Je, Museveni haamini kama Corona imeisha Tanzania? Kabudi amejikuta kapata aibu!

Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,051
12,560
Leo wakati viongozi wakiondoka viwanja vya Dodoma alianza kuondoka Rais Magufuli akafuatiwa na Rais Museveni! Wakati Museveni akisubiri gari nilimuona Kabudi akisogea eneo ambalo kulikuwa na viongozi wa Tanzania ambao walikuwa wanawaaga wageni na tayari walikuwa wameshaagana na Museveni kwa ishara ya kupungiana mikono!

Kabudi alipofika pale akaenda moja kwa moja kama na kwa tabasamu kama anataka kumpa mkono Museveni! Museveni alichofanya alimzuia kwa kunyanyua mikono miwili juu kama anamwambia rudi nyuma! Kabudi akapata ganzi na kurudi nyuma! Baada ya dakika chache aliondoka kabisa eneo hilo,nadhani alitonywa kuwa hapaswi kuwa hapo kwani uwaziri wake wa mambo ya nje ulishakoma!

NB: Museveni anatusisitiza Watanzania tuangalie TBC kwani hata yeye aliangalia kipindi cha uchaguzi na matokeo ya kwanza kutoka ilikuwa Hai na alipoona Hai tayari biashara imeisha akajua kwisha kazi!

My take: Inaonekana Museveni anamfuatilia sana Mbowe na ndiye aliyemshauri Rais Magufuli kuwa aanze naye na liwe jimbo la kwanza kutangazwa!

Kama nimekuchanganya na hujui uchangie lipi,ni juu yako!!!
 
Usijali hata sisi tunajua mmechanganyikiwa sana tangu tume itangaze matokeo rasmi ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom