Je, Mwamposa yule "mtume" muasisi wa kukanyaga mafuta ya upako ni dhehebu gani? Je ni Calvary Assemblies of God ya Prophet Maboya?

Bila shaka ni muumini wa mwaposa pasi na shaka kwa yote yaliotokea bado uko unampambania baba yako wa kiroho kweli ... majeshi majeshi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nmeona sehem unasema ungemfyeka na mapanga kama Wewe ungekua Nuhu baba wa mtoto

Kwa kifupi ungeua, Najua Wewe ni mwanachama wa fisiem
Kufyeka mtu panga sio lazima afe Ila Cha Moto aweza kiona inategemea ufyekaji na eneo la kufyeka na upanga ulikogeukia
Panga hutumika Kama fimbo kwa wakurya.Ukileta za kuleta unalo
 
Ndio ni mwanawe MTUME MABOYA kwa kiroho .Alikuwa muumini wake tu wa kawaida pale Arusha kanisani kwake akamfundisha ,kumlea hadi akaenda fungua kanisa la Calvary Assemblies Of God pale Moshi ambako vifo vimetokea, baadaye akafungua huduma ingine Dar es salaam ambayo iko pale Kawe nayo iko Chini ya CAG la Maboya. Na ASKOFU NA MTUME MABOYA ndie ASKOFU WAKE MKUU

Mtume Mwamposya huwa anahudumia makanisa mawili kwa Mpigo huwa yuko Dar es salaam na Moshi .Huweza kuhudumu kote kwa kutumia ndege za abiria.Akimaliza huku anapanda ndege anaenda kwingine kuhudumia.

Hizi ndege mara ingine zinamchelewesha huduma yake.Tunamwomba Mungu AMPE ndege yake binafsi ambayo atakuwa nauwezo wa kuondoka muda wowote atakao na kwenda kuhudumu popote sababu anahitajika mikoa yote Tanzania lakini sababu hana ndege yake binafsi mfano ya kuendesha ibada ya asubuhi labda Mwanza na ibada ingine Dar kwa siku inakuwa vigumu

Tuko kwenye maombi Mungu ampe ndege ya aina ya Gulfstream ina mbio za kutosha kwa private jets.Tushirikiane kumwombea apate

BULLDOZER MWAMPOSYA HUYOOOO

View attachment 1350819

Hawezi ku delegate wachungaji baadhi wawe wanafanya huduma moshi ni lazima gani kila huduma afanye yeye


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wewe si mmeambiwa mkae kimya kwenye mitandao kumbe na wewe ni wa kule?Naomba uzingatie kuna thread kuna manbo nilkujibu naomba ukayasome upya yamkini Mungu akakusaidia.
Imani ni kitu chenye nguvu natamani niandike vitu hapa yamkini ukafumbuka lakini shida kama umepofushwa ufahamu unaweza usinielewe.
Kwa nini mtu mmoja ahudumie makanisa mawili?Je katika wafuasi wake hakuna aliowafundisha wanaoweza kushika hiyo huduma?Ndege atapata ila siyo kutoka kwa Mungu itatoka kwenye pesa zenu ,nyie toeni pesa kwa wingi atanunua.Kama ni yeye anahudumia makanisa mawili ,kwa mfano akiugua ibada hakuna?Je Mungu akimwita?Huduma ndiyo inakuwa imeisha?
Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kisha akawatuma duniani kote tena akawaambia mtaweza kufanya hata mambo makubwa kuliko niliyoyafanya,sasa huyu yeye wanafunzi wake hawaupokei huo upako alio nao ili waweze kuendesha ibada?Je Elisha hakupokea upako kutoka kwa Eliya?Shida iko wapi hapo mbona yeye tu anajichosha unataka kuniambia katika wafuasi wake maelufu hakuna ambaye Mungu amemuona anafaa?There is a hidden agenda.Niishie hapo.
Mitume wa siku hizi ni tofauti na wa kwenye Biblia,wa siku hizi wapo mjini tu ndipo walipotumwa na wao wenyewe ndiyo wanayasimamia makanisa ila wa kwenye biblia walikuwa wanaenfda maeneo tena kule ambako injili haijafika,wanafungua makanisa,wanayasimamia yakikaa vizuri wanaweka watu wao wanaenda kwingine kufanya kazi ya utume.Hawa wetu wa kizazi hiki wako mjini tu ingawa watu wa mjini injili walishaisikia.Bora yule mchungaji mla panya,huyo mkimsikia mpeni support yuko zake huko vijijini anafanya kazi ya Bwana.
Njoo inbox nikusaidie kama unahitaji kuingia mbinguni,otherwise Mithali 14:12 inakuhusu.

Akikujibu ni tag mkuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hawezi ku delegate wachungaji baadhi wawe wanafanya huduma moshi ni lazima gani kila huduma afanye yeye


Sent from my iPhone using JamiiForums
waumini wanamhitaji Sana yeye aende Ana msaidizi wake kule ibada zingine huendesha huyo msaidizi yeye akiwa Dar
 
Kuhusu kuugua hajawahi ugua na hatutarajii augue sababu Mungu humuwazia mema usiku na mchana

Kuhusu kuhudumu makanisa mawili wala sio ajabu mwingine aweza kuwa hata na makanisa sita yote anahudumu mwenyewe.Ndio maana wachungaji wengi mfano marekani wana ndege zao binafsi wanaendesha wenyewe.Ibada ya kwanza aweza endesha morogoro.Saa moja hadi saa tatu.Ibada ya pili akawa Dar es salaam saa nne hadi saa sita mchana mchana ibada ya tatu akaendesha Mwanza saa tisa na nusu hadi kumi na moja na nusu

Hapa tu sisi ndio bado washamba.Wenzetu kule mtu akiwa na kipawa na karama wanamtumia barabara watu wanamhitaji sana unawapelekea ahudumu hata makanisa 100

Kuhusu kama akifa je itakuwaje jibu rahisi tu Mungu atainua mwingine na kuhamisha roho iliyoko ndani yake kwenda kwa huyo mwingine.Roho Ya Musa ilitoka ikaenda kwa Joshua MUSA ALIPOFARIKI,Ya ELIYA ikaenda kwa Elisha nk it is not a big deal .Kwa sasa aendelee kubeba roho yake mpaka hapo Mungu mwenyewe atakapoamua vinginevyo.

Makanisa yote unayoona ya akina Mwingira,Kakobe,SIJUI Rwakatare usijipe pesssure kuwa wakiondoka wakifa itakuwaje.

Kwa jibu lako leo nimeamini kwenye haya makanisa kuna kupumbazwa

Mbona umetoa hoja ya kitoto sawa hataumwa vipi na KUFA hatakufa au ataishi MILELE


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

SOMA HAPO
Yohana 21:25

Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.


Hayo mengine mengi ambayo hayajaandikwa unajua ni yepi wakati Roho ya ufunuo huna !!!!!!!!!

Mkuu ufunuo mwingine huwa unatoka kuzimu tumeona watumishi wengi wa mungu wakiwapotosha watu.
 
Kwa jibu lako leo nimeamini kwenye haya makanisa kuna kupumbazwa

Mbona umetoa hoja ya kitoto sawa hataumwa vipi na KUFA hatakufa au ataishi MILELE


Sent from my iPhone using JamiiForums
Wapi nimeandika hatakufa? Wewe kipofu au?
 

SOMA HAPO
Yohana 21:25

Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.


Hayo mengine mengi ambayo hayajaandikwa unajua ni yepi wakati Roho ya ufunuo huna !!!!!!!!!

Unataka kuniambia ata Yesu alifanya huu upuuzi kweli embu acha kutafsiri maandiko kinyumenyume wewe


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
waumini wanamhitaji Sana yeye aende Ana msaidizi wake kule ibada zingine huendesha huyo msaidizi yeye akiwa Dar
Mimi nilijua waumini wanamhitaji sana Yesu,kumbe wanahitaji mtu awepo,hapo ndipo tunaona kuna shida kwenye mafundisho.Mungu alimwambia Mussa achague wasaidizi ,awawekee mikono ili wamsaidie.Mshauri na yeyey achague wasaidizi ingawa najua hiyo ni ngumu na sababu wanazijua wao.Unatakiwa kuwafundisha watu wako kumtegemea Mungu hata kama haupo waweze kujitegemea.
Hata katika maisha ya kawaida boss ambaye hawezi kufanya delegation of authority kuna tatizo analo.Aidha watu wake hajawafundisha kazi au hawaamini kama wanaweza kusimamia hiyo ofisi, au ana siri zake akiwaachia ofisi zitajulikana.
 
Mimi nilijua waumini wanamhitaji sana Yesu,kumbe wanahitaji mtu awepo,hapo ndipo tunaona kuna shida kwenye mafundisho.Mungu alimwambia Mussa achague wasaidizi ,awawekee mikono ili wamsaidie.Mshauri na yeyey achague wasaidizi ingawa najua hiyo ni ngumu na sababu wanazijua wao.Unatakiwa kuwafundisha watu wako kumtegemea Mungu hata kama haupo waweze kujitegemea.
Hata katika maisha ya kawaida boss ambaye hawezi kufanya delegation of authority kuna tatizo analo.Aidha watu wake hajawafundisha kazi au hawaamini kama wanaweza kusimamia hiyo ofisi, au ana siri zake akiwaachia ofisi zitajulikana.
Karama zinatofautiana Mimi.mwrnyewe akikabidhiwa a ya dar es salaam kwa mtu mwingine naondoka .Mimi.nimeikubali huduma Yake yeye Kama yeye.

Tatizo sio yeye Ni sisi waumini hatutaki kuhudumiwa na yeyote nje ya yeye.Sisi waumini hatutaki Sasa unasemaje Afanye kitu ambacho hatutaki? Akifanya tunaondoka zetu sio kesi

Sisi hatutaki
 
Hebu dadavua hujielewi hali imekuwa worse zaidi ya kabla ya maombi or??
Hapana, ni miaka mingi imepita ila mimi si yule niliyekuwa kabisa mambo yangu mema hayako tena toka alivyoniombea I'm not a good person kabisa natamani kutoka niliko nashindwa
 
Mimi nilijua waumini wanamhitaji sana Yesu,kumbe wanahitaji mtu awepo,hapo ndipo tunaona kuna shida kwenye mafundisho.
Katika makanisa mengi ambayo waumini hawana adabu Ni ya kipentecoste na sababu kubwa Ni hiki ulichoandika hapa.Kuwa watu wanamhitaji Yesu sio mtu.
Unakuta kila muumini anajifanya Yeye na Yesu Yesu na yeye hahitaji mtu.

Anasahau kuwa Mungu kaweka mitume ,manabii na kadhalika ili afanikiwe.Kwa hiyo dharau kwa viongozi iko juu mno na hii Sasa imeenda hadi.makanisa katoliki.nk
Sisi timefundishwa Biblia inasema wazi mwamini Mungu na manabii wake ndipo mtakapofanikiwa.

Kumwamini Mungu tu bila kumwamini nabii hufanikiwii ndio msimamo wetu .Ndio.maana tunamheshimu kupindukia Mwamposya tunajua tukimwamini Mungu tu hakuna Kitu

Mimi nawaamini wote kwa mpigo Yesu na nabii wake sio Yesu peke yake hapana.Namwamini yeye na Nabii wake
Ndio.maana uwepo wake kwangu muhimu mno
 
Karama zinatofautiana Mimi.mwrnyewe akikabidhiwa a ya dar es salaam kwa mtu mwingine naondoka .Mimi.nimeikubali huduma Yake yeye Kama yeye.

Tatizo sio yeye Ni sisi waumini hatutaki kuhudumiwa na yeyote nje ya yeye.Sisi waumini hatutaki Sasa unasemaje Afanye kitu ambacho hatutaki? Akifanya tunaondoka zetu sio kesi

Sisi hatutaki
Ni kweli karama zinatofautiana ila Roho ni yule yule na yeye umpatia kila mtu karama kadri apendavyo yeye Roho na si mtu.Nashukuru unakili ya kwamba tatizo ni nyie waumini,wewe ndivyo unavyosema sisi huku tunaona nyie si tatizo tatizo ni chakula(mafundisho) mliyofundishwa.Niliuliza simwombei augue ila niluliza je akiugua hakuna ibada?Msingi ukiwa mbovu hata nyumba itakuwa shida,mafundisho mliyofundishwa yamewafanya mmtazame mtu na siyo Mungu.Hamjui ya kwamba Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote na huduma yeyote penye Mungu wa kweli anaposimama mtu,si yeye anayehudumu bali ni Roho wa Mungu anatenda kazi kupitia yeye,hii ni level ya juu na inaapply kwa watumishi wanaojitambua na kumjua Mungu.
Watoto wachanga huangalia watu,wanadhani watu ndiyo wanatenda.
Unaposema umeikubali huduma yake yeye kama yeye hilo nalo ni tatizo,kwani hujui kama mtumishi yeye ni mtumwa/mtumishi tu anayetenda kazi ni Roho wa Mungu.Nina mengi ya kueleza ila joto litazidi hivyo sitaki nielezee sana.
Huduma yeyote ya Mungu wa kweli inaweza kufanywa na mtu yeyote ili mradi awe mnyenyekevu na mtii kwa Mungu,ukiona mtumishi anaweza kufanya kitu fulani yeye tu,wala hakuna wengine wanaweza kati ya wanafunzi wake ujue kuna kitu kimekosekana.
Yesu baada ya kuwafundisha wanafunzi wake aliwaacha wakafanye prcatical,wakaombea huko mambo hayakufanikiwa,wakarudi kwake.Akawaambia mambo mengine hayawezekani ispokuwa kwa kufnga na kuomba.Plan ya Kanisa siyo kukaa,plani ya kanisa ni watu wanapokea mafundisho,wakikomaa wanaenda kuanzisha huduma,kanisa linakuwa duniani kote na siyo kanisa linakuwa kubwa hakuna ukuaji duniani.Hii maana yake kiongozi hawafundishi watu kwamba wanatakiwa kwenda kueneza injili,hajawaandaa kihuduma ,kwa hali hiyo ndiyo yatakuwepo hayo ya hakuna mwingine ispokuwa yeye.Hii si kibiblia.

Ukiona huduma fulani huyo mtu asipokuwepo huduma itakufa au haitakuwepo hapo kuna kitu hakiko sawa.
 
Anhaa nilifikiri labda maombi yake yalipandikiza kitu kibaya. Mungu anaona nia yako ya ndani kabisa, mfungulie mlango Yesu, Biblia inasema Ufunuo wa Yohana 3:20-22 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

20 Tazama, nasimama mlangoni napiga hodi. Mtu ye yote akisikia sauti yangu na kufun gua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami. 21 Atakayeshinda nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi.

So ni wewe kufungua moyo wako tu
Yesu anakusubiri uamue.Good lucky and God bless .



na
Hapana, ni miaka mingi imepita ila mimi si yule niliyekuwa kabisa mambo yangu mema hayako tena toka alivyoniombea I'm not a good person kabisa natamani kutoka niliko nashindwa
 
Back
Top Bottom