Je, Mwalimu Nyerere alikuwa na uono hafifu katika hili au sisi wasomi ndio shida?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,570
15,310
Mwalimu alipopata mkopo anasema alijifikiria sana. Akiwapa masikini chakula watakula ila baadae watasikia njaa na kutaka waprwe tena.

Yeye na team take wakaamua badala yake wamsomeshe mtoto wa masikini akiisha soma akaelimika basi ataisaidia familia yake yote moja kwa moja.

Nguvu kubwa ikaingizwa katika Elimu kwa mtoto wa masikini.

Kinachoendelea leo kama matokeo ya mkakati huu.

1. Wasomi tunao wengi lakini ni masikini kuliko wazazi wao. Yaani wengi ombaomba, watu wa kujipendekeza na waliosoma sana wamekimbilia kwenyr siasa kula kwa Maneno badala ya kula kwa taaluma.

2. Walitegemea wasome kisha waajiliwe sasa hats Mkuu wa nchi kakili hajawatendea hali katika ajira.

3. Leo Machinga darasa la nne anaweza kulisha familia nzima huku msomi chuo kikuu hawezi hata kujinunulia boxer.

4. Maisha ya wasomi wengi yanategemea ajira za wasiosoma. Yaani hawana uwezo wa kutengenrza ajira

Najiuliza wakuu, nani hapa kakosea wasomi au Mwalimu Nyerere alikuwa na uono hafifu?
 
Elimu inayomjenga mtu ajiajiri ikoje Mkuu.
Maana hata hii sio yetu tumeitoa hukohuko ughaibuni nao wanasoma hayahaya.

Au nyerere aliona Elimu gani hiy o ya kuleta utajiri?
Elimu ambayo sio ya kukariritu vitabuni bali inayomfanya msomaji aishi kwa vitendo zaidi na nadharia kiasi. Mfano shuleni zamani tulisoma sayansikilimo kwa vitendo. Unakua na bustani yako na matokeo yake unapata ujuzi pia unazalisha mali.
 
Elimu inayomjenga mtu ajiajiri ikoje Mkuu.
Maana hata hii sio yetu tumeitoa hukohuko ughaibuni nao wanasoma hayahaya.

Au nyerere aliona Elimu gani hiy o ya kuleta utajiri?
Tulisoma sayansikimu na sayansikilimo,hapo ilikua nadharia na vitendo au hujapitia kipindi hicho mkuu
 
Mitaala mobovu, wasomi wamepoteza muda kukariri, enzi zile tulisomaga mavitu mengi yasiyo na tija
 
Nchi iliharibiwa na falsafa ya uchumi wa kijamaa,hata mitaala mashule iliendana na falsafa ya ujamaa ambayo hairuhusu fikra huru na kumjenga mtu kuwa kipato kikubwa, ili watu wasijekuwa mabepari wakaja wakamuondoa nyerere madarakani
 
Tulisoma sayansikimu na sayansikilimo,hapo ilikua nadharia na vitendo au hujapitia kipindi hicho mkuu
Yap nakumbuka japo sio wa kale sana. Makini Azimio primary Musoma mjini nikiwa darasa LA Tatu nilikuwa na Bustani ya mchicha chini ya Mwalimu wa hili somo.

Ikifika break ya SAA NNE wale ambao mchicha wao umekomaa wanaruhusiwa kwenda kuuza. Ukiuza sh 100 hiyo inarudi Shule tunakunywa uji, iliyobaki ni yako. Kila siku jioni tulienda Kumwagilia.

Mkuu huwezi amino huko darasa LA sita saba tano zilikuwa zinapigwa Bustani hatari na tulikuwa tunashindana na Shule Jirani.

Leo ninapoandika hapa naandaa Bustani ya mchicha na Majani ya kunde kwa ajili ya mama na watoto kula vitu OG baada ya mboga kwenda na Maji juzi ila nabunibuni tu maana baada ya kuhama Shule ile sikuwahi kukutana na projects kama zile zaidi ya kuambiwa niende na ufagio na kadumu ka Kumwagilia maua kitenge na saasita.
 
Hiyo ndio elimu chanya kwa wakati wote,sio elimu hii ya kitabunitu
 
Mwalimu alipopata mkopo anasema alijifikiria sana. Akiwapa masikini chakula watakula ila baadae watasikia njaa na kutaka waprwe tena.

Yeye na team take wakaamua badala yake wamsomeshe mtoto wa masikini akiisha soma akaelimika basi ataisaidia familia yake yote moja kwa moja.

Nguvu kubwa ikaingizwa katika Elimu kwa mtoto wa masikini.

Kinachoendelea leo kama matokeo ya mkakati huu.

1: Wasomi tunao wengi lakini ni masikini kuliko wazazi wao. Yaani wengi ombaomba, watu wa kujipendekeza na waliosoma sana wamekimbilia kwenyr siasa kula kwa Maneno badala ya kula kwa taaluma.

2: Walitegemea wasome kisha waajiliwe sasa hats Mkuu wa nchi kakili hajawatendea hali katika ajira.

3: Leo Machinga darasa la nne anaweza kulisha familia nzima huku msomi chuo kikuu hawezi hata kujinunulia boxer.

4: Maisha ya wasomi wengi yanategemea ajira za wasiosoma. Yaani hawana uwezo wa kutengenrza ajira

Najiuliza wakuu, nani hapa kakosea wasomi au Mwalimu Nyerere alikuwa na uono hafifu?
Shida ni mfumo wetu wa elimu ni mbovu sn
 
Elimu isiyomjenga raiya kujiajiri bado inachangamoto ndani yake
Tatizo ni wanasiasa mkuu. Wanasiasa wanatuamisha kuwa unasoma ili uajiliwe na kama hujaajiliwa wakati umesoma huna haja ya kufanya kazi zisizo za kuajiliwa, wewe endelea kusubilia ajila tu. Kwani umesoma ili uajiliwe. Hili ni tatizo kubwa.

Kiuharisia kusoma ni kuongeza uelewa. Na ukiongeza uelewa unaongeza pia namna ya kupambana na changamoto za maisha.
 
Mbovu wapi Mkuu na kiongezwe au kiondolewe nini ili utengemae.
Maana kama vyuo vikuu tunachosoma ndio wanasoma ulaya na US labda kama vitendea KAZI tu viwe hafifu.

Usa wanatuzidi kwenye elimu ya msingi na sekondari mpaka high school.. huko wanatoka fit kweli kweli...

Sekondari school ya us.. ina masomo kama creative writting, public speaking, drama , music, etc etc... wao mechanics wanajifunza toka shuleni
 
Wale wanasoma kwa vitendo zaidi na siyo theory kama sisi, mbona medicine watu wanaelewa zaidi? sababu ni moja wanafanya practical zaidi.
 
Usa wanatuzidi kwenye elimu ya msingi na sekondari mpaka high school.. huko wanatoka fit kweli kweli...

Sekondari school ya us.. ina masomo kama creative writting, public speaking, drama , music, etc etc... wao mechanics wanajifunza toka shuleni
Aisee hizo za chini ni ajira kabisa .
Kwa nini kusiwe na private school ambazo zitakuwa na contents zote muhimu kama model ya elimu sahihi.

Nimewahi kufundisha English medium moja nikashangaa sana. Mtoto kajiunza mambo kwa English, akasoma na preform one lkn akifika form one ambapo ni marudio hajui na bado anataka aingie na chabo.

Labda wakuu wetu wakajifunze Singapore kwa Lee kuan Yew. Ila cha ajabu viongozi wetu wanajua hats Dr Mipango mwanzoni alikuwa anamtajataja sana huyu Brilliant dictator aliyegeuza Elimu huu chini na mahr duniani kwenda Singapore kuchukua vichwa vya kuajiri.

Tunafeli wapi
 
Mbovu wapi Mkuu na kiongezwe au kiondolewe nini ili utengemae.
Maana kama vyuo vikuu tunachosoma ndio wanasoma ulaya na US labda kama vitendea KAZI tu viwe hafifu.
Mkuu,
Elimu inalengo la kumpatia mpatiwaji wake ujuzi ama utaalamu wa kufanya jambo fulani kulingana na ngazi mtu aliyohitimu. Mfano mhitimu wa darasa la saba anaweza kuwa na ujuzi wa kuandika, kusoma ama kuhesabu. Huo ni ujuzi kwa maana anayehitimu hujua vitu hivyo. Sidhani kama tunategemea mhitimu wa darasa la saba awe na utaalamu wa nyanja fulani.

Tukija kwenye mada wahitimu wa vyuo ambao umewahesabu kuwa wasomi hupatiwa elimu juu ya utaalamu fulani. Tunazalisha watu wa taaluma kadha wa kadha toka vyuoni. Mhitimu wa chuo anapaswa kuwa na vigezo anavyoweza kuwa navyo mtu wa taaluma fulani. Ikiwa ni muhitimu wa masomo ya utabibu aweze kutibu, mwalimu aweze kufundisha na bwana shamba awe hivyo pia.

