Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

NDIYO na SIYO..!

Najua hutaelewa maana kichwa chako kitakuwa kidogo. Iko hivi Mungu ni chanzo cha kila kitu hapa duniani na mbinguni ila sasa kwasababu na makusudi maalum.

Kitalaam( sheria&law philosophy) waliosoma criminology wanajua kuwa ni sheria tu, inayoweza kuunda/kuumba kosa. Kwa msingi huo nasema dhambi ni kosa au crime kwa Mungu na hakuna dhambi ambayo haivunji AMRI/SHERIA ZA Mungu rejea vitabu vya sheria ya Musa(vitabu vitano vya mwanzo katika agano jipya).

Pili siyo Mungu aliyeumba dhambi Mungu kaumba sheria na kuziwekea utaratibu wa kuzitekeleza siye tunaozivunja ndiyo waumba dhambi, ingawa Shetani anasingiziwa kila kukicha.

Bila shaka nimejibu kwa ufupi.
Swali- je kusingekuwa na hizo sheria nini kingetokea?
 
kutenda dhambi au wema kuko ndani ya uwezo wa mwanadamu mwenyewe na si Mungu na nakazia kwa kusema Mungu yeye ni mtakatifu na mtenda mema mara zote
 
Kasoro inaangaliwa kile kibaya kilichofanywa. Kama hakuwa na kasoro asingepingana na Mungu. Angelikuwa ameumbwa kwa ukamilifu asingekuwa na uwezo wa kuasi. Mungu anaunda hardware na kisha yeye huyo huyo ndiye anaweka na operating system kwenye hiyo hiyo hardware aliyoiunda. Kama operating system ipo strong, haiwezekani kuingiwa na virus na kisha ikatenda kazi kinyume na ilivyopangwa.

Operating system ni sawa na huo utashi kwa binadamu. Mungu ndiye aliyepanga Lucifer afanye vile alivyofanya kwasababu hana uwezo kumzidi Mungu. Kwani Mungu hakujua wakati anamuumba lucifer kwamba kutokana na huu utashi niliyomwekea lucifer (jina la baada kuasi) mbeleni atafanya tukio fulani?

Kama alijua kwanini hakuchukua hatua ya kumwekea utashi usioweza kufanya hilo tukio baya mbeleni?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo unata kusema kuwa akili/utashi tuliopewa ni makosa ya MUNGU MWENYEZI?
Yaani kama ingewezekana asingeweka kabisa kitu utashi?

Huoni kuwa angekuwa hajakutendea haki ya kukupa Uhuru?Sasa si tungekuwa kama robots ambazo hazina hiari ambazo ukiziamrisha zikafanye chochote haziwezi kuhoji kama kuna madhara au faida?
Yaani unavyosema angemset ibilisi kwa namna ambayo asingeasi ina maana hapo neno hiari kwa ibilisi lisingekuwepo.Maanake ibilisi angekuwa kama robots.
Sasa MWENYEZI MUNGU hapendi kulazimisha.Ndio maana akakupa hiari ili ujichagulie mwenyewe.

Tena unatakiwa umshukuru sana maana utashi aliokupa ndio unaokusaidia kuchagua eidha kumwabudu au kutokumwabudu,kuhoji au kutohoji,kupuuza mambo au kuyatilia maanani.
Akaona haitoshi,amekupa na sheria za kufuata ili uishi maisha yasiyo na madhara kwako na kwamba ukizikiuka utaishia pabaya.Tena amekupa na nafasi ya kutubu endapo utakosea kwa bahari mbaya.

Sasa iweje ukikiuka hayo maagizo useme eti yeye ana makosa wakati kila kitu amekupa?Huo si utakuwa uzembe wa kiwango kikubwa?Yani ufanye makosa alafu umlaumu MUNGU MWENYEZI?

Tatizo letu ni kwamba tunapofanya makosa tunatafuta pa kuzitupia lawama (Kwa kesi hii utasema isingekuwa utashi nisingekosea) badala ya kuomba msamaha. Wakati huo tunsahaukuwa huo utashi tunaoulaumu ndio pia umetuwezesha kujua kuwa tumefanya makosa.

Nakushauri usitafute kisingizio mkuu.MUNGU MWENYEZI NI MKAMILIFU NA AMEKUFANYIA MEMA MENGI.

EE MUNGU MWENYEZI TUSAMEHE WAJA WAKO MAANA SI KWA HIZI KUFURU TUNAZOKUTENDEA.

Huo uhuru unakujaje ilihali wakati anamleta binadamu hakukuwa na makubaliano ya kuchagua kwamba unataka uletwe duniani au hutaki?
2. Umezungumzia swala la utashi, je binadamu wote wana utashi ulio sawa au unatofautiana?

3. Je Mungu anapenda na kufurahia binadamu watende dhambi? Mfano wakati anamuumba k2206 alijua kabisa kabla hata ya kumleta duniani kwamba kwa utashi niliyomwekea huyu k2206 atachagua mambo kadhaa wa kadhaa ambayo yatampeleka motoni. Je hapo k2206 akija duniani
atakuwa kinyume na matarajio ya Mungu au atapita mule mule kama Mungu alivyotaraji?

