Je mwanaume mchoyo na bahili anafaa kuwa mume???. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je mwanaume mchoyo na bahili anafaa kuwa mume???.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by nnunu, Apr 3, 2011.

1. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#1
Apr 3, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
NINA RAFIKI YANGU WA KIKE NI MFANYAKAZI ANAOMBA USHAURI KATIKA HILI.
ANA RAFIKI YAKE WA KIUME WANA UHUSIANO KWA MUDA WA MIAKA 9. SASA HIVI MWANAUME ANAMWOMBA AMUOE , ILA MWANAMKE AMEKATAA NA AMEMWAMBIA SABABU YA KUKATAA, ILA JAMAA AMEMWAMBIA BADO ANAMPA MUDA WA KUFIKIRIA ZAIDI LABDA ANAWEZA KUBADILISHA MSIMAMO AKAKUBALI KUOLEWA NAYE. MWANAMKE ANASITA KUtokana na uchoyo na ubahili wa mwanaume,ameshindwa kubadilika miaka 9 je kweli ataweza kubadilika wakiwa ndoani?.
NI MCHOYO SANA AU MBAHILI KUPITA KIASI.
Tangu waanze uhusiano wao mwanaume hajawahi kumtoa out mwanamke, japo mwanamke ana tabia ya kumtoa out mwanaume, amemwambia kuhusu hili lakin mwanaume anamwahidi kuwa asiwe na hofu ipo siku na yeye atamtoa na hasa watakapooana.Hajawahi kumnunulia zawadi yoyote japo huyu msichana anajitahidi kumnunulia zawadi huyo mpenzi wake. Hajawahi kupewa japo shilingi ya matumizi,ila huyu msichana mara chache huwa anampa, akimuuliza kwa nini hampi mwanaume anamjibu ampe pesa ya nini na yeye anajiweza kwa kila kitu. Ikitokea huyu dada anaumwa mwanaume atakuja kumwangalia hata mara 10 kwa siku lakin bila hata tunda wala huduma yoyote zaidi ya neno nakupenda mpenzi wangu upone haraka. Akiombwa ampeleke mahali na gari anakubali bila matatizo lakin lazima mwanamke ajaze mafuta kwenye gari,mwanamke anaweka na safari inaendeka,mwanamke asipoweka mafuta safari haiendeki.Kukiwa na tatizo lolote mwanaume ni mwepesi kuwepo lakin hachangii gharama yoyote inayohusiana na pesa.
Mwanaume ana kazi tena inayomwingizia pesa nzuri tu, anaishi kwenye nyumba aliyoijenga mwenyewe,ana gari na anajiweza kwa kila kitu, ndugu zake anawahudumia bila matatizo yoyote. Matatizo yote haya amemwambia lakin majibu anayompa ni kuwa huduma zote hizo atampa atakapomwoa.Kuna mwaka alimkopa pesa kabla ya kumkopesha alimuuliza atamlipa lini ,mwanamke alimwambia tarehe ya kumpa,mkopo alipewa ilipofika tu tarehe jamaa alimkumbusha tena asubuhi, mwanamke jion alipotoka ofisini alimlipa.Pia mwanamke aliwahi kuibiwa na wezi vitu vingi sana nyumbani kwake,akaanza upya kununua vitu alivyoibiwa, jamaa hakuchangia hata senti moja zaidi alitoa pole tu kwa mpenzi.Mwanamke alijinunulia kila kitu na mapenzi yao yaliendelea kama kawaida.

Kuna kipindi Ikabidi mwanamke amwambie MAMA WA MWANAUME(Mkwe) ili ajaribu kuongea na mwanaye, Mama mkwe alimjibu kuwa huyu mtoto amerithi tabia ya Baba yake kwani hata yeye hajawahi kununuliwa kitu chochote au kupewa pesa na mumewe tangu waoane na mpaka muda huu wanaanza kuzeeka. Kazi ya baba ni kutoa ada tu ya shule,lakin majukumu mengine anayatoa mama.Jibu hili lilimkatisha tamaa sana, ksb yeye upande wake anawaona wazazi wake wanashirikiana kwa kila jambo.
Mwanaume ameahidi kumfanyia yote watakapooAna lakin huyu dada moyo unamsita ksb anahisi maisha yao yatakuwa kama ya wakwe zake, mwanaume anaweza kumwachia majukumu yote ya nyumbani na familia kwa kisingizi kuwa mwanamke si anajiweza (ana kipato cha kumtosheleza). Huyu dada anaona hawezi kuishi na mume wa aina hii ksb ikitokea hana kazi,anaumwa hajiwezi kabisa kungiza kipato maisha si yatamwelemea,pia hana uhakika kama kweli huyo boyfriend wake atabadilika na kuanza kumhudumia.
Kumpenda anampenda na huyu mwanaume ana tabia zingine nzuri na hasa 6 kwa 6 anamridhisha 100% lakin UCHOYO NA UBAHILI umepita kiwango.
JE AMEFANYA MAKOSA KUKATAA KUOLEWA NA HUYU MWANAUME?? UPENDO SI NI KUTOA NA KUPOKEA? UPENDO GANI WA KUPOKEA TU?, HIVI NI KWELI KUWA MWANAMKE ANAYEJIWEZA KIUCHUMI HATAKIWI KUHUDUMIWA NA BOYFRIEND / MUME WAKE??.

SAMAHANI KWA MAELEZO MAREFU NAOMBA UVUMILIVU WENU.
NAOMBA USHAURI WANA JF.

2. Dena Amsi

Dena Amsi R I P

#2
Apr 3, 2011
Joined: Aug 17, 2010
Messages: 13,137
Likes Received: 255
Trophy Points: 160
Tena huyo amefanya kosa kubwa sana katika maisha yake huyo jamaa anamapenzi ya kweli kabisa na huyo dada anamapenzi ya pesa amekaa naye miaka tisa leo ndo ubahili unamshinda ana lake jambo huyo.

Wanawake tujifunze kujitegemea ana pesa halafu anataka za mwenzie za nini???

3. Rose1980

Rose1980 JF-Expert Member

#3
Apr 3, 2011
Joined: May 10, 2010
Messages: 5,701
Likes Received: 29
Trophy Points: 0

leo kdg umeenda shoto
we iweje mwanaume hana sense ya kujitolea?
kwamwanamke ata km unapokea milion kumi lakin ukapewa elfu moja tu na mpz wako bas unajiskai raha
sasa iweje mkaka hajitikisi?
uko0 ndan itakuwaje?mdada ndo agharamike kwa kila kitu?
aahh wap leo apana kdg ebu thk twice

maisha ya ndoa kusaidiana sasa jamaa hana ata chembe ..

kauliza kwa sasa kwa vle anataka kufanya maamuzi ya ndoa lakin km ingekuwa ubfrend tu angempotezea na wala asingeuliza

mapenz gan mpz wako hayupo concern ata kduchu?
km hana apo sawa ntaelewa lakin anayo ndo kwanza anataka nijihudumie ata nikimwomba lift kwenye gar lake basi mafuta nijiwekee dahh yaan ata afai ata kuwa rafik wa kawaida hafai

mama apana ...dalili zote za kuwa wewe ndo muhudumu wa familia znaonekana...MAPENZ GAN AYA YA KUCHUNWA WEWE TU?
ET MI NDO UWA NAMPA SKU MOJA MOJA ...kwanini umpe?asi anafanya kaz jaman?au zake ni zake zako ni zenu?

ANATAKA KUKUOA KWA SABABU AMEKUONA U MWANMKE WA KUTOA PESA SO UNAMFAA KWA TABIA YAKE YA UCHOYO

KIMBIA
NI BORA UWE NA MWANAUME ASIYEKUWA NA PESA KULIKO ALIYENAE AFU HATOI

4. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#4
Apr 3, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
HUYU DADA KWA VILE HAUMJUI DENA , hana mapenzi ya pesa hata kidogo, ila wasiwasi ni pale yeye atakapokuwa hana uwezo wa kupata pesa tena, iwe kwa kuumwa au, atawezaje kuishi bila hata support upande wa pili?
Samahani Dena je haujisikii vizuri MUMEO anapokuletea japo pipi ya sh 10? tena bila hata kumwomba?
Jaribu kuisoma vizuri huyu dada HANA MAPENZI YA PESA KWA HUYU KAKA, je mwenye mapenzi ya pesa angemvumilia huyu kaka miaka yote hii???.

5. nnunu

nnunu JF-Expert Member

#5
Apr 3, 2011
Joined: Mar 4, 2011
Messages: 656
Likes Received: 6
Trophy Points: 0
ROSE1980 upo sahihi kabisa, eti pesa yake ni yake peke, na ya mwanamke ni ya wote....
Maisha jamani si ni kusaidiana, au ni kusaidiwa tu??

Yeye huwa anampa kwa upendo tu , mfano akienda safarii anaweza kumwambia mpenzi wangu nilitaka leo tupate dinner pamoja lakin kwa vile nipo mbali ntakutumia pesa ukapate dinner popote japo sipo jisikie tupo pamoja, ndiyo mojawapo ya stahili anayompa kumpa pesa, kuonesha kuwa anamjali japo yupo mbali naye.

