Saguda47
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 10,766
- 18,620
Wakuu hamjambo!
Kama kichwa cha Uzi huu kinavyouliza, Mimi nikiri kuwa naamini uwepo wa Mungu mmoja aliyeumba vyote vinavyoonekana na visivyoonekana pia.
Katika vitabu mbali mbali vya dini, tunaelezwa kuwa dhambi ilitokana na uasi alioufanya shetani dhidi ya Mungu, biblia inaenda mbali kwa kudai kuwa vita vilipiganwa huko mbinguni na shetani alishindwa na akatupwa duniani akiwa na theluthi ya malaika wakawa upande wake.
Maswali:
1. Ikiwa kabla ya shetani kuasi hakukuwa na dhambi yoyote ile, tena alikuwa mbinguni kwenye utakatifu wa MUNGU, je shetani alishawishiwa au alitoa wapi mawazo ya uasi Ikiwa hakukuwa na shetani yeyote mwingine?
2. Kama MUNGU hujua mwanzo hata mwisho wa viumbe vyake, INA maana alikuwa anajua kuwa shetani atakuja kuasi baadae na kusababisha dhambi, kwanini alimuumba?
Jambo la kufikiria hapa ni kuona kwamba MUNGU alimuumba shetani/Lucifer ( dhambi) mahususi ili kuja kuwa upande maovu. Dhana hii inadhihirisha kuwa MUNGU ndie aliyeumba dhambi.
3. Je, lengo la MUNGU lilikuwa mwanadamu aishi milele bila kufa?
Hapa kuna mazoea yalishajengeka hasa kwa wakristo na waislamu kuamini kuwa isingekuwa Eva/Hawa kudanganywa na Shetani basi Leo hii wanadamu wasingekuwa wanakufa ( immortal). Hii dhana haina mantiki hasa ukiwaza kuwa wanadamu wangezaliana na kuishi milele bila kufa nadhani dunia ingekuwa imejaa mabara na visiwa vyote.
Hivyo MUNGU akaamua kuleta mauti ili kudhibiti ( control) idadi ya wanadamu duniani isizidi uwezo wa rasilimali zilizopo, fikiri Leo hii watu wanauwana kugombania ardhi je ingekuwaje akina Adam na bibi yetu Eva wangekuwepo wote?
4. Je, Dini ni matokeo ya mwanadamu kumhofia shetani?
Tunaishi katika jamii ambazo kila MTU ana juhudi za kujikwamua kuondokana na shida Kama magonjwa, njaa, vita, ambazo Mara nyingi wanadamu wanahesabu kuwa hayo yote ni sababu ya shetani, na dini wanaona ndio kimbilio ili kumkwepa shetani asiwadhuru.
Lakini wao wanaamini kuwa wanasali ili kumtukuza MUNGU, lakini kiukweli dini ni hofu ( fear of unknown) isiyo na ithibati yoyote.
5. Je, Mungu anawapenda wanadamu? Hapa jibu laweza kuwa ni ndiyo, bahati mbaya sana ukiangalia uhalisia toka zamani kuna ugumu wa kusema ndiyo au hapana.
Tunaambiwa kuwa mbinguni kulikuwa na vita Kali sana, mwaishowe malaika aitwaye Mikaeli alimshinda shetani, Mungu akamtupa ibilisi huyo huyo duniani kwa wanadamu anaowapenda sana. Mungu hakuona sehemu nyingine ya kulitupa hilo joka ila duniani ambako ndio wanadamu aliwaweka. Hii ni sawa na kuwarushia watoto wako furushi lenye nge wengi huku umewafungia chumbani na kuwataka wajikinge wasing'atwe hata kidogo.
Nimekuja kuamini kuwa: MUNGU yupo ila dini zote ni michezo ya kukamata fikra za wanadamu tu, inawezekana kabisa kuwa dini ziluletwa na shetani mwenyewe ili kuwachonganisha wanadamu wasiishi kwa upendo na amani.
Angalia jinsi Palestine na Israel, syria , Iraq n.k wanavyouana kwa misingi ya dini.
Niishie hapo, naomba waumini/maswahaba mje mtueleze hizi hoja.
Cc: Mshana Jr
Cc: Kiranga
Na wanajamvi wote karibuni.