4. Je wewe kwa ridhaa yako unapenda kutenda dhambi? Na je Ukijitathmini toka asubuhi kunakucha hadi usiku unapolala hakuna kosa lolote ulilotenda kinyume na Mungu? Kama lipo, je unadhani kuna nini ndani yako kinachokupelekea kutokuwa mkamilifu kwa asilimia 100?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu, nikuulize hivi!
Je, unaweza kutenda dhambi pasipo kushawishiwa na shetani?

Kwa Maelezo yako, MUNGU siyo kisababishi cha dhambi?
Jiulize iwapo MUNGU asingemuumba shetani dhambi ingetoka wapi?

Mtiririko ni kama huu:-

MUNGU > Shetani> dhambi.

Ukimuondoa MUNGU kwenye huo mlinganyo INA maana dhambi isingekuwepo,
Ndiyo, tunaweza kufanya dhambi pasipo kushawishiwa na shetani, kwani shetani kama ilivyo kwa mwanadamu, alishawishiwa na tamaa zake mwenyewe za kupenda ukuu, na yeye akatumia uwepo wa tamaa hiyo kwa mwanadamu kumshawishi. Mungu aliweka ubaya na wema na akaweka utashi kwa viumbe vyake vya mbinguni na kwa wanadamu kuchagua wema na ubaya. Kwa maneno mengine ubaya ulikuwepo kabla ya shetani ndo maana shetani aliuchagua. Alichofanya shetani ni kumwambia mwanadamu ukweli wa kilichokuwa nyuma ya sheria halafu mwanadamu akaamua kusikiliza na kuvunja sheria aliyokuwa amewekewa.
 
Sijaweza kupitia michango yote kwa hiyo inawezekana mtazamo wangu ukafanana na mingine hapa kuhusu swali la tatu kwamba MUNGU ALIMUUMBA MWANADAMU ILI AISHI MILELE? Jibu langu ni kuwa hapana. Mwanadamu hakuumbwa aishi milele angalau katika namna ya mwili. Mwili uliumbwa kwa malighafi isiyo ya kudumu - udongo. Na Mungu katika kuweka misingi ya nchi asingeendelea kuumba udongo bali vilivyoumbwa kwa udongo vingekufa ili udongo uendelee kuwepo. Tulitoka mavumbini na mavumbini tutarudi.

Nikisoma kitabu cha Mwanzo baada ya babu na bibi kuasi, Mungu alishauriana na wenzie akisema kuwa wale viumbe wameshakuwa kama wao - yaani sasa wanajua baya na jema. Wakiwaacha bustanini wanaweza kula tunda la mti wa uzima na kuishi milele kama wao, hivyo wakawatimua bustanini na kuuzungushia ulinzi mkali ule mti wa mzima.

Tukimwangalia Mungu kama roho na mwanadamu kama roho, ndiyo, Mungu anataka mwanadamu aishi milele. Yaani aishi kwenye wema maana Mungu ni wema. Kwa nini aliumba ubaya? Kwa sababu bila ubaya hakuna wema, bila wema hakuna ubaya. Tafsiri yetu ya ubaya ndiyo inatuletea huzuni.
 
Umekiri "ubaya" au dhambi ilikuwapo kabla hata ya shetani, je, Nini kilikuwa chanzo Cha huo ubaya?
 
Nimekiri ubaya ulikuwepo hata kabla ya shetani ila wewe ndiye unayesema ubaya=dhambi. Ubaya si sawa na dhambi. Dhambi ni kuasi, yaani kuchagua ubaya. Chanzo cha ubaya ni Mungu mwenyewe. Swali ni kwa nini aliuweka ubaya?
 
Ikiwa ni hivyo, kwanini Mungu aliweka/otesha mti wenye matunda ambayo baadae yalimsababishia mwanadamu anguko?

Huo mti wa mema na mabaya ulikuwa na faida gani bustanini tofauti na kuwa mtego wa kumwingiza mwanadamu kwenye anguko la dhambi?
 
Nimekiri ubaya ulikuwepo hata kabla ya shetani ila wewe ndiye unayesema ubaya=dhambi. Ubaya si sawa na dhambi. Dhambi ni kuasi, yaani kuchagua ubaya. Chanzo cha ubaya ni Mungu mwenyewe. Swali ni kwa nini aliuweka ubaya?
Kwani ubaya ni Nini?
 
Inawezekana labda hatuna uwezo wa kumuelewa Mungu.

Sio uwezo,watu hawataki kumjua Mola,halafu ajabu wanamjadili.

Kumjua Mola kunataka elimu na tafakari ya kina sana.

Huwezi kumjua Mola nje ya njia hizi tatu :

1. Hawasi 2. Akili 3. Ufunuo.

Na huwezi kumjua mola katika mintarafu matendo ya mwanadamu nje ya vitu hivi vinne :

1. Elimu ya Mola,yaani kujua kwake.
2. Uumbaji wake.
3. Kuandikwa kwa matendo ya mwanadamu na majini
4. Matakwa yake na matakwa ya viumbe.

