Je naweza kupata mtafsiri wa ndoto anitafsirie ndoto hii iliyonitoa Machozi?

iam Lucha

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
2,153
2,000
Wakuu habari za asubuhi.

Usiku wa kuamkia leo nimeota kuwa mimi ni miongoni mwa watumishi wa umma katika nchi hii, tena nikiwa mlinzi katika sehemu nyeti kabisa ya nchi japo sikutambua nipo katika kitengo gani.

Ghafla nikiwa katika eneo la kaz lilijitokeza kundi kama la wanajesh ambao ni wa Afrca ila siyo wa nchi hii wakiwa wamebeba silaha nzito nzito Kama Ak47, LMG, RPG, IMI negev, na M27 IAR pamoja na silaha zingine nisizo zitambua, tena wakiwa wameshatuzunguka mimi pamoja na wenzangu bila kujitambua na tukawa hatuna Cha kufanya.

Ghafla ndan katika jengo tulilokua tunalilinda likatoka kundi lingine la watu wamevaa kijeshi wakiwa wamemkamata kiongozi namba 1 wa nchi, miongoni mwa hao watu alikuwepo mtu mweupe ( mzungu) alionekana ndo Kama kiongozi wa kundi lote lile lililo tuvamia.

Yule mtu mweupe alisogea mbele akiwa ameshika kipaza sauti, lakin kabla hajaongea akatokea mtu mweusi mmoja amevaa unform za jeshi ambazo siyo za nchi hii kisha akaenda hadi ilipo bendera ya Tz na akaishusha kisha akapandisha bendera mpya ambayo ilionekana inafanafanana Kama ya Kimarekani... Sehemu hii nilipo ona bendera ya nchi yangu inashushwa na kupandishwa bendera ya nchi nyingine ndani ya nchi yangu ndo sehemu nilipotoka Machozi ya kweli katika ndoto hii ni Mara yangu ya kwanza kutoka Machozi katika ndoto nikiwa na hisia kali mno za kizalendo licha yakua uhalisia wangu sipo na uzalendo wa hivyo kabisa tena nimekinai nchi yangu.

Baada ya ile bendera inayo fanania ya Kimarekani kupandishwa ndipo yule mzungu akatoa tamko, kuwa wao hawataki kumwaga damu ya yeyote na viongozi wote wa majeshi wasijaribu kufanya chochote kwakua wao wananguvu kubwa kuliko sisi na drones tayar zipo juu ya kila kambi ya jeshi chochote kitakacho fanyika kinyme na amri yao bas wataripua kambi zote na kuteteteza watu pamoja na silaha zote, hii ni sehem nyingine niliyotoka Machozi zaidi

Akasema wanaotaka kuungana nae waungane nae kwakua ataboresha mara 10 zaidi masilahi yao (mshahara) na asie taka akae pemben, hapo majeshi yakapata mpasuko mkubwa kund moja kubwa likaungana na na mzungu yule na kundi lingne dogo lisilo na nguvu yani wale wazalendo wakaa upande mwngne, hapa machozi yalizidi kunitoka zaid kwakua kundi la wazalendo lilibaki ni kundi dogo sana ambalo lisingeweza kubadili chochote.

Yule mzungu akaondoka alaf pemben ya ile bendera ya yule mzungu ikapandshwa bendera nyingine ya nchi ya Afrca ambayo siikumbuki vizuri wakimaanisha kuwa ile nchi ndo itakua wasaidizi wa utawala wa mzungu yule, na bendera yetu ikawa haipo kabisa ikiwa ni ishara rasmi ya kutawaliwa upya na kutokua na uhuru, moyo wangu ukauma sana katika ndoto huku machozi yakinitoka nikifikiria ni lini tena tutaweza kupandisha bendera yetu

Sina lengo baya katika uzi huu ila hii ni ndoto ya kweli kabisa iliyo niumiza ikiambatana na hisia kali kitu kilicho nishangaza sana, ingekua tupo enzi za watafsiri ndoto bas siku ya leo ningeenda kwa wazee wanipe tafsiri ya ndoto hii.
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
3,774
2,000
Maana yake ni kwamba huyo nambari moja wako , mtukufu anayeweza kila jambo, anayeogopwa na kunyenyekewa na wasaidizi wake, anayeweza kuamuru jambo juu ya maslahi ya watumishi wa umma bila kupingwa safari yake ya utawala ni fupi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom