0890
Member
- Jul 11, 2015
- 28
- 42
Nami naomba nichangie katika hili. Dhambi si kitu useme imeumbwa na Mungu, dhambi ni hali ambayo inamfanya mwanadamu ajiweke mbali na Mungu kutokana na mawazo yake, matendo yake, na ata maneno yake wakati mwingine. Kama ilivyo mbingu si sehemu bali ni hali ya kuwa katika ukalibu na Mungu. Vitabu vya dini vipo wazi sana shida yetu tulio wengi tunasoma " literally " . Mungu amemuumba binadamu na malaika wakiwa huru kama ishara ya upendo kwa viumbe vyake, maana pasipo Uhuru akuna upendo na Uhuru bila nidhamu utupeleka upotovuni ndio maana Mungu akaluhusu viumbe vikose vikiamua lakini alishawajuza maana ndani ya mioyo yetu Mungu mwenyewe ameweka sheria zake. Shida walioipata malaika ndio tuipatayo wanadamu kukataa kuwa viumbe na kutaka kuwa Mungu, ukijichubguza vyema utaona ndani yako kuna maelekeo au matamanio ya wewe kuwa Mungu wa maisha yako. Kifo kinachozungumziwa kwenye maandiko matakatifu sio physical death bali ni spiritual death na ndio maana Adam na Eva walipo kula tunda ( walipo asi ) walijihisi kuwa mbali na Mungu that we call physical death. So in any way we can not escap physical death.