Na kila moja katika hayo niliyo yataja yana maelezo ya kina.

Lakini nakupa faida moja tu,kama Mola ndio aliyeumba na kumiliki kila,vipi litokee jambo ambalo yeye hataki litokee ?

Ukiona jambo limetokea ujue ametaka litokee na ukiona jambo halijatokea ujue hajataka litokee. Hivi ndivyo tunaweza kumjua Moa kwa kuanzia.

Nipo .....
 
Kilichobaki tunatakiwa kuishi kwa imani tu..Kwa hakika mimi naweza Kusema Mungu ana upendo sana na anatupenda sana.

Na hata mtu ukafa ukaenda motoni au paradise hakika unastahili sana unapoenda.Maana unastahili kulingana na ulichokuwa unafanya hapa duniani.
Ukienda paradiso ni kwa uamuzi wa mwenye paradiso yake tu maana hakuna anayestahili kwenda huko. Musa na kazi yote ile aliyoifanya alistahili kweli kutokuingia nchi ya ahadi aliyoihangaikia kwa miaka 80 kisa kosa moja halafu yule mwivi msalabani akaingia paradiso kwa kutubu dakika ya mwisho?
 
Sio uwezo,watu hawataki kumjua Mola,halafu ajabu wanamjadili.

Kumjua Mola kunataka elimu na tafakari ya kina sana.

Huwezi kumjua Mola nje ya njia hizi tatu :

1. Hawasi 2. Akili 3. Ufunuo.

Na huwezi kumjua mola katika mintarafu matendo ya mwanadamu nje ya vitu hivi vinne :

1. Elimu ya Mola,yaani kujua kwake.
2. Uumbaji wake.
3. Kuandikwa kwa matendo ya mwanadamu na majini
4. Matakwa yake na matakwa ya viumbe.

Na kila moja katika hayo niliyo yataja yana maelezo ya kina.

Lakini nakupa faida moja tu,kama Mola ndio aliyeumba na kumiliki kila,vipi litokee jambo ambalo yeye hataki litokee ?

Ukiona jambo limetokea ujue ametaka litokee na ukiona jambo halijatokea ujue hajataka litokee. Hivi ndivyo tunaweza kumjua Moa kwa kuanzia.

Nipo .....

Ukweli hatuna uwezo wa kumjua Mungu. Elimu ya Mola, viumbe, maandiko na matakwa yake kwa viumbe vinaweza tu kuthibitisha kuwa kuna NGUVU KUU katika vyote hivi ila haichunguziki wala kueleweka. Ndiyo maana tunaishia tu kujifariji kwa kusema kazi yake haina makosa, yeye ndiye mwamuzi wa yote, atabaki kuwa Mungu n.k.
 
Ukienda paradiso ni kwa uamuzi wa mwenye paradiso yake tu maana hakuna anayestahili kwenda huko. Musa na kazi yote ile aliyoifanya alistahili kweli kutokuingia nchi ya ahadi aliyoihangaikia kwa miaka 80 kisa kosa moja halafu yule mwivi msalabani akaingia paradiso kwa kutubu dakika ya mwisho?
Musa aliikosa nchi ya ahadi ila alipokufa alienda paradise.
 
Asante mkuu kwa kujibu!

Kwanza kabla ya kutoa hoja zangu, namimi niseme kitu!
Unajua mkuu, haya mambo ukiyajadili bila kuegamia upande wowote yanaleta raha sana. Kwa kweli kwangu mimi ni burudani tosha hii ninapoona watu kila hoja inayotolewa lazima ihojiwe. Safi sana na huu ndio u great thinker, hakuna kukubali kirahisi rahisi.

Sasa niende kwenye hoja!
Hili la kwanza unalozungumzia, ni kuwa kadiri ya wanaoamini Mungu, ni kuwa Mungu hana mwanzo wala mwisho, maana yake ni wa milele. Yaani kabla ya kuumba hata kitu kumoja, tayari alishakuwepo kwa kipindi Infinity kurudi nyuma. Sasa atuwezi tukasema kipindi infinity ni muda gani kwa kutaja kwa namba!! Yaani ni muda usiotamatika!!. Ona ilivyongumu ku visualize!!

Hoja yako ya pili, mkuu kadiri ya imani yako ni kuwa Mungu ni chanzo cha vitu vyooote. Sasa hapa pia tutahitaji utuelezee, Je, chanzo cha chanzo hicho ni kipi!?
Ndio, kila chanzo kina chanzo, angalia mfano huu, labda tuseme Chanzo cha kifo cha John Doe ni ajali, chanzo cha ajalu hiyo ni mwendo kasi wa dereva, chanzo cha mwendo kasi huo ni kulewa, chanzo cha ulevi wa dereva ni stress, chanzo cha stress, ni usaliti wa mkewe, chanzo cha usaliti wa mkewe ni... chanzo chanzo chanzo mpaka mwisho, na kujirudia rudia humohumo.

Mambo haya yanafurahisha sana!!
Yeye anaitwa kisababishi kisichosababishwa - the uncaused causer.
 
Back
Top Bottom