Je mwanamke unayetaka kuoa anakupenda au wewe ndiyo umempenda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je mwanamke unayetaka kuoa anakupenda au wewe ndiyo umempenda?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Anold, Mar 30, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Watu wengi hasa vijana waliofiksha muda wa kuoa au kuolewa wengi wanatamani sana maisha ya kuwa na wenza wa maisha yao. Harusi nyingi huandaliwa kwa gharama kubwa kiasi ambacho kwa mtu ambaye huna kitu unaweza kuogopa kutangazia umma kuwa unampango wa kuoa.

  Mara kadhaa nimesikia viongozi wa dini wakilalama kuwa wale waliowafungisha ndoa siku chache zilizopita wamefika ofisini kutaka ndoa yao ivunjwe au zimeshavunjika. Unaweza kujiuliza na kukosoa watu hawa ukizingatia gharama zilizotumika kuziandaa ndoa hizo kwa maana ya sherehe n.k. “ Suala la kuoa au kuolewa linahitaji uangalifu mkubwa mpaka Kufikia hatua ya kumteua na kumtangaza kuwa huyu ndiyo mtarajiwa wakweli. Kwa mwanamme ambaye anataka kuoa mke ni lazima ajiridhishe kuwa anapendwa kwa dhanti na mchumba wake huyo. Vijana wengi wamekuwa wakilazimisha wapendwe na wasichana kwa kuwapa ofa na zawadi mbalimbali hadi kuwalainisha na kutimiza haja zao, wengi wanaofanya hivyo hawana muda wa kujiuliza swali hili kuwa wasichana hao wanawapenda kwa dhati ya moyo wao? Au wamekubali tu kwa zawadi alizotoa? Athari za mwanaume kulazimisha mahusiano hadi kufikia hatua ya ndoa huwagharimu wengi kwani ndoa za aina hiyo haziishi misukosuko na kusalitiana.

  Wanaume wengi nimewasikia mitaani wanasema yule binti ananipenda kweli lakini sinampango naye” kwangu mimi hawa wanachezea bahati maana ni nadra na ni bahati ya kipekee unapojikuta msichana ndiye anayekupenda, wasichana/wanawake wengi hulazimishwa kupenda maana wengi hawana uwezo au niseme sio utamaduni kumtamkia kijana wa kiume kuwa anampenda. Hivyo basi ili kijana ufikie hatua ya kutamka kuwa unataka kuoa lazima ujiridhishe kuwa huyo unayemuoa anakupenda kwa upendo wa dhati pengine zaidi yaw ewe unavyompenda. Kinyume chake usije ukashangaa usaliti ukiinuka maana aliyemuyoni mwake sio wewe!!! hivyo usijaribu kuoa binti ambaye hakupendi kwa maana ya kuwa wewe ndiye uliyemlazimisha kwa vishawishi kadha wakadha. (ushauri huu unawahusu vijana wa kiume wanaotaka kuoa)
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Sasa mbona umeshatoa majibu mwenyewe??? Asante sana
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo mwanamke yeye ndo wakupenda zaidi alafu afanyiwe usiyotaka mwanaume afanyiwe?Unajua kwamba wapo wadada wanaolazimisha mapenzi?Tengeneza balansi...sema watu wahakikishe wanapendana na sio wanapendwa tu.Unajua kwamba wanaopendwa tu hua wa kwanza kuwakimbia wenzao siku wakikutana na wanaowapenda wao?Ndo unaanza kusikia mtu akiuliza siku zote alikua wapi huyu mpaka nikaoa mtu nisiyempenda!?BALANSI INAHITAJIKA ILI PANDE ZOTE MBILI ZIRIDHIKE.
   
 4. A

  Anold JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  kimsingi nia yangu siyo kutoa swali ni kuelimisha vijana.
   
 5. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mpendane wote.
   
 6. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Je mwanamke unayetaka kuoa anakupenda au wewe ndiyo umempenda?

  Nilivyoona hizo red tu nikajua ni swali
   
 7. A

  Anold JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  kama utafuatilia vidhuri hiyo tahadhari ni kwa wanaume tu. Ndiyo walengwa wakuu
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo wakiwa walengwa wakuu ndo uwashauri waoe wasichana wanaowapenda sana hata kama wao hawawapendi sana?Kama nia yako ilikua kuondoa tatizo hujafanya lolote maana badala ya mwanamke kuvunja ndoa kwasababu hakupenda sana..mwanaume ndo atakaefanya hivyo.Hapo umesaidia nini?Sema watu waoe watu wanaopendana na o na sio wanaopendwa nao!
   
 9. A

  Anold JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Ni kweli ila usijali angalia huo ushauri kama unamatic ukiona hauna kauka
   
 10. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Anold bana si ndo maana nikasema mbona majibu ushayatoa na nikumaanisha nimesoma na kuelewa thanx bana
   
 11. A

  Anold JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Nimewalenga vijana wa kiume maana wanapovutiwa na mavazi tu ya msichana hupeleka maombi ya ndoa bila kuangalia kuwa je huyo dada anautayari? "usiombe kuoa mke ambaye kwake wewe hukuwa chaguo lake ila amelazimika utajuta kuzaliwa maana ikitokea vishawishi vyako vimefika tamati umekwisha"
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ila ni bora kuoa mwanamke ambae sio chaguo lako 100/100?
   
 13. L'AMOUR

  L'AMOUR Senior Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wataalam wanashauri uishi na mtu anayekupenda sio unayempenda hii itakusaidia kuepuka mambo mengi. Wewe unatakiwa kuangalia tu kama unaweza kumpenda hata kama itakuchukua muda kujifunza kumpenda kwa kuwa love takes time. Vinginevyo ndio hadithi hizi za kila siku tunazosimuliana hapa jamvini. Ukijua kuwa unapendwa na ukaheshimu hilo utajikuta unafika mbali sana kimapenzi.
   
 14. A

  Anold JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  wanaume wengi sana wanapoingia kwenye mahusiano hawasukumwi na upendo bali ni matamanio. Kama huamini siku ukiongozana na mume wako au mtu wako hata kama unaamini mnapendana kiasi gani angalia mwonekano wake mnapopishana au kuona wanawake wengine. Ndiyo maana unaweza kumpenda sana kijana na kujenga matumaini makubwa ila bado akakumwaga na kukuona unajipendekeza. Hii mada ni pana inawezekana ninachotaka kukieleza kisieleweke vizuri.
   
 15. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Anzisha sred mkuu..hilo unalotaka kuongea nalo ni somo
   
 16. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  duh!! haya sasa, mie sina cha kusema nimelewa ugali wa bada na mlenda!
   
 17. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hebu tujaribu kuigeuza hii mada iwe the other way round tuone itakuwaje..
  kuoana ni kupendana bwana, na mwanamke akisema hivyo si itakuw balaa ndani ya ndoa.mhh mie simoo
  waseme waliooana ndo wana maexperience ya kujibu hili swali
   
Loading...