Je,Mwanamke akishajifungua kwa njia ya upasuaji haitawezekana tena kujifungua kwa njia ya kawaida?

Mchumiajuone

Member
Dec 15, 2016
66
33
Mke wangu alijifungua kwa mara ya kwanza kwa njia ya kawaida.
Kisha mtoto wa pili alijifungua kupitia upasuaji.
Na sasa ana ujauzito mwingine,ila wakati naandaa hospitali kaajili ya kujifungulia kuna daktari ameniambia anapaswa kujifungua kwa upasuaji kwakuwa alishawahi kufanyiwa upasuaji.
Naomba wataalamu mnifafanulie kwanini inashauriwa afanyiwe upasuaji.

NB: kiafya hana tatizo lolote.
 
Pole sana mkuu! Shida kubwa inayoweza kutokea ikiwa atajifungua kwa njia ya kawaida sasa hivi (Trial of Labour after Caesarean Section au TOLAC) ni mfuko wake wa uzazi (uterus) kupasuka (uterine rupture), ambacho kinaweza kuleta tabu kwake au kwa mtoto. Na bahati mbaya centres zetu nyingine nyingi hazina uwezo wa kuhandle complications,na ndio maana mara nyingi wanapendelea mtu aliyejifungua kwa upasuaji hata ikiwa mara moja, basi ajifungue kwa upasuaji hadi mwishoni, na ikibidi kuwa otherwise, kwa maana ya kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji (vaginal delivery following a previous Caesarean delivery) basi wanapenda kuwe na Consultant Obstetrician kwa ajili ya kutoa msaada na kuintervene iwapo complications zitatokea. Na zaidi, centres nyingi hupenda kumfunga kizazi (hysterectomy) mtu aliyejifungua zaidi ya mara 3 kwa upasuaji kwa kuhofia suala hilo hilo la uterine rupture.
 
Uwezekano wa kujifungua kwa njia ya kawaida ni mdogo.....
Kwan tatizo ilikuwa nini hadi ajifungue kwa op
 
Kwa mtu ambaye Ali opt cs je na last delivery and ni miaka saba anaweza zaa kawaida?
 
Pole sana mkuu! Shida kubwa inayoweza kutokea ikiwa atajifungua kwa njia ya kawaida sasa hivi (Trial of Labour after Caesarean Section au TOLAC) ni mfuko wake wa uzazi (uterus) kupasuka (uterine rupture), ambacho kinaweza kuleta tabu kwake au kwa mtoto. Na bahati mbaya centres zetu nyingine nyingi hazina uwezo wa kuhandle complications,na ndio maana mara nyingi wanapendelea mtu aliyejifungua kwa upasuaji hata ikiwa mara moja, basi ajifungue kwa upasuaji hadi mwishoni, na ikibidi kuwa otherwise, kwa maana ya kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji (vaginal delivery following a previous Caesarean delivery) basi wanapenda kuwe na Consultant Obstetrician kwa ajili ya kutoa msaada na kuintervene iwapo complications zitatokea. Na zaidi, centres nyingi hupenda kumfunga kizazi (hysterectomy) mtu aliyejifungua zaidi ya mara 3 kwa upasuaji kwa kuhofia suala hilo hilo la uterine rupture.
Exactly
 
kwa kipindi hiki ni ngumu.ingawa mama yangu alijifingua kwa Op mara 2 kisha kawaida mapacha mara 3.
 
Mkuu ukweli kwa kipindi hiki ukubali kuweka rehani uhai,kwa uvivu wa mkunga anakizuwia kusukuma kwa wakati kitakacho tokea hapo afadhali ya fistula inatibika!
Duuh hapo kweli vinginevyo ulipie fast track au private hospital labda waeza pata huduma nzuri ukiwa chini ya uangalizi wa gynecologist
 
Kwa CPD(cephalo pelvic disproportional) ni ngumu kidogo mama kuja kujifungua kwa njia ya kawaida ila sababu nyingine kama Mtoto Mkubwa,Malpresentation/malposition,maternal/fetal distress,kifafa cha mimba,placenta previa/abruptio mama ananafasi kubwa ya kujifungua kawaida mimba zijazo
Ila wanashauri angalau awe amekaa miaka3 kabla ya ujauzito mwingine,watoto wasiwe mapacha na pia jeraha lililopita lilipona bila Maambukizi(Sepsis)

