Je Nchi inaweza jiepusha na hasara hii kila mara?

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
848
1,212
Benki ya Dunia kupitia taasisi zake za usuluhishi za kibiashara pamoja na taasisi nyingine za Usuluhishi za kimataifa zimejiwekea utaratibu wa kuhakikisha mitaji ya wawekezaji inalindwa, pia sheria za uwekezaji za kimataifa zinatambua makubaliano ya mapatano ya kibiashara baina ya kanda na Nchi au nchi kwa nchi ( MTAs na BTAs) ambapo sheria zote hizo kwa pamoja zinatumika kulinda uwekezaji dhidi ya maslai binafsi ya upande wowote.
Tanzania ni moja ya mnufaika mkubwa wa Benki ya dunia na hivyo ni mpokeaji na mtekelezaji wa maazimio na taratibu za kifedha zilizowekwa na World Bank kama sehemu ya masharti ya unufaika.
Hivyo basi aidha kutokuheshimu makubaliano hayo, au kupuuzia au kutenda nje ya makubaliano kumeiweka nchi katika hasara mbalimbali;
1. Kushitakiwa katika Mahakama za Usuluhishi na kulipa fidia, riba na hasara zilizotokana na migogoro ya kiuwekezaji
2. Kuwa katika hatari ya kupoteza wawekezaji hasa wenye mitaji mikubwa inayohitaji uwekezaji wa muda mrefu
3. Kupoteza ushawishi katika soko la dunia na zaidi katika kuvutia wawekezaji.
Je Nchi imepata faida ama hasara katika haya?
Hikistoria toka mivutano hii ya kushitaki Serikali ya Tanzania hasa kwa kuazia katika sekta ya Nishati na Umeme hii ndio hali halisi ya fedha za walipa kodi zilizopotea au zinazotarajiwa kupotea
1.Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320! - JamiiForums - Bilioni 320
2. Lissu aibua jambo ndege ya Bombardier - Bilioni 87
3. EcoEnergy lodges $500m claim after govt revoked its land title - Zaidi ya Bilioni 1000
4. U.S. firm seeks $561 million from Tanzania in power supply dispute ( U.S. firm seeks $561 million from Tanzania in power supply dispute) - zaidi ya Bilioni 1000
5. Sh336bn award verdict against Tanesco upheld - Bilioni 336 ( Tanesco must now pay the Hong Kong arm of Standard Chartered Bank a staggering $148.4 million (about Sh336 billion on the prevailing Bank of Tanzania exchange rate) owed under a power agreement )
6. http://www.acaciamining.com/export-ban-facts/press-releases/2017-07-04.aspx
Firm seeks payment of Sh130bn award
7. Firm seeks payment of Sh130bn award - Bilioni 130 ( News reports yesterday revealed Konoike Construction Company on Tuesday asked the District of Columbia Federal Court to sign off the award it won in February 2016 against the government.)
Gharama hizi ni nje ya zile za Uendeshaji wa kesi kwa maana ya malipo ya mawakili, kulipia gharama za jumla ya kesi baada ya kushindwa ambapo Serikali yetu imekwishatumia mabilioni ya shilingi katika kukidhi matakwa haya ya kisheria.
Je kama hii ndio hali, ipo sababu ya kulipa fedha hizo zote huku unapoteza wawekezaji, ajira zinakoma na pia kukosa uendelezaji wa uwekezaji husika ? Mathalani suala la Makinikia, Je tumeacha kusafirisha ? Tuna kiwanda sasa baada ya zuio hilo ? Ipo faida tuliyoipata kama Taifa?
 
Back
Top Bottom