Je, Nani anayemwajiri Mwenzake kati ya wananchi na serikali??

Fanfa

JF-Expert Member
Sep 25, 2009
1,815
2,862
Siku zote tumekuwa tukielezwa na wanasiasa kuwa wananchi ndo mwajiri wa serikali yoyote hapa duniani. Na mimi naamini nadharia hiyo ni sahihi. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi ukweli wa jambo hili kama kweli "Wananchi ndo mwajiri wa serikali" sipati majibu.

Kama ni kweli kwa nini serikali yetu ni kichwa ngumu kiasi kwamba hawataki kumsikiliza mwajiri wao "Wananchi" na badala yake wanafanya kinyume na mwajiri wao anavyotaka.

Wananchi tumepiga kelele katika maswala mbalimbali tukitaka yafanyiwe kazi ama kupitika katika wabunge wetu, NGO's zinazotetea maslahi ya taifa, Jamii forum, watu binafsi n.k lakini bado serikali yetu haitaki kutekeleza yale tunayoyataka na badala yake wanafanya wao wanayoyataka kwa maslahi yao.

- Tumesema maliasili yetu isivunwe kwa manufaa ya wageni (Dhahabu, Almasi, Urenium, madini ya vito na mengineyo)
- Tumesema pesa zetu za EPA wahuska warudishe serikali bado inawakumbatia
- Maswala ya RICHMOND, MEREMETA, KAGODA n.k hakuna kilichofanyika
- Matumizi mabaya ya kodi zetu tumepiga kelele waache kufanya hivyo badala yake wanazifanyia kutalii mje kila siku na wengine kuzichota bila aibu
- Tunadai huduma bora za jamii (Elimu, Afya, barabara n.k) hawataki kufanya hivo.

SWALI: Kama kweli wananchi ni mwajiri wa serikali, mbona yote haya mwajiriwa hataki kuyafanya?
- Ni nani hasa anayemwajiri mwenzake ??
- Ni yupi mwenye nguvu zaidi ya mwezake, mwajiri au mwajiriwa???

Mwanakijiji na wana-forum wenzangu hebu nisaidieni kwa hili
 
Mwajiri (wananchi) kazubaa, amekua mzembe na mwenye imani potofu baada ya kulishwa limbwata na mwajiriwa (serikali).
 
Back
Top Bottom