Je, Mungu ndie alimfundisha Binadamu uinjinia, pale alipokua akimwelekeza Nuhu jinsi ya kujenga safina kwa vipimo ?

Tuliumbwa kwa mfano wake, yote mema tunayoyafanya basi ni faraja kwake na yamebarikiwa. Nuhu alipata maagizo akatekeleza na akabarikiwa yeye na uzao wake.
Great, right in track..!!!
 
Ni kweli maana hata mnara wa babeli ". The tower of Babylon"ulijengwa kwa ustadi mkubwa sana kufikia mita 700
 
Tatatizo lako wewe ni wakala Wa shetani.

Usiniulize kwanini.
Sikuulizi kwa nini, nataka uthibitishe Shetani yupo.

Isije kuwa umeshindwa kujibu hoja, kwa ujinga na uvivu wako ukatumia dhana ya Shetani kama kichaka cha kufupisha mjadala.

Unakuwa kama Bibi mmoja ambaye yeye hata akisahau sehemu alipoweka funguo zake anamtukana Shetani.

Wakati funguo kasahau alipoziweka yeye mwenyewe.
 
zaman ni tofauti na sasa kwa uelewa wangu ile safina ilijengwa kwa uwezo wa mungu na si sayansi ilotumika pale kumbuka hata waliojisaidia kwenye safina dakika ya mwisho ilikuaje,haiwezekani kirahisi tu binadamu akusanye viumbe vyote duniani so amini ilijengwa tu kwa uwezo wa aliye mtuma
 
Nina swali nje ya hii maada ningependa kujua kutoka kwako kaka mkubwa.

Una mtazamo gani juu ya uwepo wa aliens?

Je sio kuna uwezekano wa planets zingine kuweza kusupport life?
 
Ni kweli zamani na sasa hivi ni tofauti, chukulia tu maisha ya kuhadithiwa na mababu, karne ya 22 hii tunayoenda ukimfufua mwanadamu wa karne ya 12, akakuta mawasiliano ya video call atakuona wewe ni mchawi kupindukia, na anaweza kukusujudia, huo ni mfano mdogo tu wa binadamu kwamba amepewa akili ya kuchanganua au kujitathmini ( reasoning ), ametokea wapi, kwa nini yupo tofauti na wanyama wengine..?
Tatizo watu baadhi wanasoma rekodi za upande mmoja tu, wakija kwenye mjadala Kazi ni kupinga tu, wanaitupa ile reasoning, ambayo ndio imewafanya hata wajue kusoma na kutumia simu. Ambapo ndio funguo ya kutafuta elimu na kujielewa.
 
Nina swali nje ya hii maada ningependa kujua kutoka kwako kaka mkubwa.

Una mtazamo gani juu ya uwepo wa aliens?

Je sio kuna uwezekano wa planets zingine kuweza kusupport life?
Mkuu hakuna kitu kinaitwa Alliens, kwa kuwa kwenye utandawazi huu hakuna cha kuficha, wazungu wana kitu kinaitwa ku " buy time " wanapopanga mikakati yao si chini ya miaka hamsini mpaka mia, wanapoona watu wanawafuata kwa speed lazima wa create vitu vya ajabu ili kuweka delay, kwa maadui wao " kiuchumi" watu wanapohangaikia vitu vya ajabu wenyewe wanamalizia mission zao.mwisho ni kwamba hakuna sayari inayo support life .wazungu walivyokua wa ajabu wangeshaenda kujenga makasino. Au sehemu za kwenda kupumzika.
 
Sikuulizi kwa nini, nataka uthibitishe Shetani yupo.

Isije kuwa umeshindwa kujibu hoja, kwa ujinga na uvivu wako ukatumia dhana ya Shetani kama kichaka cha kufupisha mjadala.

Unakuwa kama Bibi mmoja ambaye yeye hata akisahau sehemu alipoweka funguo zake anamtukana Shetani.

Wakati funguo kasahau alipoziweka yeye mwenyewe.
Hivi ufahamu wako tu, wa kuelewa hiki kibaya na hiki ni kizuri, hakikufanyi ukajiuliza kwa nini unatofauti na viumbe wengine ? Yaani kipo kwako tu wewe binadamu ambaye tunasema uko na akili timamu ? Unajua kusoma, kuandika, na kuweka kumbu kumbu ?
 
Mkuu hakuna kitu kinaitwa Alliens, kwa kuwa kwenye utandawazi huu hakuna cha kuficha, wazungu wana kitu kinaitwa ku " buy time " wanapopanga mikakati yao si chini ya miaka hamsini mpaka mia, wanapoona watu wanawafuata kwa speed lazima wa create vitu vya ajabu ili kuweka delay, kwa maadui wao " kiuchumi" watu wanapohangaikia vitu vya ajabu wenyewe wanamalizia mission zao.mwisho ni kwamba hakuna sayari inayo support life .wazungu walivyokua wa ajabu wangeshaenda kujenga makasino. Au sehemu za kwenda kupumzika.
Mathalani umeambiwa uthibitishe kauli yako kua hakuna Alliens, utaweza???
 
Hivi ufahamu wako tu, wa kuelewa hiki kibaya na hiki ni kizuri, hakikufanyi ukajiuliza kwa nini unatofauti na viumbe wengine ? Yaani kipo kwako tu wewe binadamu ambaye tunasema uko na akili timamu ? Unajua kusoma, kuandika, na kuweka kumbu kumbu ?
Sasa hayo yote yanathibitishaje Mungu yupo?

Na kwa nini watu wanaua, wanaiba, wanadanganya etc, kama wameumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na ujuzi wote, kwa mfano wake?
 
Nimesema binadamu ana akili huru,ya utambuzi. Hapo tu ndipo unajifahamu, na hapo tu ndio umekamilika, una uhuru kamili.
 
Back
Top Bottom