Na inashauriwa kama mama alijfungua kwa Upasuaji next time ajifungulie hosp kubwa ili ikitokea dharura yote aweze saidiwa na sio zahanati labda awe ni mtoto wa kupokea tu.
 
kwa kipindi hiki ni ngumu.ingawa mama yangu alijifingua kwa Op mara 2 kisha kawaida mapacha mara 3.
Aisee! 2 previous scars, multiple pregnancy tayari ningekuwa na indication za kutosha kufanya C-section. Ilikuwa too risky kusubiri SVD
 
Nashukuru sana kwa michango yenu,nimefaidika na nitayafanyia kazi mawazo yenu ya kitaalamu
 
Pole sana mkuu! Shida kubwa inayoweza kutokea ikiwa atajifungua kwa njia ya kawaida sasa hivi (Trial of Labour after Caesarean Section au TOLAC) ni mfuko wake wa uzazi (uterus) kupasuka (uterine rupture), ambacho kinaweza kuleta tabu kwake au kwa mtoto. Na bahati mbaya centres zetu nyingine nyingi hazina uwezo wa kuhandle complications,na ndio maana mara nyingi wanapendelea mtu aliyejifungua kwa upasuaji hata ikiwa mara moja, basi ajifungue kwa upasuaji hadi mwishoni, na ikibidi kuwa otherwise, kwa maana ya kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji (vaginal delivery following a previous Caesarean delivery) basi wanapenda kuwe na Consultant Obstetrician kwa ajili ya kutoa msaada na kuintervene iwapo complications zitatokea. Na zaidi, centres nyingi hupenda kumfunga kizazi (hysterectomy) mtu aliyejifungua zaidi ya mara 3 kwa upasuaji kwa kuhofia suala hilo hilo la uterine rupture.
Nashukuru mkuu.
Ila nina swali la ufahamu.
Je,kuanzia wiki ya ngapi yafaa kupanga huo upasuaji.
 
Pole sana mkuu! Shida kubwa inayoweza kutokea ikiwa atajifungua kwa njia ya kawaida sasa hivi (Trial of Labour after Caesarean Section au TOLAC) ni mfuko wake wa uzazi (uterus) kupasuka (uterine rupture), ambacho kinaweza kuleta tabu kwake au kwa mtoto. Na bahati mbaya centres zetu nyingine nyingi hazina uwezo wa kuhandle complications,na ndio maana mara nyingi wanapendelea mtu aliyejifungua kwa upasuaji hata ikiwa mara moja, basi ajifungue kwa upasuaji hadi mwishoni, na ikibidi kuwa otherwise, kwa maana ya kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji (vaginal delivery following a previous Caesarean delivery) basi wanapenda kuwe na Consultant Obstetrician kwa ajili ya kutoa msaada na kuintervene iwapo complications zitatokea. Na zaidi, centres nyingi hupenda kumfunga kizazi (hysterectomy) mtu aliyejifungua zaidi ya mara 3 kwa upasuaji kwa kuhofia suala hilo hilo la uterine rupture.
"Once Caesarean section always Caesarean section" ni policy ya kizamani na imeshapitwa na wakati Mama aliyepasuliwa anaweza kuzaa kawaida endapo tatizo lilimfanya apasuliwe awali halitajirudia ktk mimba ijayo na kama atakaa miaka 2 na zaidi kabla ya mimba nyingine!mara nyingi wakina mama waliofanyiwa upasuaji kwa shida ya mtoto km Fetal distress mlalo mbaya wa mtoto au aliyeafanyiwa surgery kwa ajili ya kifafa cha mimba ana chance ya kujifungua kawaida kwenye mimba zijazo unless km tatizo la awali litajirudia mama pekee ambaye aruhusiwi kwa Trial of labor ni kama ana nyonga ya kiume (Android pelvis)inayompelekea kupata CPD na baadae Uchungu pingamizi au Mama matatizo ya moyo au aliyepata Fistula katika mimba iliyopita nk.Lastly Hysterectomy maana yake ni kuondoa kizazi si kufunga kizazi,kufunga kizazi kunaitwa Tubal ligation inafanywa kwa mama anayependa kukamilisha uzazi au Mama aliyefanyiwa C/S zaidi ya 3 ambaye kuendelea na uzazi kunaweza kuhatarisha maisha yake!
 
Si lazima mimi nifanya kazi na mdada mtoto wa kwanza alijifungua kwaupasuaji wa pili amejifungua kawaida so sidhani kuwa haiwezekani
 
Back
Top Bottom