Je, Mwamposa yule "mtume" muasisi wa kukanyaga mafuta ya upako ni dhehebu gani? Je ni Calvary Assemblies of God ya Prophet Maboya?

.Watumishi wa leo hamtaki kujua watu wanasema ninyi ni akina nani.
Watumishi wa Mungu wa leo wako vizuri wanamsikiliza Mungu zaidi aliyewaita kuliko watu nyie wasikiliza watu bakini na watu wenu.SABABU MUMEITWA NA WATU SIO MUNGU
 
Mtumishi hivi unajisikiliza unavyoongea ? Hivi unajua hakuna anachofanya mwamposa unaweza kusema ni revelation ila kila kitu kipo kwenye bibilia ? soma kumbukumbu la torati 33;24, uone.unauhakika na hao unaosema wanapingana na MABOYA hawajawai kutumia mafuta wala maji ? arafu acha kuifanya biblia ifeet kwenye mtazamo wako soma biblia arafu umpe ROHO MTAKATIFU nafasi akufundishe.mtumishi kuwa na jibu la mtu saa hiyo hyo inawezekana kabisa ndio maana tunaroho mtakatifu anayetukumbusha mambo yote na ndio maana tuna roho ya unabiii na huduma ya kinabihii hii ni moja wapo katika zile huduma tano.jifunze kama kitu hukipendi sio laazma ukipinge unanyamaza kimya au unaelekeza kwa njia iliyosawa sawa sawa na neno la MUNGU linavoelekeza sio unavotaka wewe
1.Nini kimekufanya uniite mtumishi?Je mimi naonekana kama ni mtumishi?
2.Hivi nimeyataja hayo majina au wewe sasa umeyaweka?Huwa sina tabia ya kutaja majina ya watu unnecessary.
Nisaidie nini tofauti ya mafunuo na mafundisho?
Tirati 33:24 issue ya mafuta kama mafuta sitaki kujibu kitoto,nataka nikiileta mada hapa nimalize kabisa.Ila swali kwako katika bilia yalikuwepo mafuta ya kukandia unga wa ngano,mengine walipaka maiti kabla ya kuzika,mengine walimiminiwa wafalme na watumishi wa Mungu kama ishara ya kutengwa na kupewa ulinzi na Mungu,na kama ni msomaji kuna viungo vilitumika kutengeneza hayo mafuta.
Na kuna mafuta ambayo hawakuruhusiwa kujipaka katika miili yao,kuna mafuta yalitumika kupaka vitu/vyombo ya hekaluni,kwa hiyo kulikuwa na mafuta ya aina nyingi.Je haya yenu ni yapi kati ya yale mengi?Ulishawahi kujua yametengenezwa kwa vitu gani,je ni vile viungo vilivyonenwa kweny biblia au labda ni ya alzeti ila yameombewa?
 
Asa
Aulizwe mwenyewe sijawahi kanyaga kanisani kwake hata sijui huwa wanasalije mimi namjua Mwamposya na kuwa ASKOFU WAKE ni MTUME MABOYA

Kwa Mwamposya nakanyaga mafuta kama kawaida na maji ya upako kama kawaida
Asante! Hofu yangu ni kuwa Mwamposya hakubaliki na wengi miongoni mwa wapentekoste lakini Maboya anakubalika zaidi. Hili linaweza kutia ukakasi mkubaliko wa Maboya kwenye waamini wa kipentekoste hapa Tanzania.
Napenda unaongea kikomavu,kuhusu kuikubali huduma ya kukanyaga mafuta
anaikubali ndio maana anamruhusu mwanae aifanye,kwa sababu haiko kinyume na bibilia kasome kumbukumbu la torati 33 yote utaona watu walikuwa wakikanyaga mafuta,yy kutoiifanya ni kwa sababu sasa hivi amebase kwenye mafundisho tu,nadhan unaelewa kwamba wote tunaweza kuwa wachungaji ila tumeitiwa kundi tofauti la kondooo na kila kondoo wananamna yao ya kuchungwa
Kumbukumbu la torati sura ya 33 haizungumzii kukanyaga mafuta Bali kuchovya mguu katika mafuta. Kuchovya siyo kukanyaga!
 
