Je, Muungano Bridge inawezekana Tanzania?

Ni upi mfanano wa Mfereji wa Suez na hilo daraja unalo-propose?

NI Waafrika wangapi wanaenda Misri kuangalia hayo mapiramidi kabla hatujawafikiria kuja kuangalia "daraja letu"?

Ikiwa Daraja la Kigamboni ambalo halifiki hata 1KM limekula takribani TZS 300 Billion, uliwahi kujiuliza daraja lenye urefu wa zaidi ya 40km litakula trilion ngapi? Nitakuwa nimesema uongo nikisema litachukua zaidi ya TZS 25 Trillion?

Ni usafirishaji wa nini hasa unaosema "miondombinu ya kurahisisha usafirishaji kwa bei nafuu" hadi daraja linaloweza kugharimu zaidi ya trilioni 25 liweze kuwa na tija? Cargo or passengers transport?

Kama ni cargo... ni mzigo upi na utakuwa unatoka pande ipi kwenda ipi hadi uwe na tija kuusafirisha kupitia daraja linalopita baharini kwa zaidi ya 40km (from Bagamoyo)

Na kama ni abiria, do you really believe usafirishaji wa abiria kwenye daraja refu kama hilo unaweza kuwa commercially and economically viable?

Thread 'Bilioni 18.8 Kujenga Ofisi ya Makamu wa Rais Dodoma' Bilioni 18.8 Kujenga Ofisi ya Makamu wa Rais Dodoma
 
Sio lazima uandike neno faida, ukichambua ulivyoandika maana yake faida yake itapatikana baadae sana au faida ni ndogo sana kiasi kwamba tusiitegemee kuendesha nchi, kumbuka kuna migodi inamiaka zaidi ya 30.
Kwanini ufanye assumptions wakati takwimu zinapatikana kirahisi kabisa?!!

Moja ya posts zangu jana , nilitolea mfano wa Cardia Valley Gold Mine uliopo Australia ambako hatutarajii kuwe na upikwajii!! Cardia ni miongoni mwa migodi mikubwa kabisa duniani!!

Pamoja na kuwa miongoni mwa migodi mikubwa kabisa duniani, mwaka 2020 walizalisha 822 koz of gold, ambayo ni takribani Kilogram 23.4k. Kama dhahabu ile wangeuza jana, ingeingiza almost USD 1.4 Billion!

Now look, pamoja na bei ya dhahabu kuwa kubwa sana, bado mgodi mkubwa kama huo uliishia kuingiza GROSS Revenue of USD 1.4 Billion!! WHY?! Hapo ndipo linakuja suala la scarcity!

Anyway, watu wanaamini Magu kasimimamia vizuri suala la madini, na kwahiyo hakuna kupigwa!!! Sasa hapa chini ni taarifa ya Bariick Gold kwa mwaka 2020

Barrick.png


Utaona hapo juu, 84% ya dhahabu iliyozalishwa na North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi ni 261 koz, 44koz, and 84koz respectively. Na 100% ya hiyo production ni 311 kozi, 52 koz, and 100koz respectively.

Hapo bila shaka utaelewa kwanini nilisema Cardia ni mgodi mkubwa kabisa kwa sababu migodi yetu 3 total imezalisha 463koz (311+52+100) wakati Cardia peke yake imezalisha 822koz.

Sasa kabla hujatoa gharama yoyote, kwa bei ya leo (according to goldprice.org) dhahabu YOTE ilyozalishwa kwa migodi yetu 3 ni USD 820 Million>>> today's price is about $1770 per oz >>, 463koz = 463,000 oz

Ukiangalia second column in RED, utapata average cost of sales kwa hiyo migodi 3 ni USD 1171/ounce! Now look, wakati bei ni 1770/oz, cost of sales (yaani total cost) ni sawa na 1171/oz!! Hapo sasa, fanya mwenyewe hesabu za ON and OFF, kisha tafakari!!

And remember, hapo kama nchi katika USD 820 Million, tutakachopata ni kodi + 16%...

NARUDIA... acha kufanya assumption! Hakuna aliyesema HAKUNA FAIDA. Hoja yangu ni kwamba mna-OVERRATE sana madini!!! Na ukitaka kujua mna-overate sana, chukulia ile Gas Processing Plant ya pale Lindi ambayo ilikuwa ijengwe kwa USD 30 Billion!

I REPEAT, GAS PROCESSING PLANT peke yake ilikuwa ijengwe kwa USD 30 Billion!!

