Je, Mwakyembe kujiuzulu Ubunge?!

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,133
1,225
Mbunge wa Kyela Dr,Mwakeyembe amelitaka bunge kutengua kanuni ili kuurudisha upya majadala wa Richmond Bungeni na wao kama kamati waruhusiwe kusema yote na ikibainika kuwa kuna mtu walimwonea yeye pamoja na wajumbe wa kamati yake wako tayari kujuuzulu ubunge wao.

Amesema kuwa hilo linatokana na wabunge pamoja na baadhi ya viongozi kueneza uzushi kuwa wapo walioonewa na wengine wanafanya jitihada za kuwasafisha kila kukicha na maneno ya uongo kila kona ya nchi.

Amesema kuwa ameamua kufikia uamuzi huo kwani kuna juhudi za makusudi zinafanywa na baadhi ya wabunge na viongozi wa chama kutaka kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa.

Pia kitendo cha Serikali kutokuchukulia maamuzi ya bunge serious na kuwachukulia hatua wahusika na badala yake wapo wabunge wanaendeleza huo mjadala bungeni ili kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa.

Akiwa anaongea hayo Lowassa alitoka nje ya bunge........

Bravo Mwakyembe.
 
Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,852
0

kaaaazi kweli kweli.
 
Mulugwanza

Member
Feb 3, 2008
88
95
Wabunge wote wangekuwa kama slaa, mwakyembe, zito and anna Tanzania ingekuwa kama ile nchi ya ahadi yenye maziwa kila kona!!!!!!!!!!!
 
Kevo

JF-Expert Member
Jun 12, 2008
1,333
0
embu angalia heading yako vizuri bwana wengine mapigo ya moyo yalikuwa yameshaanza kupishana hatuwezi kumuachia kijana machachari na shupavu kama huyu apotee ilhali mafisadi wanajizungusha tu huko bungeni lazima waadhibiwe.
 
Mfwatiliaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
1,325
0
Huyu mbunge ana busara sana, amevumilia naona sasa amechoka na kuunguruma..haya sasa, inaonekana kamati wana data nyingine ambazo hawakuziingiza kwenye ile report na inaelekea zinawagusa moja kwa moja wahusika wakuu ambao wanaotambulika kwa nickname "vigogo" wa ufisadi
 
Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,133
1,225
Uamuzi huu unatokana na juhudi za makusudi ambazo tangia jana zilikuwa zinafanyika ndani ya Bunge kuhakikisha kuwa wanawasafisha baadhi ya wahusika kwa kutumia kauli kali kali ndani ya bunge.

Naamini kuwa huu ni ujumbe mahususi hata kwa NEC YA CCM pamoja na JK kwani walijaribu hata kumsafisha huyu jamaa kwa kina sana na kuiponda kamati ya kina Mwakyembe .
 
Primera dama

JF-Expert Member
Apr 21, 2008
827
250
Wabunge wote wangekuwa kama slaa, mwakyembe, zito and anna Tanzania ingekuwa kama ile nchi ya ahadi yenye maziwa kila kona!!!!!!!!!!!
Ni kazi kuifikia hiyo nchi waulize wana wa israel watakueleza iliwachukua miaka mingapi kuifikia!Muulize MUSSA pamoja na kuwaongoza wanawaisrael lakini hakuiona kanaani!
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,383
2,000
Huyu mbunge ana busara sana, amevumilia naona sasa amechoka na kuunguruma..haya sasa, inaonekana kamati wana data nyingine ambazo hawakuziingiza kwenye ile report na inaelekea zinawagusa moja kwa moja wahusika wakuu ambao wanaotambulika kwa nickname "vigogo" wa ufisadi

Well said, La muhimu zaidi ni kwamba Mwakyembe haishi kwa kutegemea ubunge tu kama baadhi ya vimbembe humo ndani!!!!!! Hiyo ni sign tosha kwamba The guy is better than huo ubunge - Mwanaume hongera sana, courage yako inaokoa wamama wanaozaa kwa uchungu kila kukicha, we we hujui tu!!
 
Tuandamane

JF-Expert Member
Feb 2, 2008
1,221
1,225
Ni kazi kuifikia hiyo nchi waulize wana wa israel watakueleza iliwachukua miaka mingapi kuifikia!Muulize MUSSA pamoja na kuwaongoza wanawaisrael lakini hakuiona kanaani!
natabu zote alizopata Mussa toka anazaliwa na kutelekezwa kwenye mto
 
Tshala

JF-Expert Member
May 23, 2008
275
250
Inahuzunisha sana, mafisadi wao wanajiona kama wameshinda maana hamna hatua zinazochukuliwa, Bravo Mwakyembe. Yani habari ya Richmond ni kama imekufa nobody cares, and Watu kama wakina Mwanyika bado wanapeta!!! tena wanawekwa na kwenye kamati teule nyingine za uchunguzi. Tanzania kazi ipo!!!
 
Majembe

Member
Jun 18, 2008
35
0
miminachanganyikiwa na CCM kuliko chochote, jamani mbona hawaeleweki kama waliwapa watu kazi wakaifanya ipasavyo wanataka nn tena? Mwakyembe namuunga mkono wapitie upya na kama vipi aachie ngazi kama alivyosema na waanzishe chama kingine tutajiunga huko!!!!!!!!!!!
 
Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,338
2,000
hivi haya majadiliano ya bunge yanakwenda kwa mpangilio gani?
manake tulitegemea kuwa siku moja ifike aje waziri atoe ripoti imetekeleza vipi mapendekezo ya kamati ya bunge hivi ile siku imepita au bado?
au ndio amehisi wanataka kuiua hoja?
sitashangaa, manake hawa watu mafisadi wana pesa za kutosha, halafu walivyo wajinga wanapeana moyo kwa mambo ya kijinga kama haya.
sijui daktari wetu yuko wapi atutibu watanzania.
mimi huwa napenda sana bunge la baadhi ya states za USA yani historia ya kila mbunge ya choices katika kura zake inajulikana, hakuna kura ya siri.
 
Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,808
1,250
Jamani hoja ya Mwakyembe hapa ni kwamba hata Spika wa Bunge, alilegea kidogo maana hoja ya Richmond ni "AZIMIO LA BUNGE" lililopitishwa kwa kauli moja kwa hiyo ni sawa na sheria inahitaji utekelezaji tu. Kanuni za Bunge haziruhusu suala hilo kujadiliwa tena ndani ya Bunge lakini Spika amewaachia kina Chitalilo kuzungumza na sana sana akamwambia arudi kwenye hoja badala ya kukemea na kumwambia afute kauli yake na mwingine asirudie. Kanuni hiyo ndiyo iliyotumika kumzuia Rostam kuwasilisha maelezo ya kujitetea kwa kuwa hoja ilishapitishwa na kuwa ya Bunge si ya kina Mwakyembe
 
Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,808
1,250
Hoja hiyo ndiyo iliyomfanya Mwakyembe asema ikibidi kanuni itenguliwe Kamati iwasilishe upya mambo inayoyajua na wanaodhani walikosea wawasilishe ndipo ikibidi watajiuzulu kama walimuonea mtu
 
Power to the People

JF-Expert Member
Jul 11, 2007
1,199
2,000
I have a feeling this will wake some people up, wale waliozoea kusema yes Sir. CCM inakwenda na wale wajanja wangeanza kutafuta upande wa kusimama, na upande huo uwe ni wa wale wanaotetea maslahi ya wananchi.
 
Kubwajinga

JF-Expert Member
Jan 23, 2008
2,190
1,500
Je Mama Anna Kilango-Malecela na yeye vipi hakuinuka kuliongelea hili? Au hapa sasa ni pamoto kupindukia?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom