Je, Mwakyembe kujiuzulu Ubunge?!

Na kama BUNGE nalo halitasikiliza na kutekeleza OMBI hili la Mh. Mwakyembe na Kamati yake, SPIKA na BUNGE lililopitisha AZIMIO lile wanapaswa kuangalia kama wanastahili kuendelea KUWEPO. Vinginevyo WAMUWAJIBISHE WAZIRI MKUU mara moja.
 
Nafikiri Lowassa anapaswa kufahamu kuwa kuwarubuni baadhi ya wabunge hakutomsaidia kabisa make kuna watanzania wengi ambao hawako tayari kumuona anatakata kwati madudu yake yanajulikana.
 
Kwa kweli inauma sana kuonekana ni mmbea na mnafiki kwa jamii ndio maana Mwakyembe anajiandaa kwa makombora mengine kujilinda na kuangamiza pia..walichokua wanakitengeneza baadi ya mafisadi CCM ni kumfanya mwakyembe na kamati yake..hasa mwakyembe waonekane ni wanafki na wazushi na kwamba hao waliowataja katika ripoti yao wameonewa...vitu hivi hufanyika kwa kutoa vijembe vikali mno,kejeli, majungu na kutengeneza uongo kiasi kwamba kila mtu anayesikia huona ni ukweli kuwa wahusika wameonewa na mwishowe waliotoa ripoti waonekane ni watu wenye wivu, wanafiki, na wenye roho mbaya...

ikifika steji hiyo..na ndio ambayo ipo sasa ndani ya CCM basi lazima mambo mengi tusiyoyatarajia yatatokea..that means wanaoshutumiwa kuwa ni wanafiki watajitahidi wajisafishe kwa nguvu zote na waonekane walichosema ni cha ukweli ( na ni ukweli kua ni cha ukweli) na wanaoshutumiwa watajitahidi kwa nguvu zote wawateke watu wengi zaidi waamini kua kisemwacho ni cha uongo..kwa gharama yeyote ile...matokeo yake mpasuko utazidi kuwa mkubwa na wakushangaza.....( kumbuka hivi ni vita kati ya ufisadi na taifa) ambayo kwa sasa inageuka kwa individuals...

Ok alichokifanya/kisema mwakyembe ndio mwanzo wa hii story..........


'' This is the Beginning of the End''

Stay Tuned.
 
Na kama BUNGE nalo halitasikiliza na kutekeleza OMBI hili la Mh. Mwakyembe na Kamati yake, SPIKA na BUNGE lililopitisha AZIMIO lile wanapaswa kuangalia kama wanastahili kuendelea KUWEPO. Vinginevyo WAMUWAJIBISHE WAZIRI MKUU mara moja.

umepatia kwa 100%
 
Mie nina wasiwasi pale Spika alipoona kwenye mlolongo wa wachangiaji anayefuatia ni Mwakyembe akona aondoke mapema kwakuwa ingembidi akubaliane na Mwakyembe kutengua kile kifungu ili mjadala wa Richmonduli ujalidiliwe upya na wale wote wenye dukuduku zao wamwage kwenye ulingo
Huo ndio wasiwasi wangu au mnalionaje hilo wajameni
 
Mi naomba wabunge wa upinzania na wakina mwakyembe wasikubali mpaka kieleweke. waziri mkuu aliahidi kutekeleza yale maazimio ya kamati ya bunge na akasema angetoa majibu katika kikao hichi sasa anachozunguka mmbuyu nini au na yeye ashamezwa na mafisadi???????
 
Safi sana Dr. Viongozi wa nchi wanafanya mambo machafu sana, hawadhamini rasilimali za taifa wala taaluma waliyonayo wananchi wake. Iweje viongozi wanaunda tume ambazo zinatumia rasilimali haba za taifa hili pamoja na jasho la walipa kodi halafu wanaishia kukebehi ripoti hizo?. BWM aliunda tume ya Warioba kuangalia rushwa ripoti ikaishia kudhihakiwa na kufanyiwa mzaha na BWM mwenyewe, Bunge limeunda tume ya Mwakyembe kuchunguza Richmond Bunge hilo hilo linaishia kudhihaki mapendekezo ya tume na maazimio ambayo yalifikiwa na Bunge lenyewe, JK na tume ya Bomani kupitia mikataba ya madini taarifa na mapendekezo ya tume yanaishia kwa akina Sinclair - what's the habit is this?, why are our leaders making jokes with our country!, should people start throwing stones to them?. Dr Slaa, Zitto and others please back this man to ensure things are going in right direction, we are with you.
 
