Je, naweza kutumia King'amuzi cha DSTV ya Afrika Kusini nchini Tanzania?

Sele Mkonje

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
643
844
Habari wakuu,

Naomba tu kuuliza kama inawezekana nikatumia king'amuzi cha DSTV cha Afrika ya kusini nchini Tanzania. Nimeona nchi kama Zimbabwe na Malawi wanatumia sasa sijajua huko nyumbani iko vipi?
 
Ni vema ukawacheki DM dstv wenyewe ungepata majibu mujaaarabu kuliko huku by the way ni ushauri wangu binafsi tuwasubiri wengine wanaweza kuwa na majibu mazuri.
 
Kwani hivi tunavyotumia bongo ni ving'amuzi vilivyotengezwa bongo au China?
Jibu unalo, waone DSTV watakusajilia wakipenda wasipopenda basi!lakini lazima uwe na documents zote za ununuzi na uingizaj inchin tz
 
Yani namaanisha naweza nikatoka na king'amuzi changu ninachotumia huku kikafanya kazi nikifika huko.? Kama wanavyofanya watanzania wanaotumia ving'amuzi vya Azam Tv nchini Afrika ya Kusini
 
Ni vema ukawacheki DM dstv wenyewe ungepata majibu mujaaarabu kuliko huku by the way ni ushauri wangu binafsi tuwasubiri wengine wanaweza kuwa na majibu mazuri.

umemshauri vizuri sana,
ila kwa kufikiria haraka haraka Dstv ya south ni lazima ifanye kazi huku kwa sababu zinatumia satellite
 
Ndio ila kwenye kulipia utalipia kwa fedha za nchi husika mfano umfkitoa RSA itabidi utàkuwa unakilipia kwa rand
 
Tatizo sitaki kumiss soapies za Mzansi. Halafu Natumia DSTV easy view ambayo nalipia R30 kwa mwezi yani kama TSHS 4000 hivi

Mkuu wanauzaje huko king'amuzi tupu cha dstv? Nataka ninunue cha huko maana huku tunalipa hela nyingi kwenye compact na bado Uefa hatuoni.

Wakati Compact ya South Africa ina mpk chaneli za Uefa
 
Yani namaanisha naweza nikatoka na king'amuzi changu ninachotumia huku kikafanya kazi nikifika huko.? Kama wanavyofanya watanzania wanaotumia ving'amuzi vya Azam Tv nchini Afrika ya Kusini

YES. Kitafanya kazi mkuu. Cha msingi ni satellite tu bas, Kama beam ya satellite inafika huku tz basi sio dstv tu hata CANAL+ na ving'amuzi vyengine unaweza ukavitumia TZ. Cha msingi malipo, kwenye kulipia lazma umpate mtu aliyepo huko SA akulipie.

Alafu DSTV ya SA bei nafuu mno tofauti na ya kwetu.

Wapo wengi tu wanafanya hivyo.
 
Habari wakuu,

Naomba tu kuuliza kama inawezekana nikatumia king'amuzi cha DSTV cha Afrika ya kusini nchini Tanzania. Nimeona nchi kama Zimbabwe na Malawi wanatumia sasa sijajua huko nyumbani iko vipi?
Unaweza tumia DSTV decoder ya South Africa na kulipia online kwa bank card.Kikubwa Fundi Dish akufungie kwenye transponder ya DSTV south Africa(kuna transponder ya huku east africa,na ya west and south africa) na decoders zipo programmed kwa kila nchi.kuna jamaa zangu wengi tu wanatumia south africa dstv decoders hapa Tanzania
 
umemshauri vizuri sana,
ila kwa kufikiria haraka haraka Dstv ya south ni lazima ifanye kazi huku kwa sababu zinatumia satellite
satelite inayo beam south africa ni tofauti na inayobeam hapa Tanzania.Uzuri wake hii satelite inayobeam south africa footprint yake inafika Tanzania.So fundi ataelekeza dish kwenye south africa dstv beaming satellite na hapo unapata south africa dstv pacakages na malipo unalipa kupitia visa card online kwenye web ya dstv
 
Yani namaanisha naweza nikatoka na king'amuzi changu ninachotumia huku kikafanya kazi nikifika huko.? Kama wanavyofanya watanzania wanaotumia ving'amuzi vya Azam Tv nchini Afrika ya Kusini
King'amuzi chenyewe DSTV ni 99,000/ lakini unatupigia kelele na kujipa mzigo wa kusafilisha kitu ambacho hakifiki hata pesa ya Mbuzi bebelu,
Ndiyo tatizo la vitoto vya uchumi wa kati.
 
Kibongobongo king'amuzi cha startimes ukihama mkoa na chenyewe hakionyeshi. Huu ubunge wa viti maalum ovyo sana
 
King'amuzi chenyewe DSTV ni 99,000/ lakini unatupigia kelele na kujipa mzigo wa kusafilisha kitu ambacho hakifiki hata pesa ya Mbuzi bebelu,
Ndiyo tatizo la vitoto vya uchumi wa kati.
Suala sio kuja kununua Tanzania. Ila kuna utofauti kati ya King'amuzi Cha SA na cha TZ elewa hilo
 
King'amuzi chenyewe DSTV ni 99,000/ lakini unatupigia kelele na kujipa mzigo wa kusafilisha kitu ambacho hakifiki hata pesa ya Mbuzi bebelu,
Ndiyo tatizo la vitoto vya uchumi wa kati.
Naona hujaelewa mada
 
Unaweza tumia DSTV decoder ya South Africa na kulipia online kwa bank card.Kikubwa Fundi Dish akufungie kwenye transponder ya DSTV south Africa(kuna transponder ya huku east africa,na ya west and south africa) na decoders zipo programmed kwa kila nchi.kuna jamaa zangu wengi tu wanatumia south africa dstv decoders hapa Tanzania
poppah kiongozi msaada wako muhimu sana hapa, kutokana na uzoefu wako ktk haya maswala ya dishes
 
Habari wakuu,

Naomba tu kuuliza kama inawezekana nikatumia king'amuzi cha DSTV cha Afrika ya kusini nchini Tanzania. Nimeona nchi kama Zimbabwe na Malawi wanatumia sasa sijajua huko nyumbani iko vipi?
Unaweza kutumia hicho king'amuzi hapa Tanzania iwapo tu utakuwa Mkoa wa Mtwara na baadhi ya sehemu ya mkoa wa Lindi.Hii ni kwa sababu mawimbi ya satellite yake yanakomea kusini mwa Tanzania ila nchi za Zimbabwe na Malawi wanapata mawimbi yake vizuri.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom