Gody Mnazarayo
Member
- Feb 7, 2019
- 41
- 45
Akiongea kwenye Hafla ya Kodi nchi Kenya Rais Wa Nchi hiyo Dkt William Samoei Ruto ameshangazwa na ukusanyaji wa Kodi unaoendeshwa na KRA mamlaka ya Mapato ya Nchi hiyo, Kwani ni watu Million 7 tu ndio wenye number za walipa Kodi ilhali Kuna zaidi ya Wateja Milioni 30 wanafanya miamala ya mabilioni ya Fedha bila kulipa Kodi. Wakenya wengi wamechangia kauli hiyo Kwa namna tofauti lakini baadhi wameunga Mkono wakishangazwa na idadi ya walipakodi kuwa ndogo, na wengine wakisema ni heri walipe Kodi za Miamala Ili kupunguza deni la Taifa lao, ambalo hivi karibuni limetajwa kuwa deni tishio.
Kauli hii ya Rais Dkt Rutto imenikumbusha ni hivi karibuni baadhi ya watu wememtukana sana Dkt Mwigulu Nchemba tena wakifikia hatua ya kumtaka aachie ngazi Kwa sababu ya kuanzisha Tozo za Miamala, wapo waliojiita manguli wa Uchumi walijitokeza hadharani na kukosoa mpango huo wakiita ni double taxation.
Mimi nawaza hivi kweli Wataalam wa Uchumi katika nchi ya Kenya na Tanzania wanakosea kuja na njia hii ya ukusanyaji? Au tatizo liko Kwa baadhi baadhi ya watanzania wajuaji waliozoea kutolipa Kodi Halali ya Serikali, au Kuna project ya kukwamisha Serikali ya Awamu ya Sita?
Watanzania tupunguze uswahili na ujuaji, Dunia imebadilika, hatuna budi kukusanya Kodi, Kwa njia yoyote Ili kuepukana na Fedhea za mikopo yenye riba kubwa.
Sent using Jamii Forums mobile app