Je, nani wakili mzalendo anayeweza kutetea nchi yake si tumbo lake?

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF,

Katika awamu zote zilizopita nilishuhudia kesi nyingi za wazi ambazo serikali ilikuwa ikishindwa na mshindi kuja kudai fidia kubwa ambayo utugharimu tena, ili hali mtu huyo anakuwa kafanya ubadhilifu wa kutisha.

Nchi za wenzetu kuna mawakili ujitolea kuamsha kesi dhidi ya watuhumiwa kuhakikisha aidha wanarejesha walichokiiba au wanakwenda Jera.

Miaka ya nyuma, kesi nyingi za Tanesco zote tulishindwa vibaya, na watetezi wengi ni watanzania, kuna kesi za wizi uliofanyika kwenye mashirika, na unaona mtu ana mali zainazozidi mshara wake, lakini watu hawa hawashitakiwi popote.

Kuna kashifa lukuki, ambazo zemehusu rada, Escrow, vijana wapo wanadunda tu. kuwa wakili ni baraka kutoka kwa Mungu kuwa wewe ni mtetea haki, haiwezekani mtu anahujumu taifa, na wewe unaona kuwa kweli katenda kosa, lakini unamsaidia ashinde kesi alafu inatughalimu kama taifa.

Natanguliza samahani kwa ambaye anaona sijamtendea haki kwa kazi yake ya uwakili lakini, kwenye kesi za huhujumu uchumi kama mtu kafanya dhambi hii ya kuhujumu taifa, bora umlengeshe tu akafungwe hata kunyongwa lakini taifa libaki na faida, ikiwa atarudisha mali alioiba.
 
Kila mtuhumiwa ana haki ya kujitetea. Na kila mtuhumu ana wajibu wa kuthibitisha tuhuma.
Hata Mungu hakumuhukumu Adam kabla ya kumpa nafasi ya kujitetea.

Leo kuna watu wanabambikiwa kesi za uhujumu uchumi ili tu wasote rumande!

Utawala mbovu huzaa sheria mbaya na mwenendo wa sheria hizo huwa mbaya pia.
 
Kesi alizozisimamia mzee wa Musoma kofia Nyekundu hakuwahi kushinda kesi hata moja, ina maana sheria alizosomea wale walinzidi kiwango?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom