Habarini za Jumapili ndugu wa JF,
Nina imani tunaendelea kupambana na athari za ugonjwa wa korona ambao athari zake zimekuwa kubwa sana kiuchumi kuliko kiafya hasa katika jamii yetu ya Kitanzania/Kiafrika.
Nije kwenye mada yangu moja kwa moja. Kumekuwa na utaratibu wenye mkanganyiko kwa watu wa daladala hasa wa jiji la dar es salaam katika utozaji wa nauli. Makondakta wamekuwa wakitoza nauli kubwa kwa kuliko kiwango kilichowekwa na mamlaka kwa kisingizio cha vituo badala ya umbali hivyo muda mwingine kuleta mzozo kwa abiria ambao wanajua utaratibu wa mpangilio wa nauli zilizowekwa na mamlaka husika.
Hapa naweka mpangilio wa nauli kulingana na umbali kwa mujibu wa Sumatra /Latra.
Umbali -- Nauli
0.1-15km 400-450
15-20km 500-600
20-25km 600-750
Sasa natumia ruti ya Gongo la Mboto kama mfano.
Kutoka G/Mboto - Makumbusho =22km
G/mboto - Buguruni =12km
G/mboto - Ubungo =19km
Vingunguti - Buguruni =2.4km
Vingunguti - Tabata Reli =4.5km.
Kitu kinacholeta mkanganyiko ni kwamba ukipanda gari kutoka gongo la mboto mpaka buguruni ambapo ni 12 km nauli ni sh 400 lakini ukipandia gari Vingunguti na ukashuka tabata reli ambapo ni 4.5 km kondakta anakwambia nauli ni sh 500 tena anakwambia nauli ya 400 mwisho ni buguruni bila kujali umepandia wapi.
Lakini ukikagua tiketi zao zimeandikwa nauli kwa baadhi ya vituo na umbali na hali hii ya kuandika nauli za vituo badala ya umbali ipo jiji dsm kwa kiasi kikubwa kuliko majiji mengine.
Sasa je, nauli zinazotozwa na watu wa daladala wa jiji la Dar es Salaam kwa kuzingatia vituo badala ya umbali ni sahihi kwa mujibu wa mamlaka husika au ni abiria kutokuwa na uelewa kuwa nauli inalipwa kulingana na umbali na siyo vituo au ni makondakta kutokujua kuwa wanapaswa kumtoza abiria nauli kulingana na umbali na siyo vituo?
Wakuu naomba tupeane elimu juu ya hili.