Je, Naweza kuwa Mbunge au Kiongozi Mkubwa?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Naweza kuwa Mbunge au Kiongozi Mkubwa?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Boreless, Dec 28, 2009.

 1. B

  Boreless Member

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Ndugu wana JF,

  Naandika kuuliza swali nikiwa na simanzi kubwa rohoni.

  Nimempoteza rafiki yangu katika mazingira tatanishi. Rafiki yangu hivi karibuni aliweka bayana nia yake ya kugombea ubunge Kwimba. Aliamua kufanya hivyo baada ya kuombwa na kushawishiwa na wazee pamoja na vijana jimboni. Baada ya kutafajali alikubali na kuweka bayana msimamo wake. Suala la Ubunge kwake sasa ilikuwa ni suala la muda na kukamilisha utaratibu tu! Ghafla rafiki yangu amekutwa na mauti ambayo kuja kwake ni tata zaidi ya kifo cha Amina Chifupa.

  Binafsi sikuwa nimeitwa au kuombwa na yeyote nikagombee. Lakini nilikuwa ninataka nikagombee kwa dhati ya kulitumikia jimbo langu na taifa langu. Tatizo linalonipata sasa ni hii sayansi inayowamautisha ghafla wenye nia na Ubunge au Uongozi Mkubwa wa Kisiasa.

  Sijawahi kwenda kwa mpiga ramli au kuchanjiwa. Sasa, je:

  1. Inawezekana kweli mgombea kusimama katika siasa za kiwango hicho bila kinga na asimautishwe?
  2. Ni wapi zinapatikana kinga za ulinzi zenye viwango (ISO) vya uhakika?
  Nikiwa na majonzi natanguliza shukrani
   
 2. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu, kwanza nikupatie pole sana kwa majonzi hayo yaliyokufika wewe nasi wa tz wote kwa ujumla wetu.

  Ushauri wangu ni huu:

  a) Huyu mpendwa wetu anaweza kuwa amefariki kwa matatizo mengine yasiyohusiana na kugombea Ubunge. Isipokuwa kwa vile mauti imemkuta hali akiwa ameonyesha nia yake ya kugombea ubunge, wengi, ukiwemo, wanaweza kuhusianisha na ushirikina. Kwa hiyo, upande mmoja ni tukio ambalo limetokea kwa kile wazungu hukiita coincidence.

  b) Pili, kuna shida kubwa sana ambayo wengi wasiojifahamu kama wanamtumikia Mungu au wapo uvuguvugu wanayokumbana nayo. Maneno ya Mungu ktk Biblia yanasema Usiwe vuguvugu kwa vile Mungu atakutema. Na specifically ktk mambo ya Walawi 19:31 maandiko yanasema, usiwaendee wachawi wala waganga kwenda kutiwa unajisi. Kwa hiyo, ukiwa ni mkristo wa kuegesha egesha ni rahisi kupigwa juju!!!!. Kutokuwa na machale machale mwilini siyo kigezo kwamba haujakubwa na nguvu za giza. Machale mwilini ni ishara tu uwepo wa beacons za ibilisi ktk maisha ya mtu au ni alama zinazoonyesha kwamba wakati fulani mtu huyo aliwahi kupitiwa na unajisi wa ibilisi. Kwa ufupi ni kwamba imani iwayo yote, ambayo inakufanya uamini na kutegemea nguvu za giza inatosha kuweka beacons kwenye mwili wako, si lazima machale. Ukimwamini Mungu, hakuna uchawi wala uganga juu yako, sawasawa na maandiko ya Mungu katika Hesabu 23:23, yanayosema hakuna uganga wala uchawi juu ya Yakobo/Israeli. Maana yake hakuna uchawi juu ya wewe unayemtegemea Yesu Kristo. Mungu hana upendeleo ( ni somo refu), lakini somo Matendo ya Mitume 10:34-35, utaelewa angalau kwa kiasi kidogo.

  Kwa hiyo, ukienda haujajiimarisha kiroho; ukitegemea nawe nguvu za ibilisi umekwisha.

  Kwa hiyo, uchawi au uganga nk havina nguvu yoyote kama ukijenga mahusiano mazuri na Kristo Yesu.

  NIMEAMBATANISHA MAFUNDISHO NILIYOANDAA YANAYOWEZAKUKUSAIDIA KUUELEWA VIZURI UTAWALA WA IBILISI NA JINSI ANAVYOUTUMIA KUSHAMBULIA MAISHA YA MTU AU FAMILIA AU TAIFA , VIKUNDI NK.
   

  Attached Files:

Loading...