Je,Museveni atapata nafasi ya kutawala hadi kifo chake?

Tony antony

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
4,988
3,268
Katika Hali isiyo ya kawaida,nchini Uganda chini ya baraza la mawaziri wamekusudia kupeleka muswada bungeni wa kumuongezea muda raisi wa sasa mhe.Kaguta Museveni na kumpa uwezo wa kutawala hadi kifo.

Hii inakuja muda mfupi baada ya bunge hilo kupitisha mabadiliko ya Katiba na kuweka kikomo cha kutawala Urais hadi kufikia miaka 70.

Upande wa Upinzani umekusudia kupinga vikali jambo hilo kwa hali yeyote ile.

Je,Mhe.Yoweri Kaguta Museveni chini ya baraza lake wataweza kupitisha huo muswada na kumkabidhi raisi huyo kiti hadi kifo??
 
Huu ni upumbavu wa viongozi wa kiafrika, ni vyema sana hawa viongozi wakubali kukabidhi madaraka wakiwa na akili zao timamu ili waweze kuenziwa na vizuri vilivyopo na vijavyo. Uchumi wa madaraka mwisho wake ni mbaya sana!
 
Toka wapate Uhuru hadi leo, haijawahi kutokea makabidhiano ya madaraka nchini Uganda.
Huondoka kwa Mapinduzi ya kijeshi tu.
 
Tunashangaa huku kuongeza miaka saba,mambo yapo huko bwana...sisemi nkamia anachokifanya ni kizuri ni kibaya si cha kukiangalia kwa jicho la kawaida....lakini nkamia ana haki ya kukifanya alichokifanya kulingana na katiba yetu.
 
Huu ni upumbavu wa viongozi wa kiafrika, ni vyema sana hawa viongozi wakubali kukabidhi madaraka wakiwa na akili zao timamu ili waweze kuenziwa na vizuri vilivyopo na vijavyo. Uchumi wa madaraka mwisho wake ni mbaya sana!
....Haya ndiyo mambo yanayofanya akina Trump kusema kwamba tunahitaji kutawaliwa tena, na walivyo wapuuzi wanaweza kupitisha hilo jambo.
 
Haitashangaza atakapojitangaza kuwa mfalme Mu7, na atatawala hadi mauti. Akianza kuanguka kama mfalme wa anakotaka kwenda ROMA, yeye atawanyonga walinzi.
 
Back
Top Bottom