Kwa upande mwingine, Barrick Gold ndiyo kampuni kubwa kuliko zote ya uchimbaji dhahabu duniani!! Kama unavyoona kwenye hiyo screenshot hapo juu, wana migodi kibao duniani na mikubwa kuliko iliyopo Tanzania.

Kwenye hiyo screenshot, kuna migodi ya Nevada ambayo nimenyofoa kwenye screenshot ambayo kwa pamoja inazalisha 2131koz... linganisha na hiyo 463koz tunazozalisha sisi!!

Lakini pamoja na ukubwa wote huo wa Barrick Gold, thamani yao ni hii hapa chini:-
NasDaq.png


What's Market Cap? Investopedia wanatusaidia kwa kutueleza kwamba:-
What Is Market Capitalization? Market capitalization refers to the total dollar market value of a company's outstanding shares of stock. Commonly referred to as "market cap," it is calculated by multiplying the total number of a company's outstanding shares by the current market price of one share.
Kumbe pamoja na sifa zote nilizomwaga kwa Barrick Gold, shares ZOOOOOOOOTE thamani yake ni USD 33.2 Billion, almost karibu sawa na pesa inayotaka kujenga ONLY one Gas Processing Plant pale Lindi!!
 
Nani atagharamia ujenzi wake?

Nani atahakikisha usalama wa daraja hilo 24/7/365?

Unajenga daraja kwa gharama kubwa ambazo haziingizi kipato chochote kwa nchi badala yake mzigo wanatwikwa wananchi kulipa, haiwezekani.
Lile daraja la umoja la CCM na FRELIMO mbona sasa ni la kimkakati kwa chumi za SADC na Ushoroba wa Kusini mwa Tz. Hivi sasa korosho za Cabo Delgado zinaingizwa Tz kupitia daraja la umoja na kupakiwa kwenye meli kwenda Ulaya na China. Sasa hivi miundombinu ni alama nyingine mpya ya diplomasia ya kisiasa na kiuchumi pia. Mkiwa na miundombinu ya kuwaunganisha na wenzenu siyo rahisi kupigana vita. Tz na Zambia (TAZAMA, TAZARA na Tz-One Road) zinaimarisha urafiki na udugu wa kihistoria wa mataifa hayo mawili. Ni vivyo hivyo kwa daraja la Kagera, iliyokuwa reli ya Tz hadi Voi Kenya chini ya East African Railways Corporation (iliyouawa na siasa za itikadi shindanishi duniani), Pipelines ya Tz-Ug. Hivyo Samia Suluhu Hassan Muungano Bridge itaimarisha uchumi wa kitaifa, kikanda na muungano pia. Sekta moja tu ya uchumi inatosha kujenga daraja hilo tokea Bara, Unguja, Pemba hadi Mombasa; na Tz ina sekta nyingi. Mwl. Nyerere aliendesha nchi bila sekta ya migodi, alitumia sekta ya kilimo pekee kwa asilimia kubwa ndiyo maana alijenga viwanda 14 vya nguo, sekta zingine hakuzigusa zililala au alizigusa kwa asilimia ndogo sana. Muhimu ni usimamizi na uratibu mzuri tu wa mradi.

32c3444c249363ae55bd62f808f68474.jpg
13

Unity Bridge
Taswira kwa hisani ya google
 
Kuna kipindi nilikuwa nimejipumzisha pale Bagamoyo Beach, nikakiona nadhani kisiwa cha Nungwi, nadhani kuanzia pale hadi Unguja Daraja linawezekana ila litakuwa ghali ghali kweli kweli.
Hata maeneo ya mkadini usiku kukiwa tulivu
Ukikaa unasikia kelele kwa mbali tokea unguja

Ova
 
Yan unafananisha suez canal na daraja kweli? Ebu kuwa serious bas
Hukuelewa maudhui/content ya mada. Fanya revision. Hoja haikuwa ufanano wa structure kama ulivyoelewa bali ufanano wa manufaa ya kiuchumi tena nikaongezea na Mapiramidi (kusisitiza hoja ya manufaa ya kiuchumi), sasa kwa mdadisi mzuri wa maudhui/content ilitosha uone kama Mapiramidi nayo yanajengwa majini? Mbona hukuhoji ufanano wa daraja na Mapiramidi badala yake ukaohoji ufanano wa daraja na mfereji wa Suez? Nakupongeza kwa brainstorming ambayo inaonyesha at least ume-review mada tofauti na wengine wanaokimbilia kuchangia bila kusoma mada kwa uvivu na uwoga wa uwingi wa texts.

