Gomez Luna
Senior Member
- Mar 13, 2017
- 187
- 205
Kwa muda mrefu kidogo,vyombo mbalimbali vya habari vimekua vikidai kwamba Israeli imekua ikitumia ndege vita zake mpya aina ya F35I Adir kwenye mapambano mbalimbali kabla ya kuhalarishwa rasmi na jeshi la anga la Israel(IAF) kwa ajili ya mapambano hayo.
Lakini Leo,mwanahabari anayehusika na masuala ya kijeshi hasahasa ya anga bwana Thomas Newdick anatuletea ripoti ya uchunguzi toka kwa mwaandishi wa habari wa Ufaransa kuhusiana na madai hayo kwamba F35I Adir imekua ikitekeleza mashambulizi kadhaa nchini Syria.Lakini pia maelezo kuhusiana na vitu husika vilivyoshambuliwa(targets).Mwandishi huyo pia alidai kwamba oparesheni ya kwanza kufanywa na Adir(F35) ilifanywa mwezi January ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo kwenye ardhi ya Israel tokea Marekani.
Mwandishi Thomas Newdick anaeleza kwa kifupi ripoti hiyo kama ifuatavyo;
George Malbrunot, ambaye ni mwandishi wa gazeti la ufaransa Le Figaro,alitoa vyanzo vya uchunguzi/upeleIezi huo. Alipost kwenye Tweeter mifano ya ndege za Israeli F35-mbili ambazo zilifanya mashambulizi ndani ya Syria usiku wa Januari 12-13.Mashambulizi hayo yalihusisha sehemu mbalimbali ndani ya Damascus, Syria.
Tweets mbalimbali zikielezea tukio hilo
Kutokana na Malbrunot, F35 zililenga maghala ambayo yalihifadhi makombora ya Pantsir(SAM) ambayo jeshi la Israel lilikua likihofu kwamba yalikua yakipelekwa kwa wapiganaji wa Hezbollah kule Lebanon kupitia Syria.Ghala hilo linapatikana eneo la Mezzeh, kambi ya jeshi mjini Damascus.
Israeli F35I Adir
Katika Operesheni hiyo pia inadaiwa kwamba jeshi la Israel liliharibu kabisa makombora ya kutungulia ndege aina ya S300 yaliyowekwa karibu na ikulu, kwenye mlima Qassioun.Kulingana na chanzo kingine cha uchunguzi cha Ufaransa ambacho hakikutajwa jina kilieleza kwamba ndege vita za Israel F35 I Adir ziliruka juu ya ikulu ya Rais wa Syria Bashar Al Assad kabla ya kurudi tena nchini Israel.
S300 Surface to Air Missile
Malbrunot alimnukuu mwanajeshi mmoja ambae jina lake halikutajwa akisema "Kama Hezbollah wangezipata hizo Pantisir basi jeshi la anga la Israeli lingepata wakati mgumu kufanya mashambulizi yake ndani ya Lebanon".
Pantisir SAMs
Kuisoma ripoti nzima chukua linki hii
Maana kila nikijaribu kuiandika humu inakataa kutokana na Urefu nahisi.
ze kokuyo Nalendwa izzo Elungata Chenchele nankumene MURUSI Mount Kibo Root