Je mwanaume huyu anaweza kudai kwamba amefumania…?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
sad-black-woman1-378x337.jpg


"Ninakufahamu sana. Tulikutana siku ile ya harusi ya …(anataja jina). Ulikuwa umevaa gauni la mikunjo ya chini la rangi ya pinki. Namjua mumeo, nawajua ndugu zako . …. na …… na …..(anaaja majina ya ndugu zake). Nilivutiwa nawe sana, hasa nidhamu yako. Siyo kwamba nilivutiwa nawe kwa lengo lolote baya, bali nidhamu yako, na jinsi unavyowachangamkia watu. Nikipata muda nitaomba tukutane unifahamu. Pengine huo ukawa ni mwanzo mzuri wa kufanya biashara kati yetu, kwani nimeambiwa unajitahidi sana kibiashara…….."

Huu ni ujumbe wa simu alioupekea mke wa jamaa yangu mmoja aliyekuwa akifanya kazi ya mkataba mkoani na mkewe alikuwa akifanya biashara zake hapa jijini Dar. Ndoa yao ilikuwa ya amani na upendo na ilikuwa imedumu kwa miaka 12 na walikuwa wamejaaliwa kupata watoto watatu. Mwanamke huyu baada ya kupoke ujumbe huo wa simu aliujibu tu kwa kusema ahsante. Lakini aliendea kupokea ujumbe wa simu kutoka kwa huyo jamaa akizungumzia biashara anazofanya huyo mke wa jamaa yangu na kumshauri mambo mengi ambapo alipoyafanyia kazi yalimpa matokea mazuri.

Lakini kipindi chote wakati anawasiliana na huyo jamaa hakuwahi kumweleza mumewe kwa sababu hapakuwa na jambo lolote baya kati yake na huyo jamaa na isitoshe katika biashara zake amekuwa akishirikiana na baadhi ya wanaume kuagiza mzigo nje ya nchi. Baadaye huyu jamaa alimtaka mke wa huyo jamaa yangu wakutane maeneo ya mjini kwa ajili ya kujadili jambo fulani kuhusu biashara zake, kitu ambacho mwanamke huyo alikubali. Lakini wakati wote walikuwa wakiwasiliana kwa meseji tu na hawakupata kuongea kwa simu kwa sababu jamaa alimwambia kwamba simu yake ina matatizo ya spika. Alimwambia wakutane katika jengo moja hapo mjini mahali ambapo ndipo ofisi zao zilipo. Alipofika katika jengo hilo yule jamaa alimwambia yuko katika Hoteli fulani akipata lunchi na wageni wake waliofikia katika hiyo Hoteli hivyo alimuomba amfuate hapo Hotelini.

Yule mwanamke alikwenda kwenye hiyo Hoteli na alipofika pale mapokezi mhudumu alimwambia kwamba huyo mtu anayemtafuta yuko chumba namba 134 na aliacha maagizo kwamba akifika apelekwe katika chumba hicho kwani yuko na hao wageni wake. Mke wa jamaa yangu alimtumia ujumbe wa simu huyo jamaa akimtaka ashuke chini ili wakutane kwa sababu hawezi kwenda huko chumbani. Yule bwana akamjibu kwamba yupo na dada yake pamoja na mumewe ambao wanaishi nchini Hong Kong na wanachozungmza hata yeye kinamuhusu kwa kuwa ni wafanya biashara wakubwa huko Hong Kong….

Yule mwanamke alisita kidogo lakini baada ya yule jamaa kumsisistiza sana aliamua kwenda katika chumba hicho. Alipofika na kugonga mlango ulifunguliwa na aliyefungua hakuwa ni mwingine, bali alikuwa ni mumewe jambo ambalo lilimpa mshtiko mkubwa.

"Unajifanya unafanya bishara, kumbe unachapa umalaya eh….? Yaani mtu anakuita, humjui, wewe unakuja tu, tena chumbani….!" Ilikuwa ni kauli ya mumewe kisha ikafuatia maneno mengine mengi ya kashfa dhidi ya mkewe.................

Baada ya hapo ulifuata ugomvi mkubwa sana uliopelekea ndoa yao kuvunjika miezi miwili tangu kutokea kwa tukio hilo. Pamoja na juhudi kubwa zilizofanywa na ndugu, jamaa na marafiki wa pande zote mbili kutaka kuinusuru ndoa hiyo, lakini hazikuzaa matunda na ndoa hiyo ikavunjia.