Mwalimu yupo kwa ajili ya makosa ya mwanafunzi na siyo kwa ajili ya mambo sahihi ya mwanafunzi Majwala, H. A. (1983).
 
Hukuelewa maudhui/content ya mada. Fanya revision. Hoja haikuwa ufanano wa structure kama ulivyoelewa bali ufanano wa manufaa ya kiuchumi tena nikaongezea na Mapiramidi (kusisitiza hoja ya manufaa ya kiuchumi), sasa kwa mdadisi mzuri wa maudhui/content ilitosha uone kama Mapiramidi nayo yanajengwa majini? Mbona hukuhoji ufanano wa daraja na Mapiramidi badala yake ukaohoji ufanano wa daraja na mfereji wa Suez? Nakupongeza kwa brainstorming ambayo inaonyesha at least ume-review mada tofauti na wengine wanaokimbilia kuchangia bila kusoma mada kwa uvivu na uwoga wa uwingi wa texts.

Mwalimu yupo kwa ajili ya makosa ya mwanafunzi na siyo kwa ajili ya mambo sahihi ya mwanafunzi Majwala, H. A. (1983).
Na mm nilimaanisha ufanano wa manufaa sio structure. Kumbuka ule mfereji ni shortcut ya kusafirishia mizigo inayotoka ulaya kwenda asia na africa uwez linganisha na daraja la kutoka bara kwenda visiwani
 
Na mm nilimaanisha ufanano wa manufaa sio structure. Kumbuka ule mfereji ni shortcut ya kusafirishia mizigo inayotoka ulaya kwenda asia na africa uwez linganisha na daraja la kutoka bara kwenda visiwani
Zanzibar iko ndani ya soko la SADC lenye idadi ya walaji 277ml, GLR walaji 107ml na EAC is home to 177ml consumer market. Kama Zanzibar ikiwa na free port huoni daraja la Samia Suluhu Hassan Muungano Bridge litakuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi huenda kuliko hata Suez Canal? Wafanyabiashara wengi watalitumia kuingiza bidhaa. Hili daraja litafungua Marine Corridor (Ushoroba wa Baharini) kuunganisha EAC's, SADC's & GLR's Landlocked (siku hizi wanajiita Landlinked)?

Ngoja niwape siri.
Marehemu Maalim Seif alitamani kama angeingia Ikulu, angejenga Airport kubwa ya Znz kuliko JNIA, KIA, Entebe na JKIA ili ndege kubwa duniani zitue pale kushusha shehena alafu ndege za Znz zichukuwe kusambaza EAC, GLR, SADC na sehemu zingine za Afrika. Mkakati huu umesaidia sana Uturuki kukuwa. Uturuki haina viwanda lakini imeruhusu wazalishaji duniani kwenda kujenga maghala ya bidhaa zao kule ili wakizalisha kwao huko basi wanasafirisha hadi Uturuki kuhifadhi na supply inaanzia Uturuki ndiyo maana mnasikia watu wanaenda Uturuki kuchukuwa mizigo, matokeo yame-ripple-effect kwenye sekta za usafirishaji, hoteli, utalii, visa nk (Multiplier-effect) na kufanya sasa Airport ya Ankara kuwa busy namba 2 Ulaya ikitanguliwa na Heathrow Airport ya London. Ankara Airport ukubwa wake unatoka takriban Mbagala hadi Bunju na kila baada ya masaa mawili ndege 200 zinapaa zinaachia parking 200 zingine zinatua 24/7/365 (Port turnaround (embarkation and disembarkation).

Mhe. Rais, jenga Samia Suluhu Hassan Muungano Bridge hata Nyerere na Abeid Karume watakuombea kwa sababu utakuwa umewaenzi vizuri pia, utakuwa umetafuna mfupa ulioshinda watangulizi wako na utakuwa kiongozi wa kwanza mwanamke katika historia duniani kufanya yasiyowezekana na yaliyoshinda wanaume wa shoka.
 
Magufuli angetufikisha hapa bila mikopo ya kipuuzi. Madini ya tz yanaweza kufanya kila kitu.

Ujinga ujinga tunatozwa tozo ovyo madini wagawa nje kwa mikataba mibovu.
 
Back
Top Bottom