Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Para
Musa aliikosa nchi ya ahadi ila alipokufa alienda paradise.

Nchi ya ahadi ndiyo paradiso. Raha - nchi ya asali na maziwa. Ilimaanisha sasa ku-hustle vile jangwani halafu asifike alikokuwa akienda? Wapi imeandikwa kuwa alienda paradiso?
 
Yule Musa aliemtokea Yesu wakati alipopanda mlimani na baadhi ya wanafunzi wake unajua alitokea wapi?? Hivi unajua nabii Musa alizikwa na Mungu kwa jinsi alivyokuwa anampenda.Musa alienda pazuri kushinda hao walioingia kanaani.
Para

Nchi ya ahadi ndiyo paradiso. Raha - nchi ya asali na maziwa. Ilimaanisha sasa ku-hustle vile jangwani halafu asifike alikokuwa akienda? Wapi imeandikwa kuwa alienda paradiso?
 
Amri zilikuwepo tangu kuumbwa kwa Adamu na Hawa, kwa mfano, wasile tunda. Hii ni amri.
Amri za Mungu zilishushwa duniani baada ya dhambi kuingia. Anyways, dini/imani kwangu kwa sasa haina mashiko.
 
Kuna wakati nilisoma coment yako ukaonyesha wasiwasi wa kwamba dunia ingekuwa bila dini ingekuwaje.Je dini imekuwepo siku zote hizo Unahisi ilianza anza vip?
Dunia nzima kwa sasa ina watu Billion 7.,,Almost Billion 5 wanasali japo sio kwa Mungu mmoja.Hivi idea ya kusali ndani ya binadamu Unaweza kuielezea vip?
Kwa nini ndani ya binadamu kuna uhitaji wa sala.??
Huoni hio inaonyesha kwamba kuna nafasi ndani ya binadamu inakuwa special kwa kutimiza ibada na mtu anahisi mkamilifu zaidi akisali.??

Huoni kwamba Kusema hakuna Mungu ni ajenda ulioibeba ila ikiwa ni makusudio ya viumbe wasioonekana wenye kujua siri nyingi kushinda wewe??

Huoni kwamba na wewe umekuwa mhanga wa kuamini kusudio hasi na wewe umelibeba kulieneza japo ulikusudiwa kuliamini tu?
Mungu hayupo, kama unabisha, thibitisha yupo.
 
Kuna wakati nilisoma coment yako ukaonyesha wasiwasi wa kwamba dunia ingekuwa bila dini ingekuwaje.

Nina kawaida ya kufanya kuwaza na kuwazua sana, hivyo pengine ninapowaza na kuwazua unaweza kuona kama wasiwasi.

Mwalimu Nyerere aliwahi kuulizwa kama dini yake inamsukuma vipi katika maamuzi ya kisiasa, akajibu vizuri sana kwamba ni swali gumu kulijibu kwa sababu hawezi kurudi nyuma akue bila kuwa na dini ili ajione anaweza kuwa mtu gani bila dini.

Je dini imekuwepo siku zote hizo Unahisi ilianza anza vip?

Dini ilianza kwa watu kutaka kujipa majibu ya maswali ambayo hawakuwa na majibu yake. Watu wana kawaida ya kwenda wakiboresha majibu yao kadiri wanavyozidisha uelewa, kwa hiyo zamani watu waliokuwa hawayaelewi mazingira, waliona kuwa kama baba anavyozaaa mtoto na kumlea, au anavyojenga nyumba, basi lazima kuna baba mkubwa huko juu aliyeumba dunia na kuumba watu. Ni mawazo primitive. Ndiyo hizo habari za kusema radi ni sauti ya Mungu kakasirika.

Sasa hawa watu wa zamani hawakujua mengi katika sayansi, hawakujua umeme wa radi unafanya kazi vipi, hawa naweza kuwasamehe kwa sababu hawakuwa na internet.

Sasa kijana wa leo ana internet, tena kwenye simu ya mkononi, habari zote za sayansi anaweza kuzi Google, lakini bado anaamini habari za miujiza ya Mungu tu? Kama fact?

Huyu sina msamaha kwake kabisa.

Dunia nzima kwa sasa ina watu Billion 7.,,Almost Billion 5 wanasali japo sio kwa Mungu mmoja.Hivi idea ya kusali ndani ya binadamu Unaweza kuielezea vip?

Profesa Noah Yuval Harari ameelezea vizuri sana katika vitabu vyake "Sapiens: A Brief History of Humankind" na "Homo Deus: A Brief History Of Tomorrow" kuhusu kitu ambacho watu wana uwezo nacho sana, kinaitwa "manufactured reality".

Watu wana uwezo wa kutengeneza uongo kuwa ukweli, mpaka ule ukweli ukakubalika kabisa. Chukulia fedha za makaratasi. Noti ya US $ 100 ina thamani sana. Lakini thamani yake ni ya kutungwa na watu tu. Ukiwa katika kisiwa ambacho hakina watu, umetupwa huko, unapewa uamuzi uchague papai moja na $100, papai litakuwa na thamani kuliko $100. Maana $100 thamani yake si ya msingi, inategemea na mazingira. Ni ya kupachikwa tu na watu.

Idea ya kusali iliwekwa na watu waliokuwa na maswali ambayo hawana majibu yake, wakajipachikia majibu rahisi waliyoyajua wao.

Kwa nini ndani ya binadamu kuna uhitaji wa sala.??

Kuna watu wanahitaji madawa ya kulevya, wengine wanahitaji kununua nguo kila weekend.

Hilo lina maana gani? Madawa ya kulevya ni Mungu? Nguo ni Mungu?

Mimi sihitaji sala. Ulaya ya Kaskazini watu kibao hawahitaji sala, makanisa yako matupu.

Huoni hio inaonyesha kwamba kuna nafasi ndani ya binadamu inakuwa special kwa kutimiza ibada na mtu anahisi mkamilifu zaidi akisali.??

Sala ni therapy kwa watu masikini. Wenzetu matajiri wanaenda kwa therapists wanafanya therapy ya matatizo yao ya kisaikolojia.

Sala ni therapy kwa masikini wasio na therapists. Una mzigo wa matatizo yako, badala ya kwenda kwa therapist, unaenda kwa mchungaji kanisani au msikitini unafanya sala zako, unatua mzigo wako, unajisikia afueni.

Ni saikolojia tu.

Huoni kwamba Kusema hakuna Mungu ni ajenda ulioibeba ila ikiwa ni makusudio ya viumbe wasioonekana wenye kujua siri nyingi kushinda wewe??

Viumbe gani wasioonekana? Unaweza kuthibitisha wapo na si hadithi zako tu?

Huoni kwamba na wewe umekuwa mhanga wa kuamini kusudio hasi na wewe umelibeba kulieneza japo ulikusudiwa kuliamini tu?

Kama kusema Mungu hayupo na kama yupo athibitishwe ni kuamini, basi kunyoa kipara ni mtindo wa kusuka nywele.
 
Acheni mchezo na mambo ya Mungu, ina maana huko mbinguni kuna serikali ya Mungu?? Jeshi la Mungu lilishinda jeshi la shetani?? Pure imagination!!
 
Mwandishi mmoja aliwahi kuandika hivi juu ya asili ya dhambi
"Haiwezekani kuelezea chanzo cha dhambi ili kutoa sababu ya uwepo wake,lakini mengi yaweza kufahamika juu ya dhambi ili kubainisha kikamilifu haki na ukarimu wa Mungu,Mungu kwa namna yeyote ile hahusiki na uwepo wa dhambi,hakukuwa na uondoaji kiholela wa neema ya Mungu,hakukuwa na upungufu katika serikali ya Mungu,uliotoa nafasi kwa uasi,dhambi ni kitu kilichojipenyeza ambacho uwepo wake hauna sababu inayofaa kutolewa,kuitolea udhuru ni kuitetea.Endapo udhuru wake ungepatikana,ingekoma kuwa dhambi..."GC,

