Je, Nchi yetu kubadilisha Katiba ya nchi na kuwa ya chama kimoja cha siasa?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,417
2,000
Kutokana na mienendo ya kisiasa inavyokwenfa nchini kwetu, kuna tetesi kuwa watawala wetu wako mbioni kurejesha mfumo wa chama kimoja

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) inatamka kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itaendeshwa katika mfumo wa kidemokrasia na ni ya mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu

Ukifuatilia matukio kadhaa nchini kwa siku za karibuni, ni dhahiri kuwa watawala wetu wamepania kuitejesha nchi yetu kwenye mfumo wa chama kimoja

Mikakati kadhaa inaendelea nchi nzima nyuma ya pazia

Mkakati mmjawapo muhimu sana uliofanyika hivi karibuni ni kuwakata "makali" wapinzani, katika uchaguzi wa setikali za mitaa wasichukue hata mitaa mmoja nchi nzima!

Mkakati mwingine ni kivipunguzia vyama vya upinzani nguvu ili kuwezesha mambo ya watawala yapite bila kipingamizi chochote

Tumeona dalili za awali kabisa za watawala wetu katika kutimiza azma yao dhalimu katika uchaguzi wa serikali za mitaa ulioisha hivi karibuni, ambapo wagombea wa vyama vya upinzani zaidi ya asilimia 95, yalikatwa na wasimamizi wa uchaguzi huo, ambapo ni makada kindakindaki wa CCM, kwa madai kuwa wamekosea kujaza fomu za kuombea uongozi huo na wasimamizi wa uchaguzi kuzikimbia ofisi zao!

Wakati wenzao wa CCM wakidaiwa kuwa wagombea wao ni "malaika" ambapo wagombea wao wote asilimia 100, wamejaza kwa usahihi mkubwa na hivyo kufanya wagombea wao, wapite bila kupingwa!

Hivi karibuni tulimsikia Rais Magufuli akihoji iweje yeye apewe mamlaka ya kuteua na asipewe mamlaka ya kutengua ndani ya Katiba ya nchi??

Ni jambo linaloeleweka kuwa kuna baadhi ya nafasi ambazo kutokana na unyeti wake, Rais amepewa mamlaka ya kuteua, lakini amenyimwa uwezo wa kutengua

Miongoni ya nafasi hizo ni ya CAG na Majaji wa mahakama kuu

Inaonekana hiyo kupewa nafasi ya kuteua bila kupewa uwezo wa kutengua, ndiko kunakomkera na kumkosesha usingizi Rais wetu

Basi ni dhahiri kuwa watawala wetu wanafanya mipango nyuma ya pazia kutaka kuirekebisha Katiba ya nchi yetu, ili kufanya usiwepo ukomo wa Rais kukaa madarakani

Tunaamini pia kwa yale tuliyoyaona kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ni "trailer" tu na ni dhahiri kuwa picha kamili tutaiona kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
 
kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,722
2,000
yaani hawa ni kama mashetani ambapo Mungu anatoa sheria zake na mashetani nao wanapambana kutunga sheria zao!
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
22,286
2,000
Lumumba hawanaga aibu, wanaweza kufanya kweli - waanze maoni ya katiba - kisha wautoe na huo ukomo wa Urais.
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,538
2,000
Wangejua ni bora ya kupambana na upinzani kupitia vyama vya siasa na ni hatari kupambana na upinzani usio wa vyama.
Kwa wepesi wa ccm litakuwa jambo la kama kumsukuma mlevi kuipindua nchi kwa nguvu ya umma ambayo kama ilivyokuwa kwa nchi zingine jeshi litakaa pembeni maana ni la "wananchi" na sio jeshi la "viongozi"
 
mnyalilungulu

Senior Member
Sep 27, 2019
170
250
Kutokana na mienendo ya kisiasa inavyokwenfa nchini kwetu, kuna tetesi kuwa watawala wetu wako mbioni kurejesha mfumo wa chama kimoja

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) inatamka kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itaendeshwa katika mfumo wa kidemokrasia na ni ya mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu

Ukifuatilia matukio kadhaa nchini kwa siku za karibuni, ni dhahiri kuwa watawala wetu wamepania kuitejesha nchi yetu kwenye mfumo wa chama kimoja

Mikakati kadhaa inaendelea nchi nzima nyuma ya pazia

Mkakati mmjawapo muhimu sana uliofanyika hivi karibuni ni kuwakata "makali" wapinzani, katika uchaguzi wa setikali za mitaa wasichukue hata mitaa mmoja nchi nzima!

