Je, mwanaume anayo haki ya kudai mali alizochuma na mkewe baada ya ndoa kuvunjika?

Sijasoma maelezo yako, maana ni marefu balaa na yanatia uvivu kuyasoma. Halafu nimelewa gongo mixa na ganja kwa mbaaaaali. Ila acha nijibu kutokana na kichwa chako cha swali.

Ndio, mume ana haki ya kudai mali alizochuma na mke wake kisheria (Matrimornial Properties katika Sheria Za Ndoa). Mahakama itaangalia mali zilizopatikana ndani ya ndoa tu, kisha itazi thaminisha na kuzigawa kwa haki. Mali zilizo tafutwa kabla ya ndoa hazitoguswa. Hata kama mke alikua akichuma mali na kuziweka kwa jina la mtu mwingine (Akiweka pazia la kuficha ukweli) basi mume akiweza kuthibisha mahakamani zitagawiwa.

Hata kama mume alikua hana kazi na mke tu ndio aliokua akifanya kazi, kitendo cha mume kuwa bayana/kumliwaza/kumuuguza/kumsaidia mke hata kama ni shughuli za nyumbani kama vile kuosha viombo na kupiga deki au kufua au kupika (Kimahakama inahesabika mume amewekeza nguvu kutafuta hizo mali).

KUMBUKA; Kuendesha kesi si jambo dogo, inahitaji kuwekeza kwa hela na muda wa kutosha ili kuendesha kesi na kushinda. Au lasivyo utaambulia kuwa na madeni zaidi ya thamani ya pesa utakayo gawiwa. Hivyo, jipange upangike kimahesabu.
 
Sijasoma maelezo yako, maana ni marefu balaa na yanatia uvivu kuyasoma. Halafu nimelewa gongo mixa na ganja kwa mbaaaaali. Ila acha nijibu kutokana na kichwa chako cha swali....
Poleni sana hasa kwa mwanaume mwenzetu. Mke ana kesi ya kujibu, magawanyo ni pasu kwa pasu, haina ubishi, afuate wataalam wa sheria mahiri kuhusiana na kesi kama hizo tu.

Ila kesi kama hizi mbona ni za kawaida, kuanzia mapenzi, mke kuwa mtiifu na mwenye upendo, na matatizo kuanza pale atakapozaa, kukuzidi kipato na wazazi wa mke kuingilia mzozo bila hekima.

Akitaka haki yake huyu ndugu ipo, yeye tu.
 
Alishatemana nae na sasahivi anataka kuolewa na mwanaume mwengine. Na hiyo pesa hajakopeshwa, ila mkewe alitoa/alimpa kwa mapenzi yake mwenyewe. Hayo mambo ya kudaiana yamekuja baada ya kuachana
Hapo hamna kesi. Mali mkitafuta kipindi cha maelewano mkiachana hamna kudaiana tena kama mi ningekuwa jamaa vya kuuza ningeuza kabisa nikatia hela mfukoni.

Hakuna ambapo tuliandikishana kuwa mali flani ntazichukua tukiwa apart. Isitoshe mkikaa under one roof baada ya mwaka tu nyie ni mke na mume impliedly. Sio lazma cheti cha ndoa treatment ya sheria ni kuwa kila mmoja atakuwa amechangia kwa hali au mali.
 
Wakubwa zangu shikamooni! Vijana wenzangu mambo vipi! Wadogo zangu hamjambo?

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, mimi member mwezenu naomba msaada wa kuelimishwa juu ya haki na stahiki anazopaswa kupewa mwanaume baada ya kuachana na mke wake...
Dah, mpe pole sana jamaa ila ndio ajifunze next time mwanamke anaeoa asije akawa ndio anapigiwa jicho na familia yao. Maana shida ya familia zetu maskini hasa baba mkwe maskini ndio hupelekea haya majanga.
 
Hapo hamna kesi. Mali mkitafuta kipindi cha maelewano mkiachana hamna kudaiana tena kama mi ningekuwa jamaa vya kuuza ningeuza kabisa nikatia hela mfukoni.

Hakuna ambapo tuliandikishana kuwa mali flani ntazichukua tukiwa apart. Isitoshe mkikaa under one roof baada ya mwaka tu nyie ni mke na mume impliedly. Sio lazma cheti cha ndoa treatment ya sheria ni kuwa kila mmoja atakuwa amechangia kwa hali au mali.
Kweli hakuna kudaiana ila kuna kugawana.
 
mkuu Extrovert wewe noma! Jamaa ni muoga sana halafu hapendi malumbano ila ndio maana hata talaka kalazimishwa kutoa maana pamoja na kumfumania mwenyewe alikuwa yupo tayari kumsamehe kwasababu anampenda na wamezaa mtoto mmoja.
Jamaa yako ni Ndezi 😁
 
Ndio haswa msingi wa tatizo uko humu
Umeongea point kubwa sana mkuu!
Hata yeye anajuta na kukiri kuwa mkewe ndio alikuwa jicho la familia, yaani anategemewa kwa kilakitu hata wazazi wakawa hawana kauli kwake afanye zuri au baya lazima wam-support bint yao.
Halafu chengine wazazi wa huyo bint waliona kama bint yao anachumwa na mumewe kwasababu ya kipato chake, wakasahau kuwa ile ni ndoa halali hivyo mke kama anacho kipato ni wajibu kumpa au kumsaidia mumewe.
 
Back
Top Bottom