maandishi hayo nadhani yana tosha pia kumb 29:29 inatoa majibu kwa maswali kama yako
maswali mengine hata utafutaje hauta pata jibu kamili mfano ukichukua rocket yenye kasi mara100 kasi ya mwanga kisha ukasafiri nayo kuelekea angani je,unafikiri kunasiku utafika mwisho? Na kama ukikuta mwisho kuna ukuta je,upande wa pili kutakuwa na nini?
Kama ambavyo huwezi kufika mwisho wa ulimwengu vivyohivyo hauwezi kufika ukomo wa kuelewa juu ya dhambi

so dont dig too deep

mchamba sana huondoka na Mavi

have a good day
 
Nguruwe we,na ww thibitisha kama hayupo
Kwa hiyo unamuuliza nguruwe akuthibitishie Mungu wako yupo we msen.ge baridi?

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, kusingekuwa na mjadala wa kutaka uthibitisho wa kuwapo kwake.

Unavyoniuliza nithibitishe hayupo, ni uthibitisho kwamba hayupo.
 
Thibitisha Mungu wako yupo, acha longolongo.
 
Kwa hiyo unamuuliza nguruwe akuthibitishie Mungu wako yupo we msen.ge baridi?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, kusingekuwa na mjadala wa kutaka uthibitisho wa kuwapo kwake.
Unavyoniuliza nithibitishe hayupo, ni uthibitisho kwamba hayupo.
Mungu hawezi jihusisha na mijadala ya kipuuzi hata kama unaohusu
 
Mkuu wewe huwa unatushinda kwa kutuwahi kuwa tuthibitishe uwepo wa Mungu ila na mimi nikikwambia unithibitishie kuwa vilivyopo duniani vimejiumba vyenyewe basi ugumu utakaokutana nao ndio huo nasi tunakumbana nao kukuthibitishia uwepo wa Mungu.
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo na si hadithi zilizotungwa na watu tu?
 
Kwahiyo mkuu kwa lugha nyepesi Mungu alichokifana ktk hii dunia ni sawa na mtu kununua au kudondoa muvi ya vita na kuanza kuitizama na kuifurahiya? Yani aliiumba dunia na kuiweka ktk matatizo ya Vita, njaa, umasikini ili akae chini ashuhudie huku ana popcon pembeni?
Maandiko gani Sakayo, binafsi nakuwa na maswali hadi naacha nisije kusema neno zito.

Mungu alifarakanisha mataifa, ili yapigane watu wafe. Mungu gani afanye hivyo watu wafe?

Kumbuka safari ya waisraeli toka Misiri kwenda Kaanani, watu wengi walikufa kabla ya kufika huko, Kweli Mungu anapenda watu wake wafe?

Herode mfalme, aliuwa watoto wachanga sana, huyo Mungu alikuwa wapi aache vichanga vife?

Why? Why?
 
Ni sawa na kutaka kujua kabla hujazaliwa ulikuwa wapi? na siku unazaliwa duniani ilikuwaje...Je nani alikufundisha kwamba chuchu ukiwekwa mdomoni unyonye ili mawaziwa yatoke....ni sawa na kutaka kujua wakati wa kufa inakuwaje na baada ya kufa unakwenda wapi...

Mambo ya uumbaji si SIRI nzito...hapo ndipo upeo wa mwanadamu wa kufikiri unapokoma....hata uwe una degree za sayansi zote ila kuna mambo huwezi kuyajibu kwa akili zako....

Manabii wa kale walipewa ufunuo wakaandika baadhi tu ya mambo ila kuna mambo mengi sana ambayo yanabakia kuwa SIRI za uumbaji...

Kwa mfano Mchawi wa kwanza kabisa kupaa na nguo au kuua wa uchawi alifundishwa na nani?
 
hivi wewe,ngoja nikupe swali ukilijibu utajua kama Mungu yupo au la

hivi kama Mungu hayupo ulimwengu ulitokea wapi?
Ukiwa hujui square root ya mbili ni nini, ni lazima square root ya mbili iwe kumi?

Nikikwambia mtoto wa miaka mitatu hawezi kuwa baba mzazi wa mtu wa miaka hamsini, ni lazima nimjue baba wa huyo mtu wa miaka hamsini?

Mimi nakwambia katuni mtoto wa miaka mitatu hawezi kuwa baba mzazi wa mtu wa miaka hamsini (kwa sababu ya timeline contradiction).

Wewe unaniuliza, kama hiyo katuni mtoto wa miaka mitatu si baba wa huyo mtu wa miaka hamsini, baba yake huyo mtu wa miaka hamsini ni nani?

Sijui, na sihitaji kujua baba yake mtu mwenye miaka hamsini ni nani ili nijue kwamba mtu mwenye miaka mitatu hawezi kuwa baba mzazi wa mtu mwenye miaka hamsini.

Ukweli kwamba simjui baba halisi wa mtu wa miaka hamsini, haunizuii kujua kwamba mtoto wa miaka mitatu hawezi kuwa baba wa mtu wa miaka hamsini. Kwa sababu ya timeline contradiction.

Ukweli kwamba sijui ulimwengu umeanzaje, haunizuii kujua kwamba haujaanzishwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa sababu Mungu huyu dhana ya kuwepo kwake inaji contradict yenyewe, na hivyo hawezi kuwepo.
 
Mkuu wewe huwa unatushinda kwa kutuwahi kuwa tuthibitishe uwepo wa Mungu ila na mimi nikikwambia unithibitishie kuwa vilivyopo duniani vimejiumba vyenyewe basi ugumu utakaokutana nao ndio huo nasi tunakumbana nao kukuthibitishia uwepo wa Mungu.
Kwani kusema Mungu hayupo maana yake ni lazima vilivyopo duniani vimejiumba vyenyewe?

Where does this mutual exclusivity come from?

Kwani hili swali ni sawa na kurusha shilingi, useme isipoangukia kichwa, itaangukia mwenge?

Kwa nini majibu yawe mawili tu, vitu kuumbwa na Mungu, au kujiumba vyenyewe?

Unaelewa unalazimisha kuwepo na muunganiko katika mambo ambayo hayana muungano?

Unaelewa hapo ni sawa na mimi nimekataa kwamba katuni mtoto wa miaka mitatu hawezi kuwa baba mzazi wa mtu mwenye miaka hamsini, halafu wewe unaniuliza nithibitishe kwamba huyo mtu wa miaka hamsini alijizaa mwenyewe.

Kwani mimi nimekwambia alijizaa mwenyewe?

Mimi nimekwambia tu kwamba katuni mtoto wa miaka mitatu, hawezi kuwa baba wa mtu wa miaka hamsini.

Sijakwambia kwamba baba wa miaka hamsini kajizaa mwenyewe.

Sasa utanitaka vipi nithibitishe baba wa miaka hamsini kajizaa mwenyewe, wakati mimi sijasema hilo.

Mimi nimesema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo. Sijasema vilivyomo kwenye ulimwengu vimejiumba vyenyewe.

Sasa wewe badala ya kunibishia kile nilichosema, kwamba Mungu hayupo, unaenda kuchukua kitu ambacho sijasema (habari ya vilivyomo ulimwenguni kujiumba vyenyewe) na kunitaka nithibitishe.

Nikikutaka wewe uthibitishe kwamba wewe ni mtoto wa Donald Trump, kitu ambacho hujadai, utaona nakutendea haki?
 
Endelea kupuyanga tu...
Hizo zoote ni story za kufikirika tu.

You don’t need religion to have morals. If you can’t determine right from wrong then you lack empathy, not religion.
 
Back
Top Bottom