Je, Mwalimu au Mtumishi yeyote wa Serikali anahitaji ruhusa ya Mwajiri kusafiri nje ya nchi akiwa likizo?

Varbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,117
856
Juzi nilikua Airport kumsindikiza Mshkaji wangu aliyekuwa akielekea Nairobi baada ya kuja kunitembelea.

Baadae nikamuona dada mmoja anavutia simjui na simfahamu kabisa, ilionesha anasafiri nje ya nchi. Kama kawaida kaingia ndani baadae namuona anatoka akiwa frustrated analia na ni kama hajielewi nikajisogeza kuuliza kulikoni dada au umekutwa na nyara za Magufuli?

Akasema hapana, wamenikatalia kusafiri kwa sababu mie mtumishi wa Serikali. Nikamuuliza unafanya ofisi gani? Akajibu Mwalimu wa shule ya msingim

Maafisa uhamiaji wanamwambia apeleke barua ya ruhusa na anavyodai yeye anakwenda kumsalimia ndugu yake Ulaya nchi hakutaja, ameghalimiwa kila kitu na huyo nduguye na visa anayo lakini hakuweza kuondoka

Wadau kuna haja gani kumzuia kusafiri mtu anakwenda kutembea na atarudi!? Kipindi cha likizo hiki? Kutoka nje ya nchi ni kosa gani kwenye Katiba yetu?

Siku ile nilichukia sana japo kuwa sikufanyiwa mimi..
 
Yaani kaacha kufundisha watoto wa masikini kaenda kusalimia ndugu ughaibuni!??
Utaratibu wa Ruhusu ya kusafiri nje ya kituo cha kazi upo wazi na wa kutoka nje ya nchi upo wazi ....sasa yeye kama alikuwa na kiburi na akaamua kukiuka acha yamkute.
 
Hii si likizo ? Wapo watu wanamtafutia Rais Ubaya tu . Nakwambia akili ya kawaida ingetosha kumruhusu sasa asafiri.....
 
Yaani kaacha kufundisha watoto wa masikini kaenda kusalimia ndugu ughaibuni!??
Utaratibu wa Ruhusu ya kusafiri nje ya kituo cha kazi upo wazi na wa kutoka nje ya nchi upo wazi ....sasa yeye kama alikuwa na kiburi na akaamua kukiuka acha yamkute.
upo sahihi kabisa ndugu. nchi yetu hii chini ya awamu ya 5 ni kama tupo jela vile!
 
Mlizoea kuishi kama mpo nightclub au casino ..sasa hivi mnafunzwa kuishi kama Mpo ndani ya kanisa au msikiti na hayo ndio maisha sahihi.
 
Saiz likizo awafundishe akina nani.Roho mbaya tu
Yaani kaacha kufundisha watoto wa masikini kaenda kusalimia ndugu ughaibuni!??
Utaratibu wa Ruhusu ya kusafiri nje ya kituo cha kazi upo wazi na wa kutoka nje ya nchi upo wazi ....sasa yeye kama alikuwa na kiburi na akaamua kukiuka acha yamkute.
 
Yaani kaacha kufundisha watoto wa masikini kaenda kusalimia ndugu ughaibuni!??
Utaratibu wa Ruhusu ya kusafiri nje ya kituo cha kazi upo wazi na wa kutoka nje ya nchi upo wazi ....sasa yeye kama alikuwa na kiburi na akaamua kukiuka acha yamkute.
Likizo unafundisha majengo au we we na jiwe ndugu moja
 
Saiz likizo awafundishe akina nani.Roho mbaya tu
Enzi zetu wakati wa likizo tunapumzika wiki moja tu halafu tunarudi kwa masomo ya ziada...zamu za kufanya usafi shule ,Kulima mashamba ya shule ,kushiriki michezo ya umitashumta au umiseta n.k
walimu walitakiwa kusimamia haya na pia walikuwa wakiandaa masomo ya mihula inayofuata.
Isitoshe walimu walikuwa wakiendelea na zoezi la kusahihisha mitihani na kutoa ripoti.
 
Sku hizi shule hazina mashamba
 
Sku hizi shule hazina mashamba
Ni uzembe na uvivu wa hali ya juu...Ndio maana mnakuja kufundishana elimu za ujasiliamali wa kulima mbogamboga kwenye mitandao ya kijamii.
Mtu unashindwa hata kuhudumia bustani yako nyumbani!!
 
Back
Top Bottom