Je, na Wagombea wengine wa 'Urais' nchini Tanzania nao watakuwa na 'Confidence' kubwa ya Kuongea Kiingereza na Balozi wa US kama alivyoweza Lissu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,073
107,565
Kuna 'Mgombea' Mmoja hivi (bahati mbaya Jina lake limenitoka ghafla tu) nami natamani kweli kweli akishamaliza tu Ratiba yake ya Kugawa 'Kopi' za 'Vinyago' vyenye Mbuga zetu za Wanyama kwa Wageni wake Waalikwa basi nae akatishe zake aende Kupiga 'Stori' mbili tatu hivi na Balozi wa Marekani kama ambavyo leo 'Mgombea' Tundu Lissu amefanya.

Na huyu 'Mgombea' ambaye natamani nae akafanye hayo 'Mazungumzo' na Balozi huyo basi aruhusu 'Wanahabari' wote wamuweke 'Mubashara' kabisa ili Wananchi tumsikie nae akitema 'Ung'eng'e' wake ambao utamzidi alionao Tundu Lissu.

Na inasemekana kuwa huyu 'Mgombea' Yeye ndiyo 'Kihistoria' ameanza Kutangulia kwenda Ulaya mno hasa hasa Ujerumani kuliko Mwenzake Lissu.
 
Mkuu naona kuna mtu unamchokoza. Hivi akituma watu wakupeleke kwake na akwamwaga ung'eng'e wa maana mbele yako utasemaje?

... ungenge wa maana kwetu tulijifunzia SEKONDARI na baada ya hapo. Somo pekee kwa lugha ya KISWAHILI ni hilohilo. Baadae tuloenda Manzese tulikutana humo na DS, ila kwa kiingereza. Sasa kama umeboronga digree ya kwanza, SAHAU ya pili na kwa hiyo ile ya 3.

Pale unapokua nazo TATU, ungenge utakuwepo tu. Thats the point
 
Je, Unafikiri uongozi bora unatokana na kujua English?

Maendeleo ya nchi ya Watanzania|waswahili yanajengwa na Lugha ya kiingereza.

Unajua Lugha inayotumika katika jamii,biashara za kila siku na shughuli nyingi za maendeleo ni Kiswahili??

Kwanini Mnajigamba kwa Lugha ya kigeni ambayo hata isingekuwepo Tanzania bado wananchi wa kitanzania tungefanya mawasiliano yetu vizuri.

Hivi nyie baadhi ya Waafrika mbona mnatufanya waafrika wote tuonekane wajinga.
 
64 Reactions
Reply
Back
Top Bottom