Je Mwanadamu atafufuliwa akiwa na Umri Gani?

Katika biblia kuna maneno ya mungu na yasiyokuwa maneno ya mungu, maneno ya mungu ni yale ambayo yanatoka kinywani kwa yesu na ukilisoma unaweza ukaona kabisa kama hapa yesu anaongea, na maandiko ya namna hii ukiangalia utayakuta kwenye biblia ingawa si mengi, lakini hapo inaonesha wazi kwamba muongeaji si yesu ni mtu mwngine, angekuwa yesu asinge ongea hvyo katika nafsi ya mtu mwingine.
Mkuu unajua maana ya vitabu vya Injili?
 
Sio mbaya ukanambia maana yake.
Kwa kuwa hujui siyo mbaya mjadala ukaishia hapa.

Kukueleza maana yake itachukua muda sana hadi upate uelewa wa kuendelea na majadiliano.

Mwisho:Kwanini unabisha kitu ambacho hujui?
 
Kwa kuwa hujui siyo mbaya mjadala ukaishia hapa.

Kukueleza maana yake itachukua muda sana hadi upate uelewa wa kuendelea na majadiliano.

Mwisho:Kwanini unabisha kitu ambacho hujui?
Ha ha ha haaaa, ok najua ila nieleweshe nione nawe uelewa wako kama tuko sawa.
 
Roho haizeeki haina ukubwa wala udogo, so tutafufuliwa wote tukiwa na umri sawa wa Kiroho, japo kimwili tulikuwa na maumbo na umri tofauti, kama wewe ni mtu mzima utakuwa unajishangaa kuwa japo wewe ni mtu mzima lakini bado hunajiona hauna mabadiriko yoyote Kiroho yaani haujifeel kuwa ni mtoto au kuwa ni mtu mzima
Okay nimekupata. Sasa kule mbinguni zitakwenda Roho au miili?
 
Hahahaha..........aahyi,....swali tata.
Hilo rahisi sana.Watu wanafufuliwa kwa ajili ya kupewa hukumu kwa yale waliyo yatenda wakiwa duniani,waliotenda mema watalipwa pepo na ziada na waliotenda maovu watalipwa moto.

Siku hiyo mpaka viungo vitatoa ushahidi,kwa wale wajuao ya kuwa kuongea mpaka uwe na mdomo ndio uongee,wajue wanaufahamu mdogo sana juu ya mambo ya kielimu,siku hiyo kila kiumbe kitapewa haki yake,kama kulikuwa na mnyama duniani alimpiga mnyama mwenzie kwa dhuluma basi wataitwa wote mbele ya uwanja wa kisimamo,itatoka amri kwa yule aliyepigwa kwa dhuluma na mnyama mwenzie ataambiwa amrudishie kisha wataambiwa kuweni mchanga wenye kupotea.Hii inatuweka wazi ya kuwa ni viumbe viwili tu (Thaqalayni) ni ndio watalipwa pepo na moto.
 
Na aliye kufa kabla hajazaliwa je huyo atafufuliwa vipi?
Kwa ufupi kuna wale watoto waliokufa kabla ya kubalehe,katika uislamu binadamu anaandikiwa dhambi pale tu anapokuwa amebaleghe,yaani kalamu ya kuandika mema na maovu yake inakuwa inafanya kazi,ndio maana machizi kalamu zao za kuandika mema na maovu zinakuwa zimesimama,sababu lile sharti la kuwa na akili timamu linakuwa limepomoka kwa muda ule.Tukirudi katika msingi wa swali lako,nao watafufuliwa na watapewa mtihani watao faulu watalipwa pepo na watakao feli watalipwa moto.

Na kuna wale watu ambao maisha yao yote wameishi hapa duniani bila kufikiwa na ujumbe wa Mola wao mlezi,hawa nao watapewa mtihani,kisha watakao faulu watapewa pewa pepo na watakao feli watapewa moto.Hakika hakitaachwa kitu,na Mola mjuzi mwingi wa kuadhibu na mjuzi.
 
Okay nimekupata. Sasa kule mbinguni zitakwenda Roho au miili?

Kaka mwili unafukiwa na kuwa vumbi, kinachokwenda ni roho labda na miili ambayo haiwezi kuwa sawa na hii
Ukisoma baadhi ya maandiko yanasema, Mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa kwa sababu watu watakuwa kwenye mfumo mwingine wa Kiroho
 
Hapa kama ulivyokufa,ndivyo utakavyofufuliwa yani kama ulikuwa na makagali kubwa utakuwa Nayo hiyo hiyo
 
MAANDIKO YANASEMA HIVI, KUHUSU UFUFUO;

(1) KATIKA KITABU CHA

UFUNUO 20:

11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.


(2) KATIKA KITABU CHA

1 WAKORINTHO 15:

Mwili wa Ufufuo

35 Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?
36 Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa;
37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo;
38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.
39 Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.
40 Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.
41 Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota.
42 Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika;
43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu;
44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko.
45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.
46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho.
47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.
48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.
49 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.
50 Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika.
51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?
56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.
57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
58 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
 
Mkuu hizo issue si za kweli ni mistori ya kutunga tu.

Hivi unajua Yesu ali wahidi wale watu walioishi kipindi chake kuwa angerudi kabla wao hawajafa?.......yaani angerudi kabla ya kufa kwa wale waliokuwa wakimsikiliza.

Mat. 16:27-28, Kwa maana mwana wa Adam atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kadiri ya matendo yake. Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hamtaonja mauti kabla ya kumwona mwana wa Adam akija katika ufalme wake.

Huu utabiri wa Yesu kwenye Mathayo 16:27-28, ulifeli mara baada ya vifo vya waliokuwa wakimsikiliza unless kama kuna watu walioishi nyakati za Yesu ambao watukuwa hai hadi hivi sasa.

Kuna watu walioishi nyakati za Yesu walioamini kuwa angerudi kabla wao hawajafa lakini hadi leo ni miaka 2000 hajarudi.
Ufufuo plus ujio wa pili ni kama hekaya za Abunuasi, endeleeni kusubiri mkiamini atakuja.,.....lakini kaeni mkijua hakuna kitu kama hicho.
Kuna mungu??
 
Back
Top Bottom