela, natambua sana mchango wake kwa taifa la Afrika ya Kusini. Historia yake ya kutoka gerezani na kuingia ikulu hakika inavutia na ni kitu cha kutia moyo kwa wapigania haki. Zaidi atakumbukwa kwa RECONCILIATION a...liyoleta Afrika ya Kusini baina ya Weupe na Weusi......... LAKINI...... Zaidi ya hapo hivi ni MCHANGO gani Mandela ametoa kwa bara la AFRIKA?

JE NI KWELI huyu Mandela ni zaidi ya viongozi kama Mwl. Nyerere, Kwame Nkrumah na Ghadafi kwa maana ya kujitoa kusaidia bara la Afrika?

.................. Moja ya mambo ambayo jamii ya watu weusi wanalaumu ni kushindwa kwake kuutafsiri uhuru wa KISIASA katika hali yao ya maisha na manyanyaso ya KIUCHUMI............... Urafiki wake na Mataifa ya MAGHARIBI ulibadilisha mtazamo wake na kuweka mazingira mazuri kwa Wageni kwa hasara ya Waafrika wenzake..... Faida aliyopata ni KUTANGAZWA NA VYOMBO VYA HABARI vya kibepari kama Kiongozi mwenye MCHANGO ZAIDI KWA BARA LA AFRIKA!!!

Mungu akupe afya njema Mandela. Binafsi nakuheshimu kama kiongozi uliye na historia ya kuvutia uliyeanza vizuri na kumaliza VIBAYA

Mkuu naomba uelewe vyombo vya habari Africa vinafuata vyombo vya habari vya nchi za magharibi wanachotukuza. Mandela anatukuzwa vyombo vya magharibi kwa sababu kuu za RECONCILIATION kama ulivyosema hapo juu. Wazungu walidhani baada ya uhuru tutakuwa na vurugu za weusi kutaka kulipiza kisasi lkn haikutokea sana. Hii ndiyo iliyompa hiyo heshima kuliko kukaa jela na kuwa Rais wa kwanza wa Afrika Kusini huru. Hili linamfanya atukuzwe na vyombo vya Magharibu na Afrika tunafuata mkumbo lkn Mandela hajalifanyia bara la Afrika chochote cha zaidi.
 
Mandela attaheshimika kwa kuwa aliwekwa ndani kipindi kirefu na alipopata urais alas kipindi kimoja tofauti na Nyerere mara hungatuka na baada ya Muda husema mara wazee mara vijana wamemuomba aendelee kuwa madarakani
 
Mandela kwa bara la afrika ametoa uhuru wageni kuishi sauzi ndio maana kila mtu anatumbukia kule...Nyerere kikubwa sana alichofanikisha kwa 100% kusomesha hichi kizazi cha MAFISADI !!! angelijua mapema angewakata shingo angali wadogo
 
Mandela anastahili kwasababu pamoja na kuzuia vita nchi yake ameifungua na wa South na kampuni zao zimesaidia sana Africa kuanzia kwenye Bank na kampuni za bia, sigara vyakula n.k. Kama unafanya kazi kampuni ya bia Tanzania bila Mandela isingekuwa kubwa hivyo kwani mashari south africa yalitolewa baada ya madela kutoka jela. Je angefia jela south africa ingekuwa wapi leo?
 
Namheshimu sana Nelson Mandela, natambua sana mchango wake kwa taifa la Afrika ya Kusini. Historia yake ya kutoka gerezani na kuingia ikulu hakika inavutia na ni kitu cha kutia moyo kwa wapigania haki. Zaidi atakumbukwa kwa RECONCILIATION a...liyoleta Afrika ya Kusini baina ya Weupe na Weusi......... LAKINI...... Zaidi ya hapo hivi ni MCHANGO gani Mandela ametoa kwa bara la AFRIKA?

JE NI KWELI huyu Mandela ni zaidi ya viongozi kama Mwl. Nyerere, Kwame Nkrumah na Ghadafi kwa maana ya kujitoa kusaidia bara la Afrika?

.................. Moja ya mambo ambayo jamii ya watu weusi wanalaumu ni kushindwa kwake kuutafsiri uhuru wa KISIASA katika hali yao ya maisha na manyanyaso ya KIUCHUMI............... Urafiki wake na Mataifa ya MAGHARIBI ulibadilisha mtazamo wake na kuweka mazingira mazuri kwa Wageni kwa hasara ya Waafrika wenzake..... Faida aliyopata ni KUTANGAZWA NA VYOMBO VYA HABARI vya kibepari kama Kiongozi mwenye MCHANGO ZAIDI KWA BARA LA AFRIKA!!!

Mungu akupe afya njema Mandela. Binafsi nakuheshimu kama kiongozi uliye na historia ya kuvutia uliyeanza vizuri na kumaliza VIBAYA

Yeah_umenena hoja mkuu,...nimewahi kujadili hili jambo na watu fulani hapa kazini na kuhoji ni kipi hasa cha maalum ambacho Mzee Mandela kafanya kufikia kumtukuza kiasi hicho lakn watu wakaishia kutoa pointless kama za maridhiano mara msamaha kwa wazungu waliomtesa,...

Ki_ukweli kwa mtu yeyote makini ni lazima angefanya maridhiano na kutafuta suluhu na wazungu hata kama walimtesa,...tukumbuke wazungu ndio walikuwa wameshikilia uchumi wa S.A,majeshi na vifaa vya kijeshi vya kisasa_above all hao wazungu walowezi(kaburu) hawana sehemu ya kwenda zaidi ya kuwa hapo(S.A ndio kwao)..

Mbaya zaidi huyu mzee aliwarubuni waafrika na kuanza kuwanadi makaburu nchi za africa ili wawapokee kama ni wawekezaji_logic behind ni kuwa hao makaburu angalau waachie baadhi ya njia za uchumi weusi wa south africa wao watambae maeneo mengine ya africa...matokeo yake ndio haya tunayayaona wametamalaki kote africa in the name of wawekezaji huku wakiua na kunyanyasa watueg,...Tanzanite One.

My take;...Mzee Mandela anastahili heshima lakini sio kama anavyotukuzwa na walami i.e Nyerere,Gaddafi,Nkrumah and co...did much more compared to Mzee Madiba
.........get well soon mzee madiba.

Peace,Love and harmony.

Jah guide.
 
Msimfananishe huyu mzee na magamba wa TZ...Huyu mzee ni wa watu na kila mtu anajua..
Kumbuka kabla ya Bush kumvamia Sadam alitaka kwenda Iraq ili vita ikianza na yeye awepo na afie kule kwa ishara ya kupinga vile vita.
Sioni unachotaka kujua cha ajabu kuhusu Mandela.
Jua tu ni mwanadamu wa kawaida mwenye sifa zaidi ya Binadamu waliokuzunguka na si kama yuleee aliyepigwa msalabani akafufuka...
Huyu ni mwili na nyama na alizaliwa kama kawaida....
God is Great
 
Kwahiyo kian Nyerere,Nkrumah,...and co...ni magamba,...huko irak kwanini hakuenda sasa....mmmmh?

.....get well soon mzee madiba.
 
Ni kiongozi wa kipekee Africa, huwezi kumfananisha na kiongozi mwingine na si kweli eti ni propaganda ya vyombo vya habari vya magharibi. Jikumbusheni na Historia
 
Kila mtu ana sifa yake katika jambo lake. Kwa ukombozi wa Africa huwezi kumsemea mandela sana, labda kwa ukombozi wa SA. Kwa ukombozi wa Africa lazima Jina Nyerere liwepo!
 
Anayetaka kuhoji umashuuri wa mandela lazima atakuwa na utindio wa ubungo, yaani kumfananisha na nyerere ambaye alifukuza watu kwenye nchi kwa sababu za kupinganao kimtazamo na mbaya zaidi akaunda usalama wa taifa kushughulikia watu badala ya rasilimali za taifa mpaka leo ndio kazi ya usalama, mandela ni kiumbe kingine kabisa,kwenye ukweli atasema ukweli,hana ubaguzi hata chembe si wadini wala rangi.tafuteni lingine na sio huyu mzee

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Namkubali nyerere kuliko mandela atleast nyerere spoke out about ubeberu wa wazungu lakin mandela he was soft on them that's why wanampenda na kumtukuzatukuza nyerere alizungumzia siasa,jamii,uchumi,diplomasia ya ndani na kimataifa vizuri sana mi sijui mandela alikua mjamaa au bepari?alisimama wapi huyu?
 
Sidhani kama Mandela anastahili sana sifa anazopewa na jitihada alizofanya juu ya ukombozi wa bata la Africa..Ni wiki chache zmepita ilipotelewa taarifa inayoonesha Mugabe akimponda Mandela kwamba he was too soft to whites kiasi ambacho mpaka hao weupe wachache wakimiliki njia kuu za kiuchumi huko S.A.Alishindwa kubadilishwa maisha ya watu wa Soweto ambako ndipo vuguvugu la mageuzi lilipoanzia na mpaka sasa ni miongoni mwa sehemu maskini huko S.A.Ni miaka so mingi baada ya kutoka jela ndipo USA walipomtoa katika kundi la TERRORISTS na he was banned to enter the USA soil,na hlo lilifanyka tuu baada ya kuridhiana na weupe wachache wa S.A.So,in short hana mchango wowote ktk bata la Africa kama ilivyokuwa kwa Nyerere, Nkurumah, Gaddafi ni..
 
Nimejaribu kuangalia michango yote hapo juu watu wengi wana idea moja,kwamba anastahili heshima hasa kwa ukombozi wa SA lakini kwa Afrika hana mchango mkubwa mi nadhani hii imekaa sawa,akina Nyerere na Nkurumah walijitanua sana kupigania uhuru wa mataifa mengine,Nyerere aliwahi kusema kwamba kuna raha gani kuwa na amani wakati majirani zetu wana shida,Mwisho wa siku kila kiongozi anabaki na historia yake.
 
NELSON MANDELA anatukuzwa kwa jambo moja kuu duniani kama ALAMA YA MSAMAHA.

Aliweza kuwasamehe waliomfunga, akafanyanao kazi serikalini na alipokuwa rais aliwaalika waliomfunga wakiwemo maaskari wa gereza katika tafirija ya chakula Ikulu lakini pia aliunda TUME ya upatanisho kati ya watu weupe na weusi kwa lengo la kuzika kumbukumbu za ubaguzi wa rangi.

Na mengine WENGINE wataongezea

Hakika ulichosema ni kweli,hata mimi nakubaliana na wewe.
 
Back
Top Bottom