Kujiajiri ni ujasiriamali, kwa miaka mingi ujasiriamali haukuwa ukifundishwa shuleni. sasa ivi entrepreneurship ni somo kwa karibu taaluma nyingi. Walimu watasoma namna yakuwa wajasiriamali, wahandisi kadhalika, wataalamu wa karibu kila nyanja hupatiwa elimu ya ujasiriamali. Ujasiriamali unaofundishwa ni kuhusu kada husika mfano kwa madaktari unaweza kukuta kitu kama entrepreneurial medicine.

Home | Muhimbili University of Health and Allied Sciences

Kama uonavyo Muhas wanavyotoa kwenye link hapo juu. Ukikuta aliyesomea udaktari anauza nyanya na ukasema kajiajiri basi ni wazi dhana nzima ya kujiajiri hatuijui. Tatizo ni kwamba ili ujiajiri kwenye fani nyingi za kitaaluma ni lazima upate proficiency na huwezi kuwa na ujuzi wa taaluma yoyote bila kuihudumu. Taaluma nyingi zinatoa muda kwa watu fresh from school kuhudumu ili wapate ujuzi wa taaluma husika. Wapo ambao huamini ujuzi unapatikana kwa kufanya mitihani ya bodi husika kama uhasibu na uwakili ama wale ambao hutakiwa kupata ujuzi kutokana na kufanya kazi kwa kipindi cha miaka fulani mfano kwa mthamini ili uonekane una ujuzi inakupasa uhudumu chini ya mthamini aliyesajiliwa kwa kipindi kisicho pungua miaka mitatu.

Taaluma haina ujanja wa kisiasa wa kuambia watu wajiajiri wakati hujui watajiajiri vipi. Hakuna hata jambo moja lakuondoa kwenye elimu yetu na kuna watu husema sana kuwa elimu yetu ni ya nadharia zaidi mara haimuandai mtu kujiajiri na watu wengi wanaposema hayo hutaja kuwa wao walisoma sayansi kimu na kujua kulima mchicha au kufuga kuku. Ujuzi ambao hata ambae hana elimu anauwezo wa kuupata.

Hatuna mifumo mizuri ya mafunzo baada ya kupata taaluma. Usifikiri muhitimu wa uhandisi wa ulaya hujua yote anayoyajua kutokana na kukaa darasani. wengi hupata fursa ya summer internships na ni mandatory kwa baadhi ya makampuni makubwa na hata madogo. Wanatambua juu ya ulazima wa kuwekeza ujuzi kwenye wataalamu.

Ubaya ni kwamba hapa kwetu hakuna mwongozo wa wahitimu kupewa uwezo wa kuhudumu taaluma zao alafu tunalaumu watu hawana ujuzi mara hawawezi kujiajiri.
 
Mkuu,
Elimu inalengo la kumpatia mpatiwaji wake ujuzi ama utaalamu wa kufanya jambo fulani kulingana na ngazi mtu aliyohitimu. Mfano muhitimu wa darasa la saba anaweza kuwa na ujuzi wa kuandika, kusoma ama kuhesabu. Huo ni ujuzi kwa maana anayehitimu hujua vitu hivyo. Sidhani kama tunategemea mhitimu wa darasa la saba awe na utaalamu wa nyanja fulani.

Tukija kwenye mada wahitimu wa vyuo ambao umewahesabu kuwa wasomi hupatiwa elimu juu ya utaalamu fulani. Tunazalisha watu wa taaluma kadha wa kadha toka vyuoni. Mhitimu wa chuo anapaswa kuwa na vigezo anavyoweza kuwa navyo mtu wa taaluma fulani. Ikiwa ni muhitimu wa masomo ya utabibu aweze kutibu, mwalimu aweze kufundisha na bwana shamba awe hivyo pia.

Kujiajiri ni ujasiriamali, kwa miaka mingi ujasiriamali haukuwa ukifundishwa shuleni. sasa ivi entrepreneurship ni somo kwa karibu taaluma nyingi. Walimu watasoma namna yakuwa wajasiriamali, wahandisi kadhalika, wataalamu wa karibu kila nyanja hupatiwa elimu ya ujasiriamali. Ujasiriamali unaofundishwa ni kuhusu kada husika mfano kwa madaktari unaweza kukuta kitu kama entrepreneurial medicine.

Home | Muhimbili University of Health and Allied Sciences

Kama uonavyo Muhas wanavyotoa kwenye link hapo juu. Ukikuta aliyesomea udaktari anauza nyanya na ukasema kajiajiri basi ni wazi dhana nzima ya kujiajiri hatuijui. Tatizo ni kwamba ili ujiajiri kwenye fani nyingi za kitaaluma ni lazima upate proficiency na huwezi kuwa na ujuzi wa taaluma yoyote bila kuihudumu. Taaluma nyingi zinatoa muda kwa watu fresh from school kuhudumu ili wapate ujuzi wa taaluma husika. Wapo ambao huamini ujuzi unapatikana kwa kufanya mitihani ya bodi husika kama uhasibu na uwakili ama wale ambao hutakiwa kupata ujuzi kutokana na kufanya kazi kwa kipindi cha miaka fulani mfano kwa mthamini ili uonekane una ujuzi inakupasa uhudumu chini ya mthamini aliyesajiliwa kwa kipindi kisicho pungua miaka mitatu.

Taaluma haina ujanja wa kisiasa wa kuambia watu wajiajiri wakati hujui watajiajiri vipi. Hakuna hata jambo moja lakuondoa kwenye elimu yetu na kuna watu husema sana kuwa elimu yetu ni ya nadharia zaidi mara haimuandai mtu kujiajiri na watu wengi wanaposema hayo hutaja kuwa wao walisoma sayansi kimu na kujua kulima mchicha au kufuga kuku. Ujuzi ambao hata ambae hana elimu anauwezo wa kuupata.

Hatuna mifumo mizuri ya mafunzo baada ya kupata taaluma. Usifikiri muhitimu wa uhandisi wa ulaya hujua yote anayoyajua kutokana na kukaa darasani. wengi hupata fursa ya summer internships na ni mandatory kwa baadhi ya makampuni makubwa na hata madogo. Wanatambua juu ya ulazima wa kuwekeza ujuzi kwenye wataalamu.
Mkuu umeandika vitu vingi vikubwa hata vingine sijawahi kuvifikiri kwa mpangilio hivi.
Nitasoma tena na kutoa chsngamoto
 
Mwalimu alipopata mkopo anasema alijifikiria sana. Akiwapa masikini chakula watakula ila baadae watasikia njaa na kutaka waprwe tena.

Yeye na team take wakaamua badala yake wamsomeshe mtoto wa masikini akiisha soma akaelimika basi ataisaidia familia yake yote moja kwa moja.

Nguvu kubwa ikaingizwa katika Elimu kwa mtoto wa masikini.

Kinachoendelea leo kama matokeo ya mkakati huu.

1. Wasomi tunao wengi lakini ni masikini kuliko wazazi wao. Yaani wengi ombaomba, watu wa kujipendekeza na waliosoma sana wamekimbilia kwenyr siasa kula kwa Maneno badala ya kula kwa taaluma.

2. Walitegemea wasome kisha waajiliwe sasa hats Mkuu wa nchi kakili hajawatendea hali katika ajira.

3. Leo Machinga darasa la nne anaweza kulisha familia nzima huku msomi chuo kikuu hawezi hata kujinunulia boxer.

4. Maisha ya wasomi wengi yanategemea ajira za wasiosoma. Yaani hawana uwezo wa kutengenrza ajira

Najiuliza wakuu, nani hapa kakosea wasomi au Mwalimu Nyerere alikuwa na uono hafifu?

THE POWER OF FAITH, UKIAMINI KUWA UNAWEZA UPO SAHIHI, NA UKIAMINI KUWA HAUWEZI UPO SAHIHI............WALIOMFUNDISHA MWAMFUNZA KUAJIRIWA NA KUTUMIKIA WATU NA SIO KUAJIRI WATU UNADHANI ITAKUWAJE SASA?
 
Elimu inayomjenga mtu ajiajiri ikoje Mkuu.
Maana hata hii sio yetu tumeitoa hukohuko ughaibuni nao wanasoma hayahaya.

Au nyerere aliona Elimu gani hiy o ya kuleta utajiri?
Ukitegemea kuajiriwa imekula kwako ,ni nchi gani ya afrika iwe South mpaka North imeajiri nusu ya wananchi wake.Tanzania sisi ni nani tunalaumu serikali yetu inayokusanya 1.5t ambayo ukiwa na wafanyakaz wa umma 2m maana yake maendeleo yatasimama na gharama itakuwa ni mishahara tu .Hatujafikia hako acha tuijenge nchi kwa miundo mbinu ya kiuchumi na baadae mambo yatajiseti kama Mtu kamaliza Masters ya Mine Engeniaring na kakosa hata kwenye Private Company uilaumu serikali kuna vijikampuni vingi tu wasomi mnaweza pata kazi shida kila mmja anataka serikali kwa sababu ajira ya kudumu na Pssf mzigo unakuwaga umetuna kuliko hata wa Private sector kazi zipo nyingi sana hamzitaki kuna DJ yupo kenya ni doctor ila yupo DISCo anatafuta ugali wa familia .
 
Back
Top Bottom