Je, nani amekwamisha malengo yako mwaka 2019 yasitimie?

Mpuretamu

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,227
1,999
Mwaka ndio huo tunauaga (unatuaga?) leo. Nina uhakika kila mtu alijiwekea malengo yake katika maisha yake. Mimi pia nilikuwa na malengo ya kwangu.

Kwa kila mtu pengine kuna hatua fulani ya malengo yako umeyafikia, ama pengine kuna sehemu (kubwa au ndogo) umekwama kufikia kile ulichokuwa umekilenga.

Katika kufunga mwaka huu kila mtu afanye reflection ya alichokuwa amekipanga na kutaja mtu/watu waliokwamisha kufikia malengo yao mwaka 2019.

Watu hao waweza kuwa marafiki, familia, ndugu wa mbali na wa karibu, wanasiasa, viongozi wa dini, wachumba, walimu (hata wahadhiri), watumishi wa umma (askari, madaktari, wahandisi, n.k).

Tutiririke. Mimi nina arrears zangu serikalini hazijalipwa, nimeshindwa kununua Toyota IST yangu, sijui nani kanikwamisha hapa!!
 
Back
Top Bottom