Je mzee 6 anauchungu wa kweli na nchi au maslahi binafsi?

majata

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
431
179
wadau msimamo wa mzee 6 mimi binafsi unanichanganya sielewi mzee huyu kama kweli anayoyasema anayatenda au hayatendi, naomba wataalamu wa mambo wanisaide kujua msimamo wa huyu bwana6.
 
ana uchungu na tumbo lake na hatma ya siku zake za baadae
 
Hana uchungu na nchi huyu fisadi papa bali ana usongo wa kukalia kiti cha urais, hizo sarakasi zote ni mkakati wa kwenda magogoni.
 
wadau msimamo wa mzee 6 mimi binafsi unanichanganya sielewi mzee huyu kama kweli anayoyasema anayatenda au hayatendi, naomba wataalamu wa mambo wanisaide kujua msimamo wa huyu bwana6.
Pinder hana machunga wala nini, ila ana kipaji cha kuigiza na machozi ya jirani.
 
Hana chochote anacheza na akili za wajinga, ni ikulu anayoililia, hamna kitu nafikiri wako kwenye campaign ya kufufua chama chao cha jamii. Lazima ile kwake.
 
Binafsi nilikuwa nafikiri huyu mzee ni mzalenda mpenda haki kumbe sivyo,ni ndumilakuwili anajipendekeza sana kwa JK ili maisha yake yaweze kwenda,siyo mtu mzuri hata kidogo
 
wadau msimamo wa mzee 6 mimi binafsi unanichanganya sielewi mzee huyu kama kweli anayoyasema anayatenda au hayatendi, naomba wataalamu wa mambo wanisaide kujua msimamo wa huyu bwana6.

uraisi mtamu.
 
Hana lolote huyo, ni tumbo lake tu anafikiria. Kama ana uchungu angeng'ang'ajiaje nyumba ya spika, angemwachia makinda ili serikali isihangaike kumpatia makinda nyingine. Haoni hiyo ni kuumiza walipa kodi zaidi. Sasa anazungumza kwa sababu ya maumivu ya kunyimwa uspika bado hayajapona.
 
Mimi sidhani kama anauchungu na nchi zaidi ya kujivalisha ngovi ya kondoo,nasema hvyo kwasababu 3 nazozifahamu,6 anakaa kwenye nyumba inayolipwa na ofisi ya spika dola elfu 8 kwa mwezi,na anaishi kwa kivuli cha kujipachika jina la spika mstaafu, huku aligombea akakosa nafasi, pili analipwa mafao kama spika mstaafu huku analipwa mshahara wa ubunge na uwaziri wake, na anasafiri kwa fast class popote aendapo na vyote hvyo hawezi kuweka hadharani na kwa kuogopa mambo yake yasitoke anajidai anauchungu na nchi, kama vile haitoshi amejenga ofisi kubwa ya spika urambo huwo siyo ubadirifu wa fedha za umaa? Hivi sasa ofisi hiyo inafanya kazi gani? Kuna zahanati ngapi hapo urambo kwann hakukarabati? Jibu mnalo na mtakao pata nafasi muulizeni awajibu.

Huyo ni fisadi nyangumi
 
Angekuwa na uchungu na nchi asingejenga ofisi ya uspika kule urambo kwa mamilioni ya walipa kodi akiamini kwamba atakuwa spika wa maisha.
Ni mnafiki namba moja hapa tanzania, na ajiulize hata akiwa mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji alifanya nini kusaidia kusolvu swala la umeme tz?
 
Ondoa kabisa huyu mnyamwezi kwenye orodha ya wenye uchungu na nchi hii. Ni mnafiki na opportunist tu.
 
kikwete si ampe huo uwaziri mkuu atulie huyu kinganganizi wa madaraka?
huyu atawatoa foho mpaka ahakikishe amekuwa waziri mkuu.
kwa anayebisha tuwekeane dau.
 
Huyu jamaa6 ni mnafiki mkubwa na Mzandiki!hana msimamo,leo atatetea ufisadi kesho atauponda! Kinyonga tu!
 
Angekuwa na uchungu na nchi asingejenga ofisi ya uspika kule urambo kwa mamilioni ya walipa kodi akiamini kwamba atakuwa spika wa maisha.Ni mnafiki namba moja hapa tanzania, na ajiulize hata akiwa mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji alifanya nini kusaidia kusolvu swala la umeme tz?
Kuna ambaye sio mnafiki ccm?Mkiweza kunitajia hata mmoja nitawapa shilingi moja ya Tz.
 
nashukuru kwa michango yenu wadau, mwanzo nilikuwa na mwamini sana mzee huyu lakini mashaka yangu yalianza wakati ameshikilia kazi za waziri mkuu bungeni nika mfananisha na popo kwani hoja ya wapinzani kuhusu posho ilikuwa ya msingi sana katika kuchangia mabadiliko ya matumizi ya selikari lakini alipinga bila hoja za msingi. Sikupata jibu kuhusu huyu babu na nia yake..
 
Kama anaona serikali na chama vyote vina matatizo angekaa pembeni ili asaidiane na wananchi kupambana na hiyo serikali na chama kibovu. Akumbuke Lyatonga Mrema alichofanya wakati wake.
 
wadau msimamo wa mzee 6 mimi binafsi unanichanganya sielewi mzee huyu kama kweli anayoyasema anayatenda au hayatendi, naomba wataalamu wa mambo wanisaide kujua msimamo wa huyu bwana6.





huna haja ya kuchanganyikiwa, kwani matendo ya kinafiki ni dhahiri, kwanini aendelee kulipiwa pango na mkewe alikopeshwa nyumba?? wajinga ndiyo waliwao. kama ni mkweli aseme kwanini muswada wa sheria ya famasi mwaka jana haukupata nafasi kuingia ndani ya bunge, kama kweli anasimamia haki na ukweli. you can cheat some people sometime, but you can not cheat all the people all the time
 
Nasema hv 6 kuwa rais ni heri hata hii nchi tukampa PITA KUGA MZIRAYI, tujue moja.
 
Back
Top Bottom