Je, Nape alikuwa ni mmoja wa waandaaji wa #VoNoCo dhidi ya Rais Magufuli?

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,394
4,748
Ama kweli ule msemo wa ''ningejua urais uko hivi nisingechukua fomu'' una maana kubwa nyuma yake.

Urais una mengi sana...urais ni kama vile hali ya vita ambayo maadui wanatokea ndani na nje ya jeshi lako.

How come waliojiita wapigania chama wanakaa chini na kupanga mipango dhidi yako kwa maslahi ya kundi lao na sio chama au nchi basi...ukiwaza hivyo ni lazima uwe mbogo tu...Good thing state and party machineries ziko chini yako na zinafanya kazi 24/7 kwa ajili yako.

Yote kwa yote namhurumia Magu lakini pia namkubali sana kwa kuicheza hii game ya "Tz political chess" kwa ustadi wa hali ya juu sana na kwa hisani ya wapiga kura na wazalendo wa kweli utashinda kiulainii ukiwaacha watu wakilia vijijini mwao.

Nikumbushe tu hata JK nyerere alikutana na hilo kundi sumbufu toka enzi zile...alilikemea lakini wapi...nadhani muda muafaka wa kuli-wipe out umefika...at any cost...!!

Najua JPM anawaona anawaona....anawaona wanapokutana na anawaona wanachokipanga and always amekuwa smarter and lightyears ahead of them....

SENT AS RECEIVED!!

"BE AS WISE AS THE SERPENT YOU ENCOUNTER"
 
Sikuelewi. Nchi sasa watu wamejawa na hofu na umaskini unaongezeka kwa kwa kasi. Kama wasiwasi ni wasaliti mbona hata Yesu alisalitiwa na Yuda Iskarioti.
 
Mleta mada umeandika utumbo mtupu, kwa sababu...
1/Ngosha hajui kabisa kufanya siasa, yaani kwenye siasa ni Bashite kabisa, hivyo hawezi kamwe kucheza hizo political chess..

2/Kinachofanywa sasa na Ngosha ni Ubabe, Vitisho, Visasi, kufukuza nk. Hakuna siasa ya namna hiyo milele.

3/Makada wengi wa CCM wana wasiwasi mkubwa sana kuwa iwe mvua iwe jua 2020 CCM haiwezi tena kutoboa kirahisi kwenye siasa (Rejea kauli za hivi karibuni za Kinana, Nape, Bashe, Msukuma, Ridhwan, JK)
 
Tanzania ya enzi za nyerere tofauti na hii ya sasa!
kama nyerere aliweza kuwa wipe out hao waliomsumbua kirahisi usifikiri itakwa rahisi kwa jpm enzi hizi
 
Kwamba uliemuandikoa ni mtu smart...nitakua wa kwanza kupinga jogoo wa shamba hawiki mjini...
aliwika nyerere kwa nini jpm ashindwe. watoto wa mjini wanajivunia kula chapati za kumimina wakati wa shamba wanaangalia maisha ya baadae.
 
Kama chama kilianza kumshinda muasisi wake mwenyewe Mwalimu Nyerere, kikajigeuza kuwa chama cha mabwanyeye badala ya chama cha wakulima na wafanyakazi (Jembe na Nyundo); mbele ya macho yake mwenyewe, akabaki kulalamika: "CCM sio Mama yangu"! Ni nani huyo wa kukibadilisha chama hiki kilichomshinda profesa wa siasa?! Kukata, kutisha na kuwapoteza baadhi yao ni kukiua chama chenyewe ndani kwa ndani zaidi kuliko kukibadilisha, kwani strong arm tactics haikuwahi kuwa suluhisho vinginevyo kina Mobutu, Bokassa, Gadhafi, Saddam, Hitler, Mussolin na wengineo wengi kama hao wangekuwa bado wanapeta katika Dunia hii!
 
Naomba nisaidiwe welewa,Nape kamwita bashite mpuuzi...je,mtu anayemwamini huyo mpuuzi na kumpa kazi ya kuendesha mji mkuu/jiji kuu kabisa nchini tumwitaje??
Hii haimaanishi kuwa yeye ndiyo katukanwa zaidi?
mkubwa wa haowatu ataitwaje?? Nauliza tuu wenyetafakuri pana
 
Mleta mada umeandika utumbo mtupu, kwa sababu...
1/Ngosha hajui kabisa kufanya siasa, yaani kwenye siasa ni Bashite kabisa, hivyo hawezi kamwe kucheza hizo political chess..

2/Kinachofanywa sasa na Ngosha ni Ubabe, Vitisho, Visasi, kufukuza nk. Hakuna siasa ya namna hiyo milele.

3/Makada wengi wa CCM wana wasiwasi mkubwa sana kuwa iwe mvua iwe jua 2020 CCM haiwezi tena kutoboa kirahisi kwenye siasa (Rejea kauli za hivi karibuni za Kinana, Nape, Bashe, Msukuma, Ridhwan, JK)
Irudie hiyo list hapo mwishoni mwa post yako
 
Back
Top Bottom