Samahani Huwa sipokei huduma kutoka kwa nabii mgeni nisiyemjua
Pole ndugu,wewe unadhani kila mtu ni nabii?Je maandiko yanasemaje?Wapokeeni wageni ,watu msiowajua kwani kwa kufanya hivyo mnaweza kuwapokea malaika.Wewe unajuaje kama je ni mpango wa Mungu niongee na wewe upone,huoni kwa kukataa kwako unaweza ukawa unakataa kile ambacho Mungu anataka aseme na wewe kupitia mimi?
Fikiria kwa makini,si unajua muda mwingine Mungu hutumia watu kusema na watu.au unadhani hao viongozi wako ni malaika?Kawaulize kama Mungu hajawahi kutuma watu wawaambie jambo fulani muda mwingine watu wasiowajua.
Mimi nimetumia maandiko kusema na wewe,je nimekosea?Ningekuja na maneno tupu ingekuwaje?
Hujui kama kuna watu walikuwa watumishi wa Mungu dunini nsa wako kuzimu?Unadhani Yesu aliposema "Ondokeni kwangu enyi wanafiki siwajui,wakamwambia tulitoa pepo na kuombea wagonjwa kwa jina lako" unadhani hawa walikuwa washirika wa kawaida?
Unadhani kuwa mtumishi wa Mungu ni ticketi ya kwenda mbinguni?Hujui lile andiko ambalo hata kiongozi wako amelisema
" tafuteni kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao bilu huo hakuna awezaye kumwona Mungu".Ticketi ya kuingi mbinguni kama ulikuwa hujui ni utakatifu na siyo uongozi kanisani au vyeo.Kwa hudum watu watavishwa taji kwa kazi walizozifanya zikiisha kupimwa kwa moto.
Sikulazimishi ukitaka njoo ukitaka acha,Neno la Mungu lina uhai litaendelea kusema na wewe trust me,litasema na wewe siku zote za maisha yako.Kwa sababu sijaongea maneno yangu bali maneno ya Mungu.
 
Watumishi wa Mungu wa leo wako vizuri wanamsikiliza Mungu zaidi aliyewaita kuliko watu nyie wasikiliza watu bakini na watu wenu.SABABU MUMEITWA NA WATU SIO MUNGU
Kwa hiyo Yesu alikosea aliposema huwezi kusema unampenda Mugu usiyemwona wakati unamchukia jirani yako(mtu) ?
Wewe karoho ka kutwist mambo kameanza,sijasema usimsikilize Mungu lakini nilichomanisha watu pia wananafasi.Unataka kuniambia watu wakisema mchungaji wenu ni mwizi mtaignore completely?Nikuulize hujawahi kusikia watumishi wa Mungu wameanguka?Watu unaoishi nao wewe wanakujua kuliko hao washirika wenzako mnaokutana jumapili na katikati ya wiki,mtu aliyesafi kwa Mungu hata watu wanaomzunguka watamkubali.Au hukusoma maandiko ya kwamba " wakati Yesu anakua alimpendeza Munga pamoja na wanadamu?

Watoto wachanga mnasumbua sana muda mwingine ila biblia inasema tuwavumilie,siku moja mtakuwa.
 
