Je, nani alifinance project ya ujenzi wa Safina?

Baada ya Mwenyezi Mungu kumpa Mchoro kamili wa Ramani ya SAFINA nabii NUHU:- Unadhani Kwa Ufahamu unaoujua wewe au Kwa Dini uliyoisoma wewe, Huyu Nabii Nuhu alitengenezaje Boti ile Kubwa zaidi Duniani.. alipatawapi material na Nani Alifinance Project Yote!
Where God directs,he provides!....jibu ndio hilo
 
Mwanzo wa biblia imeelezea taifa la Israel kwa upana bila watu wengine ila kiuhalisia watu wengine walioitwa wa mataifa walikuwepo ikiwepo sisi wataznania
Biblia ngumu sana kuielewa kaka kuna muda unafika mpakani unaogopa kukufuru tu ukijitia mfukinyuzi mfano ishu ya kaini alipomuua ndugu yake Habil tunaambiwa alikimbia ili watu wasimdhuru, je ni watu gn hao!? Tunaambiwa mungu alimuwekea alama ili yeyote atakayemuona asimdhuru na atakayemdhuru atalipiziwa kisasi mara 70, pia tunaona alipofika katika taifa hilo alikutana na majitu akajitwalia mwanamke huko,swali je hao majitu ni viumbe wa nani!? Na kama kulikuwa na watu wengine je hao kwanini hawajazungumziwa katika uumbaji wao!?
 
Biblia haijaandika wazi ni muda gani haswa Nuhu alitumia kuijenga safina, kwa sababu

Biblia haielezi kwa uwazi ni muda gani Nuhu alichukua kujenga safina. Wakati Nuhu anapotajwa kwa mara ya kwanza katika Mwanzo 5:32, ana umri wa miaka 500. Wakati Nuhu alipoingia ndani ya safina, ana umri wa miaka 600. Muda uliochukuliwa kujenga safina unategemea muda uliopita kati ya Mwanzo 5:32 na wakati ambao Mungu aliamuru Nuhu kujenga safina (Mwanzo 6: 14-21). Kwa kabisa, ilichukua miaka 100.

Kwa hiyo ukitazama vizuri utaona kabisa muda uliotumika ni mrefu sana hivyo nina imani kabisa watu waliojenga safina walikuwa ni wengi
Ila ilihitaji moyo kumaliza muda wote bila kukata tamaa na hapo ndio maana ikazuka zana ya kumcheka na kumkebehi mana alilowambia halikuwa linatimia.
Lakini kuhusu mnefili Ogu kuna kitabu fulani cha kidunia kinasema
Wakati garika inaanza hakuwa eneo la dunia alioilenga Mungu na ndio maana historia ya Ogu inajirudia hata wakati garika ilipokwish kupita na hii inamaanisha Ogu hakusombwa pamoja na garika ile japo hatuelezwi kiuwazi ni nini kilitokea hadi ogu akaja kuwa mfalme miongo michache baada ya garika na wakati alitajwa wakati wa ujenzi wa safina...

Lakini pia vitabu vingie vinasema
Wanefili hawakufa katika garika ile maana walikuwa ni malaika waliojivika miili ya kibinadamu na wakajivua na kuwa roho wakati wa garika na kurudi mbinguni huko wakatengwa na malaika watiifu na hapo wakakimbilia kwa malaika muasi ambae tunamwita shetani.

So kuhitimisha mawazo yangu kulingana na vitabu vingi vioneshavyo ni kuwa Nuhu hakuijenga safina peke yake,walijenga wengi ila Mungu alihitaji waliomaliza mwanzo mwisho na ndio mana wakapatikana watu nane badala ya wanne,yaani wale watoto watatu wa Nuhu na yeye mwenyew,
Mana hata Mke wake hajatajwa japo wengi wanadai anaeza kuwa ni Naama
Kitabu cha kidunia?
 
Biblia haijandika kila kitu ..kingeandikwa kila kitu Basi kingekuwa kitabu kikubwa sana..ndio maana ukitaka upate upana wa mambo usome pia vitabu vya historia na tamaduni mbali mbali za zamani ..kitabu Cha mwanzo pekee unaweza kuibuia maswali mengi Sana zaidi ya haya hasa kuanzia uumbaji ,kaini na Abel, uzao etc..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
nafikiri umesoma kwenye biblia dimension ya safina
niambie species milioni 4(ukizidisha mara mbili milioni 8) zinaweza kuenea vipi kwenye hiyo safina!!!
halafu akae na mbuzi bila kumla!!!!!
the bible is the best selling comic book
Mkuu kwanza yatupasa tujue gharika ilitokea wapi?? Unaposema hizo species million kadhaa je zinapatikana eneo husika gharika ilipotokea??

Ladba kama ilitokea dunia nzima lakini aidhani kama ilitokea dunia nzima. Labda Nuhu alichukua species zilizopo eneo ambapo pataharibikiwa.
 
Kabla hujajiuliza Simba anakaaje na swala bila kumla jiulize inakuaje mwenye kupooza anaambiwa simama ujitwike godoro uende zako na akainuka akaenda zake? Kama hutapata jibu la swali la pili basi hata la kwanza hutalipata.
Umewahi kumshuhudia kwa macho yako mtu Alie pooza akipona?
 
Back
Top Bottom