Je muswaada huu utadhibiti fedha chafu... Kwenye uchaguzi???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je muswaada huu utadhibiti fedha chafu... Kwenye uchaguzi????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BabuK, Dec 23, 2009.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2009
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Fedha chafu sasa basi

  [​IMG]
  Mwandishi Wetu​
  Disemba 23, 2009 [​IMG]
  HATIMAYE serikali imeonyesha kwa vitendo nia yake ya kukabiliana na tatizo la rushwa katika siasa kwa kutangaza muswada wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kwa nia ya kuweka utaratibu wa kudhibiti fedha chafu kuingia katika siasa.
  Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, jana Jumanne ilitangaza muswada sheria mpya ya kusimamia gharama za uchaguzi na kuzifanyia marekebisho Sheria ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kupitia muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali (The Electoral Laws, Miscellaneous Amendments Act, 2009).
  Marekebisho hayo pamoja na mambo mengine yatawezesha kutungwa kwa Sheria ya Gharama za Uchaguzi (The Election Expenses Act, 2009) kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010.
  Muswada huo uliosainiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Novemba 26, 2009 unaonyesha kwamba sheria hiyo mpya ikipitishwa na Bunge itasimamia na kuratibu mapato na matumizi ya gharama za kampeni kwa vyama vya siasa na wagombea.
  Katika maelezo ya ‘madhumuni na sababu’, imeelezwa kwamba sheria hiyo itaweka utaratibu utakaoiwezesha Serikali kuchangia gharama za kampeni na uchaguzi kwa vyama vya siasa na pia kuratibu zawadi, misaada na michango itakayotolewa na wagombea wakati wa kampeni.
  “Sheria inalenga katika kuweka utaratibu wa kudhibiti matumizi ya fedha wakati wa kampeni za uchaguzi na kuweka mfumo wa kisheria wa uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma na vile vile kuanisha adhabu kwa watakaokiuka masharti,” inaeleza sehemu ya madhumuni ya muswada huo.
  Sheria mpya imeelezwa kulenga kupunguza matumizi mabaya ya fedha wakati wa kampeni na uchaguzi ikiwa ni pamoja na moja ya njia ya kudhibiti vitendo vya rushwa ndani ya vyama vya siasa wakati wa mchakato wa uteuzi na wakati wa uchaguzi.
  Kwa mujibu wa maelezo ya muswada huo, kutakuwapo na utaratibu wa kisheria utakaowezesha kuwapo haki na usawa katika matumizi ya vyombo vya habari vya umma na ulinzi kutoka kwa vyombo vya dola wakati wa kampeni hadi uchaguzi wenyewe.
  Hatua kadhaa zimependekezwa katika muswada huo ikiwa ni pamoja na kufutwa kwa mgombea atakayejihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa kampeni na uchaguzi na kuwapo kwa vipengele vya faini ya hadi shilingi milioni kumi.
  Mbali ya vitendo vya rushwa, sheria mpya itawalazimisha wagombea na vyama vya siasa kutoa taarifa ya vyanzo vya mapato nje ya ruzuku itakayokuwa inatolewa na Serikali, hatua ambayo imeelezwa inalenga kupunguza kuingia kwa fedha haramu katika siasa.
  Kumekuwapo na vilio vya matumizi makubwa ya fedha katika siasa kiasi cha kuwafanya watu wenye uwezo wa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kukata tamaa kujihusisha katika siasa na hivyo kugeuza siasa kuwa mikononi mwa wenye fedha pekee.
  Hatua ya sasa ya Serikali kuandaa sheria ya udhibiti wa matumizi ya ovyo ya fedha itaibua changamoto jipya kwa watu wenye uwezo mkubwa kisiasa ambao walikwisha kukata tamaa kujihusisha na siasa kwa kuchelea kutumia rushwa.


  Chanzo: Raia Mwema toleo la Disemba 23-29, 2009.
   
Loading...