1.Nini kimekufanya uniite mtumishi?Je mimi naonekana kama ni mtumishi?
2.Hivi nimeyataja hayo majina au wewe sasa umeyaweka?Huwa sina tabia ya kutaja majina ya watu unnecessary.
Nisaidie nini tofauti ya mafunuo na mafundisho?
Tirati 33:24 issue ya mafuta kama mafuta sitaki kujibu kitoto,nataka nikiileta mada hapa nimalize kabisa.Ila swali kwako katika bilia yalikuwepo mafuta ya kukandia unga wa ngano,mengine walipaka maiti kabla ya kuzika,mengine walimiminiwa wafalme na watumishi wa Mungu kama ishara ya kutengwa na kupewa ulinzi na Mungu,na kama ni msomaji kuna viungo vilitumika kutengeneza hayo mafuta.
Na kuna mafuta ambayo hawakuruhusiwa kujipaka katika miili yao,kuna mafuta yalitumika kupaka vitu/vyombo ya hekaluni,kwa hiyo kulikuwa na mafuta ya aina nyingi.Je haya yenu ni yapi kati ya yale mengi?Ulishawahi kujua yametengenezwa kwa vitu gani,je ni vile viungo vilivyonenwa kweny biblia au labda ni ya alzeti ila yameombewa?
Sasa brother kama hujui ni mafuta ghani yanatumika pale why unacooment negative ? yan unacomment kwa hasira kwa kitu usichokijua ? why unawahukumu watu hujui hata wanafanyaje huduma ? mafunuo ni jambo ambalo MUNGU anweza kukupa kwa kipindi fulani au kwa ajili ya watu fulani.ila mafundisho basic truth inayosimama kwa ajili ya muda wote
 
Asa
Asante! Hofu yangu ni kuwa Mwamposya hakubaliki na wengi miongoni mwa wapentekoste lakini Maboya anakubalika zaidi. Hili linaweza kutia ukakasi mkubaliko wa Maboya kwenye waamini wa kipentekoste hapa Tanzania.
Kumbukumbu la torati sura ya 33 haizungumzii kukanyaga mafuta Bali kuchovya mguu katika mafuta. Kuchovya siyo kukanyaga!
Hivi brother unaweza kuchovya bila kukanyaga ? au unabisha tu kwa sababu hupendi ?
 
Asa
Asante! Hofu yangu ni kuwa Mwamposya hakubaliki na wengi miongoni mwa wapentekoste lakini Maboya anakubalika zaidi. Hili linaweza kutia ukakasi mkubaliko wa Maboya kwenye waamini wa kipentekoste hapa Tanzania.
Kumbukumbu la torati sura ya 33 haizungumzii kukanyaga mafuta Bali kuchovya mguu katika mafuta. Kuchovya siyo kukanyaga!
Na bibilia ya kiingereza pale inatumia neno deep
 
Kanisa lake Ni part ya CAG,lakini hiyo huduma ya kukanyaga mafuta ameianzisha bila kufwata protocol za CAG,niliona kwenye mtandao mmoja waumini wa CAG wakisema makanisa yao hayana hiyo huduma mwamposa kajibunia from no where.
Ha ha ha kweli mkuu, Mwamposa amekuwa maarufu kuliko bosi wake. Sijui mnyakyusa wa wapi huyu?! Watumishi wanyakyusa wengi ni wanyenyekevu na hawana tabia za kitapeli kama Mwamposya. Mfano mzuri Mwakasege, Kameta, Bukuku, Mwakipesile wa EAGT, Mwakisyala n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu dadavua hujielewi hali imekuwa worse zaidi ya kabla ya maombi or??

Maboya amewahi kuniombea huyu aisee toka aniombee sijawahi kujielewa nimekuwa wa tofauti i am trying so much to find myself 😭😭

Ni miaka mingi sana imepita
 
Ndio ni mwanawe MTUME MABOYA kwa kiroho .Alikuwa muumini wake tu wa kawaida pale Arusha kanisani kwake akamfundisha ,kumlea hadi akaenda fungua kanisa la Calvary Assemblies Of God pale Moshi ambako vifo vimetokea, baadaye akafungua huduma ingine Dar es salaam ambayo iko pale Kawe nayo iko Chini ya CAG la Maboya. Na ASKOFU NA MTUME MABOYA ndie ASKOFU WAKE MK
Oook kumbe ndiko alikoanzia huduma so master wake akahitaji kafara za palepale, now it make sense🤔
 