6. Dena Amsi

Dena Amsi R I P

#6
Apr 3, 2011
Joined: Aug 17, 2010
Messages: 13,137
Likes Received: 255
Trophy Points: 160

Rose sijaenda kushoto hata kidpgo mapenzi sio pesa bana mtu aakuja kukuona hospital wewe unadai hakuletei kitu? Yeye kuja ni muhimu kuliko pesa

7. WiseLady

WiseLady JF-Expert Member

#7
Apr 3, 2011
Joined: Jan 22, 2010
Messages: 3,248
Likes Received: 16
Trophy Points: 135
uuuuwi! Hata kama ni kupimana nope! !:car:

8. Dena Amsi

Dena Amsi R I P

#8
Apr 3, 2011
Joined: Aug 17, 2010
Messages: 13,137
Likes Received: 255
Trophy Points: 160

9. Dena Amsi

Dena Amsi R I P

#9
Apr 3, 2011
Joined: Aug 17, 2010
Messages: 13,137
Likes Received: 255
Trophy Points: 160
Halafu mambo ya zawadi inategemea na mtu na mtu

10. WiseLady

WiseLady JF-Expert Member

#10
Apr 3, 2011
Joined: Jan 22, 2010
Messages: 3,248
Likes Received: 16
Trophy Points: 135
dena!si kila kitu ni mapenzi ya pesa pls yani hosp ameshindwa hata kubeba machungwa 2?kha!hata huyu dada ni mvumilivu kwa miaka 9 yote!

11. Dena Amsi

Dena Amsi R I P

#11
Apr 3, 2011
Joined: Aug 17, 2010
Messages: 13,137
Likes Received: 255
Trophy Points: 160

Hebu niambie kipi bora atume pesa au Ribena halafu yeye mwenyewe asionekane

12. Rose1980

Rose1980 JF-Expert Member

#12
Apr 3, 2011
Joined: May 10, 2010
Messages: 5,701
Likes Received: 29
Trophy Points: 0

na akioombwa lift pia mafuta atie bnt ?
akuna tafu ata kdg?
wwe apana bwana u mzigo na km ivo historia ya baba ilivyo mama ndo majukumu yote ist fear

mh apana apo nakataa

na pa uyo kaka kumwomba ela dada wakat ana ela yake inakuwaje?  mkaka kujitoa kdg japo si sana inahusu sana japo aonyeshe sign lakin et kavu kavu afu mbaya zaid anakuomba wewe wakat yeye anayooo mmh apanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!

karibu wali njegere wali naz spnach....karbu DA

13. M

MaMkwe JF-Expert Member

#13
Apr 3, 2011
Joined: Sep 5, 2007
Messages: 284
Likes Received: 3
Trophy Points: 0
Hivi wanaume wamekwisha?

Mshaurini binti akatafute mwingine. Aachane na huyo mchoyo na bahili. Masikini binti inawezekana jamaa si mchoyo wala bahili ila ni njia ya kumkatisha tamaa tu.

14. m

mamakunda JF-Expert Member

#14
Apr 3, 2011
Joined: Jul 4, 2010
Messages: 371
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
Mimi niko kinyume nawe, nina shaka na huyu jamaa, unajua ni kawaida sana ya wapenzi kusaidiana kwa shida na kwa raha, sasa jamani mweziye alipoibiwa hata senti tano hakumsaidia? Maneno matupu hayavunji mfupa, na kwenye biblia imeandikwa imani bila matendo imekufa, sasa huyo jamaa nakupenda kwa mdomohaitoshi kwa hali halisi ya kibinadamu. Afadhali huyo binti amkatae tu, manake boranusu shari kuliko shari kamili.

15. WiseLady

WiseLady JF-Expert Member

#15
Apr 3, 2011
Joined: Jan 22, 2010
Messages: 3,248
Likes Received: 16
Trophy Points: 135
hakuna hata kimoja bora,,aonekane akiwa na ribena hata kama si kila siku

16. Dena Amsi

Dena Amsi R I P

#16
Apr 3, 2011
Joined: Aug 17, 2010
Messages: 13,137
Likes Received: 255
Trophy Points: 160

Mie sikubali kabisa kwanini mng'ang'anie mwanaume atoe? Mwanamke ukitoa kidogo kelele mpaka mtaa wa jirani. Miaka tisa mingi sana kashamzoea

17. M

MaMkwe JF-Expert Member

#17
Apr 3, 2011
Joined: Sep 5, 2007
Messages: 284
Likes Received: 3
Trophy Points: 0
Swadakta, kuendelea na jamaa huyu ni sawa na kukubali upofu. Mapenzi ni upofu kwa wasioona. yeye kesha muona jamaa ana hila, wa nini
kuendelea naye?

Atafute mwenza atakayemjali kwa hali na mali.

"Nyege kunyegezana"

Shaaban Robert

18. Dena Amsi

Dena Amsi R I P

#18
Apr 3, 2011
Joined: Aug 17, 2010
Messages: 13,137
Likes Received: 255
Trophy Points: 160

Na mimi nasema hivi mapenzi sio vitu wala mali bali ni moyo

19. Rose1980

Rose1980 JF-Expert Member

#19
Apr 3, 2011
Joined: May 10, 2010
Messages: 5,701
Likes Received: 29
Trophy Points: 0

:bored::bored::bored:

20. Rose1980

Rose1980 JF-Expert Member

#20
Apr 3, 2011
Joined: May 10, 2010
Messages: 5,701
Likes Received: 29
Trophy Points: 0
km ni moyo bnt kaonyesha
kwasasa anauliza kwa sababu anataka ndoa thats y anauliza wa swaga izi anafaaa au?

Loading...