Kumbe mume alikuwa ana wasiwasi sana na biashara za mkewe jinsi zilivyokuwa zinakua kwa kasi jambo ambalo halikumfurahisha, hivyo akaamua kumuwekea mtego mkewe kwa kujifanya huyo jamaa na mwisho wa siku mkewe akanasa na kusababisha ndoa yao iliyodumu kwa miaka 12 kuvunjika.

Je mnadhani ilikuwa ni halali kwa mume kumuwekea mkewe mtego kama huo…………….?

Hebu wana JF fungukeni hapa.
 
Duh; hii kama ni kweli ni mbaya sana. The fact kwamba mwanamke alikataa kwanza kwenda chumbani mpaka alippdanganywa ilitosha kumuona anajiheshimu. Nina amini alikuwa ana mbinu ya kujinasua kama ingekuwa tofauti, hata kama ni kupiga kelele tu.

Sijui tatizo la huyo mumewe, sitaki kuamini alikuwa anamtafutia tu sababu mkewe labda ana tatizo la kutojiamini.
 
Ukimchunguza bata sanaa hutomla!!!!!! Ndo yaliyomkuta hayo!
 
Duh; hii kama ni kweli ni mbaya sana. The fact kwamba mwanamke alikataa kwanza kwenda chumbani mpaka alippdanganywa ilitosha kumuona anajiheshimu. Nina amini alikuwa ana mbinu ya kujinasua kama ingekuwa tofauti, hata kama ni kupiga kelele tu.

Sijui tatizo la huyo mumewe, sitaki kuamini alikuwa anamtafutia tu sababu mkewe labda ana tatizo la kutojiamini.

Ukiona mtego haushiki ujue mtegaji una matatizo.
 
Nafikiri ilikuwa sahihi kuweka mtego lakini si afiki kuvunjika kwa ndoa, kwa sababu baada ya kugundua udhaifu wa mkewe angetakiwa kumwelewesha ili siku nyingine asiingie katika mtego km huo, pamoja na kumsisitiza suala kuwa muwazi kwake.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Je Unadhani ni kwa nini jamaa aliamua kumfanyia mkewe hivyo?

ni wivu tu ulikuwa unamsumbua, na njia aliyoitumia haikuwa sahihi kama lengo lake kweli lilikuwa ni kujua kama mkewe natoka njee ya ndoa.

hakumtendea haki mkewe, kwa mazingira hayo huwezi kusema umefumania.
wakati umekuwa ukuta kwangu ntarudi mkuu
 
kwa kweli nimesikitishwa sana kama ni kweli. .. kwanza pole kwa bibie,,,
hivi huyu man naona alikua na mambo ingine,, kwanza alikua na wivu wa kunawiri kwa biashara ya mkewe
naona alidhani mke atapata wealthy nzuri kuliko yeye hivo akawa na wasi
tatu inaonekana alikua na wasi,, alishamchoka mkewe,,
mume atafanya kila jambo kumwine mkewe na sio kumtafuta kwa mabaya tena kwa mitego,,,
nalaaani kitendo alichofanya na anahitaji arudi akaombe msamaha, maana alichofanya ni udhalim wa hali ya juu
kwa mke na kwa watoto
 
Jamaa hakuwa na nia nzuri na mkewe. Hatua zote alizopitia hakuna inayomfanya mkewe awe hatia zaidi ya kutomweleza mumewe kuhusu "rafiki mwema"
 
huyo ni among wanaume vilaza hapa chini ya jua yaani kama life ya ndoa iko hivi hata sishawishiki lol ngoja nile bata mie.
 
ni jambo la kushangaza huyo jamaa ameshindwa kumuamini mkewe kwa miaka yote hiyo. Alifanya hivyo ili iweje? Hicho si kipimo cha uaminifu
 
mwanaume mpumbavu tu ndo atadiriki kufanya hivyo........huyo mwanamke asijisumbue...mumewe kiazi
 
Mkuu mtambuzi namsifu sana huyu mama kwanza alionesha msimamo sana tu. Na kwa mume alitakiwa ampende sana mkewe!! Ila tu kama alifanya hivyo ili kupunguza kasi ya biashara/maendeleo ya mke ambayo najua ni overall maendeleo ya family basi huyu mwanaume hafai. Kwa mantiki hii huyu mama tena asepe mbaya kabisa!! Yaani nimpate mwanamke mchakarikaji tena ambaye hata anasita kumfuata mwanaume halafu nichukie!! Ningekuwa naoa mara ya pili ningeomba contact za huyu mama aiseeee!! Ni vile mimi ni monogonous!!!
 
Back
Top Bottom