Mkakati mwingine ni kivipunguzia vyama vya upinzani nguvu ili kuwezesha mambo ya watawala yapite bila kipingamizi chochote

Tumeona dalili za awali kabisa za watawala wetu katika kutimiza azma yao dhalimu katika uchaguzi wa serikali za mitaa ulioisha hivi karibuni, ambapo wagombea wa vyama vya upinzani zaidi ya asilimia 95, yalikatwa na wasimamizi wa uchaguzi huo, ambapo ni makada kindakindaki wa CCM, kwa madai kuwa wamekosea kujaza fomu za kuombea uongozi huo na wasimamizi wa uchaguzi kuzikimbia ofisi zao!

Wakati wenzao wa CCM wakidaiwa kuwa wagombea wao ni "malaika" ambapo wagombea wao wote asilimia 100, wamejaza kwa usahihi mkubwa na hivyo kufanya wagombea wao, wapite bila kupingwa!

Hivi karibuni tulimsikia Rais Magufuli akihoji iweje yeye apewe mamlaka ya kuteua na asipewe mamlaka ya kutengua ndani ya Katiba ya nchi??

Ni jambo linaloeleweka kuwa kuna baadhi ya nafasi ambazo kutokana na unyeti wake, Rais amepewa mamlaka ya kuteua, lakini amenyimwa uwezo wa kutengua

Miongoni ya nafasi hizo ni ya CAG na Majaji wa mahakama kuu

Inaonekana hiyo kupewa nafasi ya kuteua bila kupewa uwezo wa kutengua, ndiko kunakomkera na kumkosesha usingizi Rais wetu

Basi ni dhahiri kuwa watawala wetu wanafanya mipango nyuma ya pazia kutaka kuirekebisha Katiba ya nchi yetu, ili kufanya usiwepo ukomo wa Rais kukaa madarakani

Tunaamini pia kwa yale tuliyoyaona kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, ni "trailer" tu na ni dhahiri kuwa picha kamili tutaiona kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
tatizo hutaki kuushughulisha ubongo wako ndomana unaongea pumba
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,099
2,000
Hakuna kitu kama icho alishindwa Mugabe, Museveni, Kagame jiwe kama atajaribu kufanya uo ujinga itakuwa ndio mwisho wake.

Walio zaliwa jana tu ndio hawaelewi nini kilisababisha kuja kwa mfumo wa vyama vingi africa ni amri wala haikuwa ya kubembeleza kutoka nchi zinazotupa misaada na WB&IMF

China anafanya vile kwa sababu ategemei misaada ya magharibi na WB&IMF kama wanataka kufanya ivyo wasitishe kwanza misaada ya nchi za magharibi na mikopo ya WB&IMF.

Tatizo la jiwe ni kufanya mambo kwa kukurupuka bila kujua historia na kusikiliza wapambe watu makini wapo pembeni wanamcheka tu.
 
THE BREED

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
1,756
2,000
acha wabadili ni haki yao!!!LAKINI cha kujiuliza ni nani alijua haya kuwa jiwe ana roho mbaya?je wakibadili siku akiingia alie mbaya kuliko huyu watafanyaje?maana hata huyu aliepo hakuna anae tamani aendelee hata wale waliompa nafasi wanajuta!acha yawatokee puani!!!
 
Kwa kweli hata kama walijua ana roho mbaya, lakini si kwa kiasi hiki anachowafanyia watanzania
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom