Je, Mwalimu alihodhi maendeleo na kupeleka Butiama?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Mwalimu alihodhi maendeleo na kupeleka Butiama??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Oct 16, 2008.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Oct 16, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,806
  Likes Received: 5,115
  Trophy Points: 280
  ..nimestaajabu kusikia haya.

  ..je Butiama ilistahili maendeleo yote haya?

  ..tukihalalisha alichofanya Mwalimu kwa Butiama, tutaweza kuharamisha anachofanya Kikwete kwao Lugoba?


  ..hili hapa chini lina chembe-chembe za ukabila.

  ..ninavyoelewa Mwalimu siku zote alisisitiza Utaifa/U-Tanzania.

  ..je, katika faragha alitukuza ukabila/Uzanaki? hebu soma hapa chini??

  ..HABARI NZIMA INAPATIKANA TOKA GAZETI LA RAIA MWEMA. BONYEZA HAPA
   
  Last edited: Oct 16, 2008
 2. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii ni butiama ipi anayoongelea huyu?
   
 3. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Hata mimi nimebaki mdomo wazi?? Nimeshindwa kushangaa.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Oct 16, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,806
  Likes Received: 5,115
  Trophy Points: 280
  Magabe Kibiti,

  ..soma maneno ya Jackton Manyerere mzaliwa wa Butiama.

  ..anadai Butiama ilipata kuwa na benki 2, posta,simu,umeme,matrekta na malori yasiyo idadi, viwanda vya kushona nguo...etc etc.

  ..Je, Jackton Manyerere ni muongo?

  ..Je, wewe umefika Butiama. Je, Butiama haijapata kuwa na vitu vyote alivyodai Manyerere?

  ..mimi nimeleta hoja hii kama swali ili kupata ukweli zaidi? kuna uwezekano yote aliyoeleza Manyerere yalipatikana kutokana na nguvu za kujitolea za wananchi wa Butiama.
   
 5. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza lazima uwe na hakika kama alichosema Manyerere ni cha ukweli kabla ya kuuliza kama kilitokea kwa nguvu ya wananchi au la. By the way, swali la kwanza kwenye post yako ya kwanza uliuliza hili:

  tayari ulikuwa umeamini (au kuonekana kuamini) kuwa Mwalimu alifanya haya kwa Butiama na ukataka kuhalalisha au kuharimisha anayofanya Kikwete huko Lugoba.

  Weka msimamo na mtizamo wako wazi ili ueleweke.

  Kuhusu Manyerere kuzaliwa Butiama, ikizu, au Mugango sidhani kama hiyo tu inamfanya awe mtaalamu na msemaji wa kuaminiwa wa kila kilichofanyika na kisichofanyika huko.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,'
  Nakushauri mwenyewe utembelee Butiama ujionee. Sijui Jackton anazungumzia Butiama ipi. Maendeleo pekee niliyoona pale wakati wa mazishi ya Mwalimu yaliuwa kuwepo umeme na viosk vya Vodacom na Tritel. Na urithi pekee ambao Mwalimu aliwaachia nje tu ya Butiama(kuelekea Kiarano) ni bwawa kubwa la maji kwa sababu hawa walikuwa wakihangaika kutafuta maji siku nzima. Kama kuna benki na posta basi zimefunguliwa baada ya 2004( last time I visited) Na sina hakika kweli kama huyo mwandishi amekulia Butiama. Anaweza kuwa ana asili ya hapo lakini sidhani anaijua Butiama.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Oct 16, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,806
  Likes Received: 5,115
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  ..Manyerere anazungumzia Butiama "enzi za Mwalimu Nyerere."

  ..ukitulia na kusoma makala yake utaona anazungumzia in the past tense. kwamba Butiama ilipata kuwa na Benki 2, umeme,maji,posta, malori yasiyo na idadi, viwanda vya kushona nguo, etc etc?

  ..wewe unazungumzia mwaka 2004, labda walishindwa kuvi-maintain kama kawaida yetu wa-Tanzania.

  ..hii habari imetoka kwenye gazeti la Raia Mwema, na kuna anuani ya mwandishi humo ndani naomba mumuandikie kama mnapingana naye.

  Magabe Kibiti,

  ..habari hii imenishtua kidogo. imenipa picha tofauti kabisa na Butiama iliyokuwa mawazoni mwangu kwa miaka mingi--tena mimi ni mtu mzima.

  ..inawezekana kabisa nimekurupuka katika posting yangu ya kwanza, lakini naomba ukweli wa suala hili.
   
 8. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli umekurupuka mzee, bila kujali feelings zako dhidi ya Mwalimu, next time chukua muda kufuatilia ukweli wa anti-mwalimu posts kabla ya kuzipa alama ya juu ya ukweli kama ulivyofanya hapa.

  Mimi nimezaliwa Tarime (few miles toka butiama) lakini nimetembelea sana butiama wakati nikiwa high school (nimesoma Mara boys) kwa sababu one of my friends alikuwa anatoka huko. Pia, most of my primary school mates wamesoma Ikizu sec so meeting place yetu ilikuwa butiama kwa mwl wakati tukikimbia shule once in a while (tafadhali usiniseme kwa mzee magesa - headmaster).

  Haya anayoyasema Manyerere sijui ameyatoa wapi ndio maana nikauliza kama anaongelea the same butiama ninayoijua mimi au nyingine.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Oct 16, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,806
  Likes Received: 5,115
  Trophy Points: 280
  Magabe Kibiti,

  ..Butiama unayoizungumzia wewe ni ya miaka ipi?

  ..pia wewe uliona nini tofauti na hicho anachoelezea Manyerere?

  ..unajua hapa kuna kauli za Manyerere anayedai ni mwenyeji wa Butiama vs. wewe mtoto mtoro wa shule uliyekuwa ukijificha Butiama.
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Nakupata vizuri sana. Nimerudia kuisoma tena ile makala. Ninachofahamu mimi ni kwamba jitihada nyingi za maendeleo Butiama zilifanywa na marehemu Joseph Nyerere. Hata katika mazishi yake Mwalimu alikiri kuwa hajaifanyia Butiama kitu na hizi shule na hospitali mnazoziona alizianzisha Joseph. Sasa kuwa na posta sioni noma na wewe unaweza kuelewa usumbufu kwa Mwalimu kwenda Musoma mjini kupata barua zake. Pia ukiisoma makala utaona kuwa maendeleo yote hayo anayoyataja Jackton yalianza kufifia baada ya kifo cha Joseph Nyerere. Hata hivyo haiwiani kabisa na heading ya topic kuwa Mwalimu alihodhi maendeleo--inaashiria kuwa alitumia fedha ambazo labda zilikuwa zitumike Bariadi au Mugango na kuzipeleka Butiama. Bado nakupa changamoto ukipata muda utembelee Butiama ukajionee mwenyewe. Na kuhusu Butiama kuwa mji Mwalimu hakukubaliana na wazo hilo kwa sababu Butiama hakuna ardhi ya kutosha na kama Butiama itaamuliwa kuwa mji basi watahitaji eneo la kujenga makao makuu na miundombinu yote inayoendana na mji wa kisasa. After all Butiama is only 26 miles away from Musoma mjini do they really need another city especially now that the road is good and you can be in Musoma in 45 minutes?
   
 11. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninaongelea Butiama ya miaka ya 90 ambayo sio tu haikuwa na vyote hivyo anavyosema Manyerere, haikuwa na magofu ya hivyo vyote anavyosema.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Oct 16, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,806
  Likes Received: 5,115
  Trophy Points: 280
  Magabe Kibiti,

  ..wakati ukitoroka shule na kujificha Butiama ulipata kuona magofu ya kituo kilichojengwa na wa-Cuba?

  ..zaidi, uliona magofu ya kitu gani haswa? huelezi uliona nini huko Butiama tofauti na anachosema Manyerere.
   
 13. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nduguzanguni,

  Aliyoyaandika Manyerere ni ya ukweli. Kama alivyoeleza Jasusi, maendeleo yote yaliyoelezwa na Manyerere yalitokana na juhudi binafsi za Marehemu Mzee Joseph Nyerere akiwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Ujamaa cha Butiama. Kumbukeni pia kwamba juhudi binafsi ya Mzee Joseph Nyerere akiwa kiongozi wa Vijana wa TANU ndizo zilizojenga jengo la Vijana Kinondoni. Mzee huyu alikuwa ni Mzalendo nambari one na mtu wa kuchakarika vilivyo kwa manufaa ya kijiji na taifa kwa ujumla. Alikuwa anatumia contacts zake na marafiki zake wa nje na ndani ya nchi kuendeleza miradi hiyo yote.

  Pia tukumbuke kwamba si kijiji cha ujamaa cha Butiama ambacho kiliweza kupata maendeleo wakati huo. Nakumbuka baada ya Mwalimu kustaafu Mama Maria alialikwa kwenda kutembelea baadhi ya vijiji vya Ujamaa vya Mkoa wa Iringa ambako nako kulikuwa pia na maendeleo ya aina yake. Katika kijiji kimoja kinachoitwa Nzihi kulikuwa na maendeleo ya kujivuniwa. Wanakijiji walikuwa wakitengeneza mafuta yao wenyewe ya kupikia, wakisindika sukari guru na sukari mchanga, walitengeneza sabuni, walijijengea nyumba za kisasa za bati n.k. Yalikuwa ni maendeleo makubwa. Vilikuwepo vijiji vingine vya aina hiyo nchini mwetu.

  Sijui kama hivi sasa ukienda kwenye vijiji hivyo utakuta muendelezo wa maendeleo hayo yaliyokuwepo wakati huo. Hali hiyo ndiyo iliyotokea hata Butiama. Uongozi wa kijiji ulipobadilika, walioshika madaraka walihakikisha wanaiba na kufuja mali za kijiji. Magofu yapo Butiama. Jengo lililokuwa karakana liliachwa bila uangalizi wowote nadhani hatimaye liligeuka kuwa gofu. Halikadhalika jengo kubwa na zuri wakati huo likiitwa Jengo la Maendeleo lililokuwa na ukumbi mkubwa wa mikutano nalo liliachwa kuwa gofu. Inasemekana ndipo ulipofanyikia mkutano wa NEC baada ya Mheshimiwa Mkono kujitolea kuufanyia ukarabati.

  Mwalimu hakujiingiza kwenye shughuli za maendeleo ya kijiji cha Butiama alitoa mchango wake kama mwanakijiji lakini masterminder wa shughuli zote za maendeleo kijijini hapo alikuwa ni Mwenyekiti wa Kijiji Mzee Joseph Nyerere.
   
 14. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilichosema ni hiki:

  Kwamba,

  hakukuwa na magofu ya viwanda vya nguo, benki mbili, matrekta na malori yasiyo idadi, nk nk
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Oct 16, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,806
  Likes Received: 5,115
  Trophy Points: 280
  Bibi Ntilie,

  ..wewe umefika Butiama, au hayo uliyoyasema ni hadithi tu za vijiweni?

  ..Jasusi anadai alikuwa huko mwaka 2004, hakuona kitu.

  ..Magabe naye wakati akiwa shuleni alikuwa akitorokea Butiama, na hajawahi kuona hata magofu ya karakana zinazozungumziwa hapa.

  ..mimi ambaye sijafika Butiama nimuamini nani kati yenu?
   
 16. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilidhani kuwa umeshaweka imani yako kwa kile alichosema Manyerere kwa vile ni mzaliwa wa Butiama?
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Namuaminia Bibi Ntilie. Kama nilivyosema, itakuwa worth your while siku moja ukipata likizo upite pale, angalau kwa siku moja tu. Kama alivyosema Bibi Ntilie by 2004 mengi yalikuwa yamebaki maghofu. Kumbuka kuwa Joseph alifariki 1987. Kumuuliza Bibi Ntilie kama amewahi kufika Butiama ni kama unamwuliza Pope if he is Catholic?
   
 18. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushauri mzuri sana huu Jasusi,

  Natumaini Jokakuu ataenda butiama na kushuhudia magofu ya viwanda vya nguo, benki 2, matrekta na malori yasiyo na idadi na kisha arudi kulinganisha hayo na kinachofanywa na Kikwete Lugoba leo hii.
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Oct 16, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,806
  Likes Received: 5,115
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  ..now, how about kati yako wewe na Bibi Ntilie? kwasababu to some extent she is agreeing with what Manyerere is saying about Butiama.

  Bibi Ntilie,

  ..asante kwa kutuhabarisha kuhusu mchango wa Joseph Nyerere.

  ..je, kati ya aliyoyaeleza Manyerere ni yapi ya kweli na yapi ya uongo?

  ..je, unaweza kutueleza mara ya kwanza kufika Butiama ilikuwa lini? vilevile umetembelea mara ngapi Butiama?

  ..Jasusi alikuwa huko 2004, na Magabe alikuwa huko in the 90s.

  Magabe Kibiti,

  ..wewe uliona magofu ya kitu gani huko Butiama?

  ..it is you against Manyerere na Bibi Ntilie.
   
 20. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Joka,

  Manyerere kaeleza mambo kadha wa kadha kwenye makala yake likiwemo ya jinsi maendeleo ya kijiji cha Butiama yalivyofifia kutokana na sababu alizozitoa. Na makala yake imezungumzia kwa undani kwa nini anadhani kwamba si busara Butiama kuwa Wilaya etc. Au kwa hoja yako ya ukweli na uongo wa Manyerere unataka tuzungumzie suala la Butiama kuwa Wilaya? Wewe waonaje, kutokana na aliyoyaandika Manyerere unadhani ni busara kijiji hicho kubadilishwa sura?
   
Loading...