Na kama BUNGE nalo halitasikiliza na kutekeleza OMBI hili la Mh. Mwakyembe na Kamati yake, SPIKA na BUNGE lililopitisha AZIMIO lile wanapaswa kuangalia kama wanastahili kuendelea KUWEPO. Vinginevyo WAMUWAJIBISHE WAZIRI MKUU mara moja.

...'makombora' yaanze kurushwa kwa huyu mh. Pinda, Waziri Mkuu akiwa ni mkuu wa shughuli za serikali Bungeni! ...Mh Mwakyembe is right!

wallahi natanzika na serikali kuunda kamati ya kuchunguza kadhia fulani, wakati hizo kamati zikiwasilisha matokeo ya uchunguzi wa kamati kwa 'sirikali', inaundwa tena kamati kuipitia matokeo ya kamati ije itoe matokeo ya kamati baada ya miezi sita... ukizidisha kamati mara miezi sita ya kutoa majibu ya kamati unapata miaka mitano...

Usanii mtupu, hakuna majibu yanayotolewa.

ndio mwendo mdundo?!
 
Sasa mambo yanaanza kuiva. Nishasema huko vyuma kwamba legacy ya JK itakuwa uwazi. Ila huu uwazi siyo kuwa JK anataka bali unakuja kwa vile watu hawamuogopi. Kwa hiyo JK nafikiri abadilishe MOTTO from ANGUKA to UWAZI. Mpaka 2010 tutaona mengi. Wazee mliopo bongo tumwagieni mavitu!!!!!!!
 
Wakuu,
Hiki ndo ninachokitaka hasa, na siyo habari za kupeleka jeshi letu Zimbabwe. Bravo Mwakyembe!

MUNGU MUBARIKI MWAKYEMBE. UMWEPUSHE NA UOVU WA DUNIA HII NA ASIDHURIWE NA MAFISADI WA CCM.
 
Spika Anazibeba Dhambi La Kuyumba Kwa Kanuni Za Bunge Toka Pale Ilipoundwa Kamati Ya Mwakyembe,utendaji Wa Kamati,taarifa, Mapendekezo Na Hatimaye Resolution Ya Bunge Na Kile Kilichotokea April Pale Ndg.rostam Alipozimwa.

Anabeba Lawama Ingine Aliporidhia Wabunge Wake Wakutane Na Chama Chao Mapema June Na Mbaya Zaidi Chama Na Bunge Vilipojikita Ktk Agenda Hizi Za Richmon+epa Licha Ya Kuwa Tayari Zilishakuwa Mikononi Mwa Taasisi Zenye Mamlaka Ya Kikatiba Na Sheria Kwa Maagizo Ya Bunge Lenyewe Kwa Richmond Na Rais Kwa Lile La Epa.

Sidhani Kama Ndg Sitta Anatambua Namna Anavyovuruga Mwenendo Mzima Wa Kisayansi Ktk Utatuzi Ya Mambo Yote Haya!!

Mwakyembe Yuko Sahihi Kutetea Kanuni Za Bunge Ziheshimiwe, Lakini Huyu Ni Jasiri Maana Analishawishi Bunge Kufanya Kitu Ambacho Hawawezi Kukifanya Anapolitaka Lifute Azimio Lake Na Kurejewa Kwa Ripoti Ambayo Yeye Anasema Itajumuisha Yote Hata Yale Yaliyoachwa Kwa Kuinusuru Serikali! Hapo Ameanzisha Jambo Jipya, Anataka Tuamini Kuwa Kuna Mengi Hayajatamkwa Mle Ripotini Ila Kamati Imeyahifadhi, Na Sasa Wako Tayari Kuyaweka Hadharani!! Kuna Nini Anatufundisha Dkt.Mwakyembe , Richmond Iligusa Wake Kwa Waume Matumboni Mwao, Leo Unatuambia Hukueleza Yote ? Kwa Faida Ya Nani? Na Sasa Unashauri Mvunje Kanuni Zenu Rasmi Ili Uyatamke Hayo Yaliyomo Sirini Kwa Faida Ya Nani ?!! Mimi Niliamini Kuwa Ripoti Ilibeba Kila Kitu Na Kuwa Bunge Ni Sehemu Ya Wananchi Ambapo Hakuna Siri Wala Usalama Wa Nani, Maana Siye Ndiye Nchi,ndiyo Serikali Na Ndio Watanzania Wenyewe Hasa, Dkt Anajitofautishaje Na Muiran Rostam? Hoja Yako Ya Leo Imekaa Vizuri Sana Na Inaamsha Hamasa Ya Kizalendo Lakini Sisi Tunakudai Hizo Zilizomo Sirini Ili Tuamue Wenyewe Aidha Kunyoa Au Kusuka Kinyume Cha Hapo Mh.dkt. Mwakyembe Mwisho Wa Siku Utazidiwa Hoja Na Maadui Wa Haki.
 
