Je, Mwamposa yule "mtume" muasisi wa kukanyaga mafuta ya upako ni dhehebu gani? Je ni Calvary Assemblies of God ya Prophet Maboya?

Kumbeeeeeee
Mimi sikujua kama amri imetolewa na nabii wakae kimya kwenye mitandao.

Mimi kumsema nabii na mtume nimetishiwa kufa, na kwamba nichunge ulimi naongea sana nisije kumlaumu mtu yeyote wakati napewa cha moto.
Serious?Aisee ilikuwaje ni hapa JF au nje ya JF,njoo inbox unipe abc za hiyo kitu.Ulitaka kutia mchanga kitumbua cha watu?
 
Ucjal kwa kuwa asha mwaga damu itapatikana tu
Ndio ni mwanawe MTUME MABOYA kwa kiroho .Alikuwa muumini wake tu wa kawaida pale Arusha kanisani kwake akamfundisha ,kumlea hadi akaenda fungua kanisa la Calvary Assemblies Of God pale Moshi ambako vifo vimetokea, baadaye akafungua huduma ingine Dar es salaam ambayo iko pale Kawe nayo iko Chini ya CAG la Maboya. Na ASKOFU NA MTUME MABOYA ndie ASKOFU WAKE MKUU

Mtume Mwamposya huwa anahudumia makanisa mawili kwa Mpigo huwa yuko Dar es salaam na Moshi .Huweza kuhudumu kote kwa kutumia ndege za abiria.Akimaliza huku anapanda ndege anaenda kwingine kuhudumia.

Hizi ndege mara ingine zinamchelewesha huduma yake.Tunamwomba Mungu AMPE ndege yake binafsi ambayo atakuwa nauwezo wa kuondoka muda wowote atakao na kwenda kuhudumu popote sababu anahitajika mikoa yote Tanzania lakini sababu hana ndege yake binafsi mfano ya kuendesha ibada ya asubuhi labda Mwanza na ibada ingine Dar kwa siku inakuwa vigumu

Tuko kwenye maombi Mungu ampe ndege ya aina ya Gulfstream ina mbio za kutosha kwa private jets.Tushirikiane kumwombea apate

BULLDOZER MWAMPOSYA HUYOOOO

View attachment 1350819

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serious?Aisee ilikuwaje ni hapa JF au nje ya JF,njoo inbox unipe abc za hiyo kitu.Ulitaka kutia mchanga kitumbua cha watu?

Usishituke sana wanajiona kama Mungu watu (ila wanajiita manabii)Na atakae leta fyokofyoko atakufa.

Na hapa JF tunafurahisha genge tu hizi kelele hazimnyimi usingizi kabisa
 
Wako kibao mbona.Wako binadamu wengine hata kufa hawafi Mfano kwenye Biblia Henoko hakufa,Musa hakufa ,na Eliya hakufa.

Mungu hakusema kila binadamu ataugua au kufa .Kuna wengine wengi tu akiahidi hawatakufa Mfano siku ya mwisho wa dunia kutakuwepo kundi la watu ambao watakuwa hawajafa .Ambao watanyakuliwa Kama walikuwa watakatifu watanyakuliwa wazima wazima .

Kwa hiyo usisikile hata ule upuuzi wa anapizikwa mtu kuwa ouhh mwenzetu katakngulia kufa na sisi tuko njiani kufa kumfuata sio kweli inategemea si.kila mtu atakufa parapanda ikilia ya meisho wa dunia ambao haujulikani Ni lini wengine watanyakuliwa wazima wazima
Kwaiyo kama utakuwa unadhambi hunyakuliwi unabaki kwa dunia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemsikia Prophet Maboya akizungumzia msiba mkubwa wa watu kufia kwenye HUDUMA kwa kukanyagana. Najiuliza je Mwamposa yuko kwenye dhehebu la CAG LA Maboya?

Anayejua atufahamishe.
Hivi karibuni niliwahi kusema humu jukwaani kuwa Roho Mtakatifu huwa hahitaji kusaidiwa na chochote ikiwa ni pamoja na mafuta ya upako; hahitaji chochote cha kumsaidia katika utendaji wake wa kazi, zaidi ya yeye mwenyewe. Naendelea kusikitika sana kwa kilichotokea Moshi, ila naweza kusema kuwa ni indicator kubwa kuwa Roho Mtakatifu hafurahishwi na mafuta ya upako au kitu kingine chochote kile kinachofana na na hicho; na kama watu wataendelea, kuna uwezekano yakaja yakatokea madhara makubwa zadi huko mbele.

Kinachotokea kwa waumini wa Mwamposa ni kwamba kuna dua na sala au maombi wanayofanya halafu Roho Mtakatifu anawajibu, na wanapokea sawasawa kabisa kulingana na walivyoomba, mtendaji akiwa ni Roho Mtakatifu perce, ila sasa wanaopokea wanaminishwa kuwa ni mafuta ya upako badala ya kueleweshwa kuwa ni Roho Mtakatifu. Kilichotokea kwa waumini hawa mimi naweza kusema ni mgogoro kati ya mafuta ya upako na hasira ya Roho Mtakatifu kwamba yeye RM hawezi kuwa anatenda kazi halafu sifa zinaelekezwa kwenye mafuta ya upako, badala ya kuelekezwa kwake. Waache kwa sababu wakiendelea yatakuja kutokea makubwa zaidi!
 
waroho yaani walaku/ wenye hamu kupitiliza
Asant, maana kuna dhehebu moja mitaa ya kanda ya ziwani kuanzia Mwanza, Mara mpaka Kenya linaitwa Roho na vijitawi kibao. Wanavaa kanzu na baragashia zenye msalaba mwekundu kwa wanaume na wanawake vitambaa kichwani hawatembei vichwa wazi.
Wana piga ngoma kama dufu ila zakwao ni kubwa, mfano wa zile ngoma walizokuja nazo mashabiki wa Gor Mahia kutoka Kenya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asant, maana kuna dhehebu moja mitaa ya kanda ya ziwani kuanzia Mwanza, Mara mpaka Kenya linaitwa Roho na vijitawi kibao. Wanavaa kanzu na baragashia zenye msalaba mwekundu kwa wanaume na wanawake vitambaa kichwani hawatembei vichwa wazi.
Wana piga ngoma kama dufu ila zakwao ni kubwa, mfano wa zile ngoma walizokuja nazo mashabiki wa Gor Mahia kutoka Kenya.

Sent using Jamii Forums mobile app
hahah hilo kanisa linamfaa Nabii Tito
 
Back
Top Bottom