Je, Ndoa za vijana ni changamoto?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,558
21,494
Wakuu,

Ndoa ni jambo jema. Siku za hivi karibuni vijana wengi wamekuwa wakichelewa sana kuoa. Vijana hao wa kiume wamekuwa na sababu zao tofauti tofauti.

Baadhi ya sababu hizo ni kuwa wanajipanga na maisha, kupata mke sahihi, wengine ni waoga maana wameona wanandoa wengine wameachana na wengine hawaelewani.

Swali langu; Je ndoa kwa vijana ni changamoto?

Tujuzane hapa

 
Tuanze kwanza na kwako, wewe umeolewa?

Kama bado nadhani utakuwa na maana halisi ya changamoto tunazopitia vijana kwenye suala zima la ndoa.
 
Siku hizi vijana wanaona mengi na wanapitia mengi. Ndio maana wanaogopa kuingia kwenye ndoa!

Last time I checked, the word marriage didn't sound good!
 
Yaani mimi hakuna kitu ninachokiogopa na kukichukia kama kupigiwa. Ugumu ndo unakuja Je? Nitaishi naye bila kuchapiwa? Nilipo hapa kituo cha kazi,wake za watu wanapigwa mpaka huruma kwa waume zao yaani,yaani kama wameolewa na wanaume wengi tofauti.Hii ni hatar sana.
 
Ni changamoto asee ndio maana unatanguliziwa cheti kabla ya mitihani, maana wangesema watoe cheti baada ya mitihani wengi wasingekuwa na vyeti vya ndoa.
 
Ndoa sio changamoto...!!Shida ni expectactions/matarajio kwenye hiyo Ndoa.
Men tunamtazamo tofauti na kabsa na wanawake.Kimbembe ni kuweza wote kua na matazamo Mmoja hapo ndo shida.
There is so much noise kuhusu ndoa Inatuwia vigumu kufanya maamuzi.

Personally I wish I get married coz najua ni kitu chema na cha baraka,Sio fashion wala status bali ni wito Mtakatifu.
 
Ndoa ni heshima, hasa hasa kwetu sisi wanawake, kila mtu anamtazamo wake mfno mm sina mpango wa kuolewa na wala sifikiriii
 
Back
Top Bottom