Last edited:

MWAKYEMBE TUPE RAHA....WEWE NI JEMEDARI USIYEOGOPA


Wakuu, wakati umetimu wa kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli, na mafisadi ole wao wakae chonjo, haogopwi mtu, hapendwi mtu, hapa ni uzalendo tuu na maendeleleo ya Watz ndio yanayowekwa mbele na si matumbo ya watu binafsi na familia zao na watu wao wa karibu.

Hii ndio raha ya kuwa na Mbunge asietegemea ubunge au siasa pekee kama ndio njia pekee ya yeye na familia yake kuendelea kula na kuishi. Huyu Mh. akiona mizengwe imezidi 'taaluma' yake inatosha kumfanya yeye na familia yake kuishi raha mstarehe.

Lazima wabunge wetu wafikie wakati wachore mstari mwekundu na kutuma ujumbe mzito kwa wabunge waoga aidha wawatumike wananchi na kuacha kujali ubinafsi wao, na wasimame upande wa wananchi au wasimame upande wa mafisadi. It is time to make choice either with the general public or with mafisadi. You can't be both or undecided.

Mwakyembe wewe ni jemedari endeleza mapambano mkuu.
 
huyu ndio mbunge wa ccm ambae anauchungu na watu....sio mama kilango anayesema moja leo kesho analibadilisha.

spika na atoe nafasi tupate kuwekewa dhahiri muongo nani......manake lowasa na genge lake wanataka kujifanya wema na wasafi sana.
 
JK kweli wakati wake umefika?maana mm naona kabisa anapoteza mwelekeo wenzake watamshinda akidhani mambo yako shwrari kumbe kuna vugux2 laja kwa kasi sana .........wabunge wamezidi kuweka maslahi binafsi mbele badala ya utaifa na masilahi ya waliowatuma......"wapinzani sahihi watatoka ndani ya CCM...."
 
Yeye Anasema Itajumuisha Yote Hata Yale Yaliyoachwa Kwa Kuinusuru Serikali! Hapo Ameanzisha Jambo Jipya, Anataka Tuamini Kuwa Kuna Mengi Hayajatamkwa Mle Ripotini Ila Kamati Imeyahifadhi, Na Sasa Wako Tayari Kuyaweka Hadharani!! Kuna Nini Anatufundisha Dkt.Mwakyembe , Richmond Iligusa Wake Kwa Waume Matumboni Mwao, Leo Unatuambia Hukueleza Yote ? Kwa Faida Ya Nani? Na Sasa Unashauri Mvunje Kanuni Zenu Rasmi Ili Uyatamke Hayo Yaliyomo Sirini Kwa Faida Ya Nani ?!!
Hii ni kweli alitakiwa aseme yote wakati ule ule. Kidogo haijakaa vizuri.
 
Wakati jua linapochwea linachwea tu,hakuna kizuizi!ccm machweo yashafika,na muadhini swala ya magharibi ashatoa adhana,tujiandae!
 
SISEMU ilishapoteza mwelekeo tangu kitambo, siamini kama wananchi wa kule Kyela watamruhusu aondoke bungeni for good. Naamini watamruhusu ahame chama kisha agombee ubunge, arudi kulichachafya bunge na serikali. Sasa ndiyo tutaona nani ana nguvu SISIEMU au wananchi wa Kyela.

Hainingii akili serikali kuendelea kukumbatia wezi huku wakiendelea kudanganya wananchi eti zile pesa hazikuwa za serikali, bull%&*. Saa ya ukombozi imefika.
 
Bravo Mwakyembe, Six, come man, njoo ukamilishe unabii wa anguko la mafisadi!

Ujue kweli alisema Mkijiji awa fisadi wamelewa ugimbi, yaani walisha ona hoja wameizika NEC na tayari wakaona warushe vijembe bungeni na ulozi juu! Mungu awalinde Mwakyembe na kamati yako na asinunuliwe hata mmoja akaja wasaliti, simameni imara ukweli siku zote utashinda!
 
Back
Top Bottom