Ndio ni mwanawe MTUME MABOYA kwa kiroho .Alikuwa muumini wake tu wa kawaida pale Arusha kanisani kwake akamfundisha ,kumlea hadi akaenda fungua kanisa la Calvary Assemblies Of God pale Moshi ambako vifo vimetokea, baadaye akafungua huduma ingine Dar es salaam ambayo iko pale Kawe nayo iko Chini ya CAG la Maboya. Na ASKOFU NA MTUME MABOYA ndie ASKOFU WAKE MKUU

Mtume Mwamposya huwa anahudumia makanisa mawili kwa Mpigo huwa yuko Dar es salaam na Moshi .Huweza kuhudumu kote kwa kutumia ndege za abiria.Akimaliza huku anapanda ndege anaenda kwingine kuhudumia.

Hizi ndege mara ingine zinamchelewesha huduma yake.Tunamwomba Mungu AMPE ndege yake binafsi ambayo atakuwa nauwezo wa kuondoka muda wowote atakao na kwenda kuhudumu popote sababu anahitajika mikoa yote Tanzania lakini sababu hana ndege yake binafsi mfano ya kuendesha ibada ya asubuhi labda Mwanza na ibada ingine Dar kwa siku inakuwa vigumu

Tuko kwenye maombi Mungu ampe ndege ya aina ya Gulfstream ina mbio za kutosha kwa private jets.Tushirikiane kumwombea apate

BULLDOZER MWAMPOSYA HUYOOOO

View attachment 1350819
Mkuu unasali kwa mwamposa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 KOR. 12:5-6
Tena kuna huduma tofauti, na Bwana ni yeye yule. Kisha kuna tofauti wa kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote

Tofauti ziko kwenye huduma na namna ya kutenda kazi,Kutenda kazi kuko tofauti.Ni kama mkulima mwingine jembe la mkono,mwingine trekta ,mwingine plau ya ng`ombe,Wote wakulima.
👍
 
Tumeambiwa kwa uhakika kuwa dhehebu lake ni Calvary Assemblies of God yaani CAG chini ya Prophet Maboya!! na uzuri Maboya hajamkana!! Ni baba aliyejitosa kumsemea vizuri mwanawe wa kiroho hata katika hali ngumu. Wengine wangemtosa!
Hata watoto Wengine huwa hawana adabu kwa wazazi wao wa kiroho Wakati wamewatoa mbali.Hebu fikiria Nuhu mitoto yake aliiokoa isiangamie na gharika Wakati Wengine wote walikufa.

Mzee Nuhu wa watu kahangaika mwenyewe kujenga safina ili mitoto yake isiangamie kwa gharika.

Kweli mitoto yake Ile ikapona haikuangamia. Kuna Siku mzee wa watu akapata changamoto ya kiroho akalewa chakari akakaa uchi Toto moja bwege likaanza kumcheka baba Yake ona zee Hilo liko uchi.

Mtoto Hakuwa hata na shukrani na huruma kwa mzee wa watu jinsi alivyowaokoa .Mzee wa watu akamlaani yule mtoto wa Mwisho na akalaanika kweli.Yule mzee Nuhu alikuwa na huruma Sana ningekuwa mimi like Toto ningelifyeka na mapanga.Wale watoto Wengine waliomsitiri baba yao wakabarikiwa

Mitoto nayo mingine haina adabu kwa wazazi wao wa kiroho

Mtume Maboya Ni baba wa Kiroho Ana ukomavu mkubwa mno wa kihuduma.Angekuwa baba wa hivi hivi angemruka Mwamposya na kumwachia ahangaike mwenyewe.
 
