Je, mwisho wa kubadili hati ya kusafiria (passport) ya zamani ni lini?

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,929
Habarini za muda huu!

Naomba kujua, nina passport ya zamani niliipata mwaka 2014, mwisho wa muda wake ni mwaka 2024

Baada ya kuanza zoezi la passport za kielektroniki sikupata muda wa kufatilia zoezi hilo.

Naomba kujua, je, mwisho wa kubadili passport za zamani na kupata za kielektroniki ni lini, na je ni hatua au documents gani natakiwa kuwa nazo?

Msaada wenu wakuu

Karibuni

Sent using komputa mpakato
 
kikoozi,
Hiyo Passport yako uliokota?
Immigration si wapo kwa akili ya wananchi na wageni wanaohitaji Huduma ya immigration au Sifa za kujitangaza una passport.
 
Angalia hiyo mkuu
Screenshot_20191209-185626~2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi na kwasisi ambao tangu tuchukue passport mwaka 2010 mpaka leo ipo vile vile haina ata mhuri wa kitongoji cha jirani tutapewa kipaumbele..?

Sio muda wa kubadili
Bali 31 Jan 2020 Ndio mwisho Wa matumizi ya passport ya zamani
Ila kubadili au kupata Mpya ni kwa wakati wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi na kwasisi ambao tangu tuchukue passport mwaka 2010 mpaka leo ipo vile vile haina ata mhuri wa kitongoji cha jirani tutapewa kipaumbele..?
The Choji,
Msukuma wa watu unajiita jina kubwa wakati patupu.
Mtafutaji halafu unakaa na passport miaka kumi hujaenda nayo hata Ihayabuyaga?
Wewe usisumbuke hakuna mtu atakupa Passport, huihitaji watachukuwa Passport yao wakuuambie siku utapata safari uombe upya.
Ticket ya safari lazima iambatanishwe.
 
Back
Top Bottom