Je naweza kupata nyumba nzuri ya kuishi na yenye uzio (fensi) na geti kwa range ya TSH 35-50 Milioni?

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,929
Habari za uzima, heri ya mapinduzi kwa wa Zanzibar wote, Niende kwenye poit moja kwa moja kwa sasa nipo mkoa flani kwa utafutaji baada ya kumaliza masomo yangu moja ya chuo hapa hapa tanzania, sasa nimeona nichange pesa ili niweze kununua nyumba mkoa wa mwanza na kuanza kuishi uko

nataka kujua mawili matatu kuhusiana na mwanza maana mimi sio mwenyeji wa mkoa huo ila nilifika siku moja nikapapenda tu.

1. Je naweza kupata nyumba nzuri ya kuishi na yenye uzio (fensi) na geti kwa range ya ela hii (TSH 35-50 MILLION)
2.
Je ni maeneo gani ya mwanza naweza kupata nyumba kwa range iyo ya bei na eneo likawa zuri na lenye kufikika vizuri kwa gari bila shida?
3. Je ni eneo gani ambalo litakuwa ni zuri ambalo ata nikishuka kwenye ndege airport ya mwanza naweza kufika kwangu kwa uzuri kabisa ata kwa usafiri wangu (private car) au tax, ubber, tax f nk.

NOTE: Nimekaa sana DAR, nimesoma DAR, nimefanya mishe mishe zangu nyingi DAR ila sijapapenda DAR.

Na mengineyo mtakayo taka kunishauri ndugu zangu mnao ijua mwanza nawakaribisha.
 
Nenda kwanda Mwanza kaishi kwenye nyumba ya kupanga, baada ya mwaka utajua kila kitu na kupata majibu ya kila kitu apo juu.

Ushauri bomba, kuongezea mwanza ni sehemu isiyo na msongamano wa magari, kufika airport ni jambo rahisi ata utokee km 22 kutoka airport.

Maeneo. Ilemela, nyasaka, kiloleni, ata buswelu kutakufaa
 
Back
Top Bottom