Asa
Asante! Hofu yangu ni kuwa Mwamposya hakubaliki na wengi miongoni mwa wapentekoste lakini Maboya anakubalika zaidi. Hili linaweza kutia ukakasi mkubaliko wa Maboya kwenye waamini wa kipentekoste hapa Tanzania.
Kumbukumbu la torati sura ya 33 haizungumzii kukanyaga mafuta Bali kuchovya mguu katika mafuta. Kuchovya siyo kukanyaga!
Swala sio kukubalika na watu Wawe dini ya kipentecoste au yeyote .Swala Ni kukubalika na Mungu wao sio watu wa dini!!!

TB Joshua wa Nigeria hakukubaliwa na mpentecoste hata mmoja sababu wao walikuwa na vigezo vyao vya kujitungia kimoja mtu ili akubakiwe awe na baba wa kiroho.mpentecoste aliyemlea kiroho TB Joshua Hana,kingine awe kasoma vyuo.vya kipentecoste vinavyotambulika TB Joshua Hana ,kingine aonyeshe kanisa alipokuwa akisali kabla kuanza huduma TB Joshua akawa Hana wakasema hatukutambui wote.Akaeema sawa nyie Kama hamnitambui.basi hamkumniita ninyi.Kaniita Mungu akaanza kuchapa kazi Sasa hivi Duniani kote Hakuna mpentecoste Kama TB Joshua mwenye kanisa ambalo Lina watu wa rangi zote Duniani na ni mhubiri pekee ambaye viongozi wa dunia wengi wameshaenda kusali kwake ibadani Tanzania Akina Raisi Magufuli wakiwemo

Mtu aliyeitwa hahangaiki Sana kutambulika na watu .Na Yesu alikataa hayo mambo kwamba ufanyapo kitu usifanye ili uonekane mbele za watu wakukubali au la Angalia baba yako aliye mbinguni anakukibali?

Kwa hiyo Kama watu wa dini ya pentekoste hawaitambui sio.kesi waendelee na dini yao sisi tuendelee na Mwamposya wetu.

Sio kesi
 
Hata watoto Wengine huwa hawana adabu kwa wazazi wao wa kiroho Wakati wamewatoa mbali.Hebu fikiria Nuhu mitoto yake aliiokoa isiangamie na gharika Wakati Wengine wote walikufa.

Mzee Nuhu wa watu kahangaika mwenyewe kujenga safina ili mitoto yake isiangamie kwa gharika.

Kweli mitoto yake Ile ikapona haikuangamia. Kuna Siku mzee wa watu akapata changamoto ya kiroho akalewa chakari akakaa uchi Toto moja bwege likaanza kumcheka baba Yake ona zee Hilo liko uchi.

Mtoto Hakuwa hata na shukrani na huruma kwa mzee wa watu jinsi alivyowaokoa .Mzee wa watu akamlaani yule mtoto wa Mwisho na akalaanika kweli.Yule mzee Nuhu alikuwa na huruma Sana ningekuwa mimi like Toto ningelifyeka na mapanga.Wale watoto Wengine waliomsitiri baba yao wakabarikiwa

Mitoto nayo mingine haina adabu kwa wazazi wao wa kiroho

Mtume Maboya Ni baba wa Kiroho Ana ukomavu mkubwa mno wa kihuduma.Angekuwa baba wa hivi hivi angemruka Mwamposya na kumwachia ahangaike mwenyewe.
Mkuu nmeona sehem unasema ungemfyeka na mapanga kama Wewe ungekua Nuhu baba wa mtoto

Kwa kifupi ungeua, Najua Wewe ni mwanachama wa fisiem
Juzi kwenye kile chombo cha kutunga sheria nlimsikia mwehu mwenzenu akisema zk auwawe, je Ndiyo tabia zenu fisiem kuuwa watu??

Je Wewe ni mlokole huko unakosali Ndiyo mnafundishwa hivo??

Kwa kauli yako ina maana una support vifo vilivotokea moshi vilivo sababishwa na huyo mtume wako???

Nasubir majibu Tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom