Je Mwanadamu atafufuliwa akiwa na Umri Gani?

Tangu nizaliwe leo ndio nimesikia hiki kitu ulichosema.

Hebu tueleze haya mambo uliyapata wapi?..........Binafsi nadhani ni propaganda za kutengenezwa ili zi-fit utabiri wa Yesu ambao haukutimia.

Ndio maana nimesema ipo simulizi yaani "church historical tradition" inasema hayo! Hatuna maana kuwa imethibitishwa rasmi, ila ipo simulizi ya jinsi hiyo. Ni kama zile zinazohusu maisha ya baadaye ya wanafunzi wa Yesu, kwamba fulani alifia wapi na fulani alikufa namna gani! Huwezi kuzikataa hizo kwani zipo kwa kila dini. Hizi zinaaminika ikiwa zitakuwa na ushahidi wa waandishi wengi ama vyanzo vingi vya kihistoria. Nipo Safari nje ya nchi nitakapo rudi nita-attach source moja wapo ya hii Habari.
 
Ndio maana nimesema ipo simulizi yaani "church historical tradition" inasema hayo! Hatuna maana kuwa imethibitishwa rasmi, ila ipo simulizi ya jinsi hiyo. Ni kama zile zinazohusu maisha ya baadaye ya wanafunzi wa Yesu, kwamba fulani alifia wapi na fulani alikufa namna gani! Huwezi kuzikataa hizo kwani zipo kwa kila dini. Hizi zinaaminika ikiwa zitakuwa na ushahidi wa waandishi wengi ama vyanzo vingi vya kihistoria. Nipo Safari nje ya nchi nitakapo rudi nita-attach source moja wapo ya hii Habari.
Ok.
 
Maswali kuhusu ufufuo hayajaanza Leo tangu enzi za mtume(saw).m/Mungu anasema ktk qurani.je Titapokuwa ktk mapande yaliyovurugika tutarudishwa katika umbo jipya
 
Mkuu hizo issue si za kweli ni mistori ya kutunga tu.

Hivi unajua Yesu ali wahidi wale watu walioishi kipindi chake kuwa angerudi kabla wao hawajafa?.......yaani angerudi kabla ya kufa kwa wale waliokuwa wakimsikiliza.

Mat. 16:27-28, Kwa maana mwana wa Adam atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kadiri ya matendo yake. Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hamtaonja mauti kabla ya kumwona mwana wa Adam akija katika ufalme wake.

Huu utabiri wa Yesu kwenye Mathayo 16:27-28, ulifeli mara baada ya vifo vya waliokuwa wakimsikiliza unless kama kuna watu walioishi nyakati za Yesu ambao watukuwa hai hadi hivi sasa.

Kuna watu walioishi nyakati za Yesu walioamini kuwa angerudi kabla wao hawajafa lakini hadi leo ni miaka 2000 hajarudi.
Ufufuo plus ujio wa pili ni kama hekaya za Abunuasi, endeleeni kusubiri mkiamini atakuja.,.....lakini kaeni mkijua hakuna kitu kama hicho.
Ktk hyo aya naamini hayo sio maneno ya Yesu, km yangekuwa maneno yake asingeongea km anamzungumzia mtu.
 
Habari zenu wana JF Poleni na Mihangaiko ya Dunia hii.

Okay leo nina swali kuhusu suala la siku ya kufufuliwa wanadamu wote. (Kwa wale wanaoamini kua baada ya kifo kuna siku ambayo tutafufuliwa)

Ningependa kufahamu

Je mwanadamu atafufuliwa akiwa na umri Gani?

kama atafufuliwa na umri aliokufa nao je wale wabibi ambao wamekufa hawaoni, hawana meno, wanajisaidia vitandani vipi watafaidi huko peponi?

Na je mtoto mchanga akifufuliwa hivyo hivyo nae atafaidi vipi ufalme wa mbinguni?

Asanteni.

c3cc96485cee8ffd6ca6ee0c73532b78.jpg

Roho haizeeki haina ukubwa wala udogo, so tutafufuliwa wote tukiwa na umri sawa wa Kiroho, japo kimwili tulikuwa na maumbo na umri tofauti, kama wewe ni mtu mzima utakuwa unajishangaa kuwa japo wewe ni mtu mzima lakini bado hunajiona hauna mabadiriko yoyote Kiroho yaani haujifeel kuwa ni mtoto au kuwa ni mtu mzima
 
Wale watakao jaaliwa kwenda peponi tu Allah atujalie na sisi tuende pepeponi
 
Kwahiyo vitabu vya dini ni story za watu wa kale siyo?
Katika biblia kuna maneno ya mungu na yasiyokuwa maneno ya mungu, maneno ya mungu ni yale ambayo yanatoka kinywani kwa yesu na ukilisoma unaweza ukaona kabisa kama hapa yesu anaongea, na maandiko ya namna hii ukiangalia utayakuta kwenye biblia ingawa si mengi, lakini hapo inaonesha wazi kwamba muongeaji si yesu ni mtu mwngine, angekuwa yesu asinge ongea hvyo katika nafsi ya mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom