Je mwajua kuwa Barrick imeisha uzwa kiujanja na sasa ni Anglo America?

Mkira

JF-Expert Member
May 10, 2006
425
119
Hii ninasikia ni mara ya tatu kwa Kampuni hiyo kubadili jina.

Mara ya kwanza walichuma kampuni ya kikanada, baadaye Barrick na sasa ninasikia kuna mmliki mwingine hata mwezi mmoja bado!!?


HII YOTE NI JANJA YA KUKWEPA KODI! AU KASHIFA WANAKIMBIA JE VIONGOZI WETU HAWALIJUI HILO! MAANA jk ALISEMA KUANZI MWAKA 2010 WATAANZA KULIPA KODI JE HILO KAMPUNI JIPYA. HIZI NI ZA NDANI KWA WAFANYA KAZI WALIOKO HUKO!!

HUO NDIO UKWELI WENYEWE!

LOWASA VIPI?
 
Je mwajua kuwa Barrick imeisha uzwa kiujanja na sasa ni Anglo America?
Hii ninasikia ni mara ya tatu kwa Kampuni hiyo kubadili jina.

Mara ya kwanza walichuma kampuni ya kikanada, baadaye Barrick na sasa ninasikia kuna mmliki mwingine hata mwezi mmoja bado!!?


HII YOTE NI JANJA YA KUKWEPA KODI! AU KASHIFA WANAKIMBIA JE VIONGOZI WETU HAWALIJUI HILO! MAANA jk ALISEMA KUANZI MWAKA 2010 WATAANZA KULIPA KODI JE HILO KAMPUNI JIPYA. HIZI NI ZA NDANI KWA WAFANYA KAZI WALIOKO HUKO!!

HUO NDIO UKWELI WENYEWE!

LOWASA VIPI?
 
hatujui, ndio wewe unatuhabarisha.
saasa ni juu yako kama umekusudua kuleta upupu ili utuwashe tujikune au ukweli.

ila imekalia kiudaku udaku hii stori
 
Udaku! kampuni ya Ki Canada ndio hiyo hiyo Barrick, sasa sijui ya kanada sijui ya wapi ni UZUSHI.
 
Jamani nyie mnataka source na Bikira hapoa alishasemaa? na mnukuu
HIZI NI ZA NDANI KWA WAFANYA KAZI WALIOKO HUKO
. Yeye kasikia kaleta hapa kama kuna mwenye info zaidi aziweke kama hatuna basi tupige kimya akipata nyingine ataweka.
 
Nimeambiwa na mfanyakazi wa humo ndani Barrick huko Tarime.

Tena ninasikia siku hizi hata wale wabongo wasomi waliokuwa wanjipendekeza kwa Matajiri Barrick, nao wameamua kuungana na wenzao watanzania ili kudai haki zao.


Je mwajua vifaa vya kuchimbia(mitambo) ni mikubwa kuliko hata inayotumika huko Ghana ambako dhahabu inapatika chini saana wakati ya kwetu iko juu juu!! Mpaka hata hao waghana wachache wanaofanya kazi humo Barrick wanaishangaa nchi yetu na sisi watanzania?

Tulitakiwa kama serikali kuwapa limit ya capacity ya vifaa ili wachime taratibu badla ya kuchukua mali nyingi kwa muda mfupi kama vile wanafuzuzana na muda wa miaka mitano ili watuachie mashimo.

Ni vema pia waulizeni ndugu, marafiki zenu wanaofanya kazi huko ili tuone kama habari zinatofautiana.

KWANI KUBADILI MAJINA NI JAMBO GENI!

TUNA MFANO HALISI KWA SHERATON, ..., THEN MOVENPICK.

LISEMWALO LIPO AU LAJA. LAKINI PIA YAWEZEKANA IKAWA SI ZA KWELI.

ILA KWA WALAJI NA WALE AMBAO NDUGU ZAO WANASAIDI MIKATABA AU AMBAO SERIKALI NI ZAIDI YA BABA/MAMA ZAO WATAKIMBILIA KUSEMA NI UONGO BILA HATA KUJIULIZA.
 
Nadhani si vyema kukatisha tamaa watu wenye taarifa za awali ambazo zinaweza kufanyiwa kazi na ama kuthibitishwa ama kukanushwa. Hili si gazeti kwamba habari zake lazima zikamilike. Zinaweza kuja habari zilizokamilika na pia zinaweza kuja FUNUNU ambazo zinawapa wana JF nafasi ya kuchambua. Kazi kwetu kuchambua. Inawezekana hata ikawa ni suala lilipo katika mjadala kama ilivyokua Backlays walivyonunua NBC kupitia ABSA, ilianza kama FUNUNU kabla ya mjadala kulipuka huko Afrika Kusini na hatimaye kutimia na kuwa kweli na hadi leo, serikali ya Tanzania haijasema chochote pamoja na kuwa na hisa katika NBC. Viongozi wetu wamewaachia ABSA kuuza kwa bei kubwa wakati wao waliichukua benki bureeeeeeee. na sasa wamepata fedha wamenunua benki huko Msumbiji, sijui serikali yetu imepata nini.
 
yaani bado lile jengo jeupe pale baharini kuuzwa na wananchi wenyewe kupigwa bei tugawane vyetu kila mtu ale kona kivyake....
 
Back
Top Bottom