Je,mwanamke akiwa ananyonyesha anaweza kupata ujauzito?

sodeely

Senior Member
Oct 3, 2011
187
117
Mimi nina mke wangu na ananyonyesha mtoto wa miezi 7,lakini kutokana na hali halisi ya kibinadamu tumejikuta tukifanya mapenzi..bila kinga..
Je,anaweza kushika mimba?
 
inategemea!mimba inawezekana!kama mwanamke anaenda mzunguko wake wa hedhi!
 
Mara nyingi kama ananyonyesha muda wote mzunguko wa hedhi husimama, lakini kama ni mwajiriwa anamwacha mtoto nyumbani muda mrefu na kunyonyesha wakati wa usiku peke yake basi mzunguko wake hurejea kawaida. Ikitokea hujachukua tahadhari, anaweza kushtukia mimba imeshika kwa ule mzunguko wa kwanza baada ya kunyonyesha, tafadhali mjali mwenzio na chukua hatua stahiki.
 
Mimi nina mke wangu na ananyonyesha mtoto wa miezi 7,lakini kutokana na hali halisi ya kibinadamu tumejikuta tukifanya mapenzi..bila kinga..
Je,anaweza kushika mimba?

Ndio, anaweza kushika mimba.
 
Mama akiwa ananyonyesha kwa ukamilifu (exclusive breastfeeding - kunyonyesha bila chakula kingine au maji kwa mtoto) ana kinga ya kutopata mimba kufikia asilimia 98 (natural contraception protection) mpaka miezi sita baada ya kujifungua. Kinga hii huwa nzuri zaidi mama anaponyonyesha mara nyingi zaidi na kwa muda mrefu zaidi kwani anaongeza uzalishwaji wa hormone inayoitwa prolactine ambayo inazuia upevushwaji wa yai (essential for contraception effect) na pia inazuia menstruation.

Lakini inawezekana mama akapevusha yai (ovulate) hata kabla hajaanza kupata siku zake, kwa hiyo kuna uwezekano wa mama anayenyonyesha kupata ujauzito hata kabla hajaona siku zake. Kwa hiyo akina mama wanaonyesha exculusively wanashauriwa waanze kutumia njia ya uzazi wa mpango miezi mitatu baada ya kujifungua, vinginevyo ajiandae kutengeneza kapacha kalikopishana miezi na pacha wa kwanza.

Mama ambaye hafanyi exclusive breastfeeding au hanyonyeshi kabisa ana uwezekano wa kupevusha yai (ovulate) mapema zaidi yaani hata wiki ya 6 - 12 baada ya kujifungua. Kwa hivyo huyu kitaalmu na kiutafiti anatakiwa aanze kutumia njia ya uzazi wa mpango wiki ya 3 baada ya kujifungua.

Njia za uzazi wa mpango zinazoshauriwa kwa mama anaenyonyesha ni pamoja na vidonge vyenye dawa moja (mini pill au progesterone only pill) ambavyo havipunguzi uzalishwaji wa maziwa kama vidonge vya dawa mbili (combined oral contraceptive pills). Pia anaweza kutumia vijiti ama sindano, hizi nazo zina progesterone ambayo haina effect kwenye milk production. Kama amemaliza uzazi anaweza kufunga mirija.

Kwa yule asiyenyonyesha anaweza kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango. IUCDs (Loop) pia zinaweza kutumiwa na mama anayenyonyesha na asiyenyonyesha.

kwa hiyo sodeely tumia protection. Miezi saba toka kujifungua mkeo aweza pata mimba hata kama hajaanza menstruation.
 
naongea kwa herufi kubwa kuwa jiandae kupata pacha hapooo. Sasa miez 7 yote bado tu hujafanya Mpango? Kikawaida mwsho wa kujiamini ni miez 6 tu. Lakin hata hyo 6 ni hatari pia maana wanawake wanatofautiana sana.
 
naongea kwa herufi kubwa kuwa jiandae kupata pacha hapooo. Sasa miez 7 yote bado tu hujafanya Mpango? Kikawaida mwsho wa kujiamini ni miez 6 tu. Lakin hata hyo 6 ni hatari pia maana wanawake wanatofautiana sana.
Uzi wa mwaka 2011 huu we jamaa.
 
Back
Top Bottom